Inashauriwa kutokula chakula kizito mida ya usiku

Sele Mkonje

JF-Expert Member
Oct 2, 2011
643
844
Tuko kwenye dunia ambayo kila kukicha kuna tafiti mpya au tunakumbushwa yale ambayo tunatakiwa kuyazingatia kila siku kwenye maisha.

Na ninafahamu watanzania wengi huchelewa kufika nyumbani na hata kula chakula cha jioni. Kwenye mida ya saa mbili usiku hivi ndio utatukuta chakula kipo mezani lakini Wataalamu wanasema tunakosea kula chakula time hiyo kwa maana chakula kizito mwisho wa kula ni saa kumi na moja jioni na baada ya hapo ni tule vilainilaini tu.

Unaambiwa kuanzia saa kumi na moja jioni na kuendelea hautakiwi kula chakula kizito bali vile vyepesi tu mfano Juice maji na matunda sababu ukila chakula kizito na kulala muda mfupi baadae kitazuia ufanisi wa msukumo wa damu mwilini na mwisho wa siku ndio tunapata magonjwa ya shinikizo la damu.
[HASHTAG]#mckonjetv[/HASHTAG]
 
Hii ni kweli..nadhani pia si tafiti mpya elimu hii imekuwepo mda mrefu sana kuhusu ulaji wa vyakula nyakat za jioni...tatiz na ratiba ya weng baad ya mizunguko ya kazi ujikuta mda huo ndo wako nyumbni...kw lazim tu wale washibe.
 
Back
Top Bottom