Inaniuma sana jamani,mke wangu kaniacha,.

Inaniuma sana jamani,mke wangu kaniacha,.

Hajakukimbia..kaenda Tafuta ahueni ya stress atarudi tu...wewe Tafuta kodi ulipe...

umaskini ukiingia ndani
upendo hutokea dirishani.
kosa pesa ujue tabia mkeo
pata hela ujue tabia za mmeo
mke mwema hutoka mbinguni
mme mwema hutoka benki na MPESA,TIGO PESA NK
 
.....unamaanisha uwe na genge lako sio!!?? Hapa ndipo unapokosea, tena sana! Sio lazima uwe na mtaji wa kuanzia. Unaweza kwenda kuomba kazi ya usaidizi kwa mkaanga Chipsi, kama ni sehemu inayochanganya unaweza lipwa buku tano kwa siku na kula unakula hapo.
nimehangaika sana na najitahidi na vibarua vya hapa na pale mke wngu ale mwanangu avae na nauli za kila siku,ila mambo yanazidi kubadilika,maisha yamebadilika jamani..
 
kiukweli sikua serious nilifanya tu kupoteza mawazo,maisha yananichanganya sana,

na kama pia haupo seriours tutajuaje?
lakin pole ni maisha ndivyo yalivyo na changamoto zake.wakati wewe uko kwenye hali hio kuna mtu anazo pesa lakini yuko na maradhi au anauguliwa au shida yoyote ili mradi tu changamoto ziwepo katika maisha,haijalishi ni mwenye mali au asie nilazima kuupitia msoto. vumilia tu na hio hali wakati uki mtanguliza MUNGU nae atakunekania,shida iliotokea leo haitayafanya maisha yaishe bali yataendelea,jua litakucha na litakuchwa pia,bidii ni ustahimilivu.ina aminika MUNGU hatoi jaribu linalo mshinda mtu uwezo wa kulibeba. mtumainie MUNGU, angaika huko na huku kutafuta chakufanya, vumilia, na usiuruhusu moyo wako kuwazia kushindwa bali wazia MUNGU amekunusuru na magumu mangapi sembuse hili. kila la heri ndugu na Mwenyezi MUNGU akutie nguvu.
 
Mkuu ipo siku yule atoaye riziki atakuheshimisha. JF ni nyumbani naamini kaka na dada watajitokeza
 
Daah nimekuonea huruma hadi basi, sina hata cha kukusaidia but Mungu ni muaminifu atakukumbuka wakati wa shida zako. Pole sana

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
umaskini ukiingia ndani
upendo hutokea dirishani.
kosa pesa ujue tabia mkeo
pata hela ujue tabia za mmeo
mke mwema hutoka mbinguni
mme mwema hutoka benki na MPESA,TIGO PESA NK

Mkono mtupu haulambwi
 
Ukiwa unapata hela jaribu kufanya savings then uanze vibiashara vidogo
 
Maskini pole sana usijali Mungu atakusaidia utapata kazi
 
Gentleman umeachwa???? pole sana rafiki
 
Back
Top Bottom