Inaniuma, mpenzi wangu anaolewa

Bemendazole

JF-Expert Member
Nov 14, 2020
2,362
5,881
Wana MMU naombeni mnipe tu pole.

Mie ni mtu nisiyeumizwa na mambo ya mahaba, lakini nashangaa kuona huyu single mother niliyekutana nae kwenye pilika za maisha mkoani Mbeya, anaolewa 😥.

Huyu single mother mie nilikuwa ni msafiri na mpitaji ili nililazimika kukaa baada ya kusema amenasa ujauzito. Sasa katika pilika pilika za kulea ujauzito, nikajikuta napata hisia 😀.

Ila baada ya kugundua kuwa naletewa mapicha picha si ndio nikakapiga chini. Ila si haba, kamekula sana vijisenti vyangu vya kila mwezi.

Sasa nimeona picha ze send off yake nimeumiaje? Sijui niende nikafanye vurugu 🤗. Yaani hapa hata sijielewi. Nahisi siku yangu leo imekuwa mbaya kabisa.
 
Lakini kitu ambayo watu wengi hawajui na sisi wanaume hua hatuizungumzii kabisa ni juu ya maumivu makubwa na makali hasa tunapo wapoteza wale tulio wapenda na kudhani kwamba hawana pakwenda ama hawatopata wakuwapenda zaidi ya sisi.
Ukweli ni kwamba wanaume tunaumia sana mioyo kuliko wanawake, na kwetu wanaume hua tunatunza sana haya mambo mioyoni ila tunajikaza tu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom