The Phylosopher
JF-Expert Member
- Mar 11, 2015
- 1,503
- 2,046
Ndugu wanabodi kama mtakumbuka vizuri, tukiwa mwanzoni kabisa mwa kukabiliana na changamoto ya COVID-19 mwaka uliopita, ni Serikali hii hii iliamuru level seat kwa daladala zote zinazofanya kazi hapa mkoani Dar.
Mara tu baada ya amri hiyo, hali ya usafiri wa umma ilikuwa tete, kwani abiria walikuwa wengi sana, jambo lililopelekea Serikali kuruhusu pikipiki bajaji na gari ambazo ni maalumu kwa kubebea wanafunzi vikaidhinishwa kubebea abiria, ili kujaribu kunusuru hali.
Pamoja na jitihada zote hizo, hali ya usafiri ilibaki kuwa tete. Bado kulikuwa na adha kubwa ya usafiri.
Ilikuwa kawaida sana kusubiri gari kituoni kwa zaidi ya saa nne hadi tano.
Kwa hali ya kawaida miundombinu ya usafiri Dar imezidiwa sana na idadi ya watu, ambapo hata kukiwa kawaida kabisa hali ya usafiri ni tete.
Hapa ndipo najiuliza, ina maana huyu mkuu wetu wa mkoa haijui Dar kweli? Ni kweli covid ni tatizo lkn kwa nini kiongozi anatoa tangazo ambalo halina uhalisia wowote?