Inanitisha nisaidieni!!!!!!!!!

Kaka nakupata uzuri sana, ila jaribu kuvaa viatu vyangu....mpaka sasa sijaamua kama nionane naye au lah, ila inatisha

siri kubwa ya ushirikina ni hofu
ukidharau tu utashanngaa.....hakuna cha kuogopa...kabisa
 
onana nae lkn iwe sehemu ya wazi na uwe umeongozana na watu wa karibu.na kama ni kweli alitaka kufanya hivyo c mtu mwema kwako kaa nae mbali.
 
Pole sana Mkuu. Japokuwa umeambiwa kuwa alikuwa anataka kukutoa kafara, lakini huna udhibitisho kama ni kweli. Hiyo inawezekana kuwa ni heasay tuu unless kama una ushahidi mwingine mwingine wa kudhibitisha. Inawezekana ikawa ni kweli ni story nyingine kabisa. Inaonyesha kama alitaka kukuona tokea mapema lakini ndugu zako hawakumpa hiyo nafasi.

Definitely, utakuwa na mixed feelings za kumwona na hilo ni sawa kabisa hasa kutokana na uliyoambiwa. Hilo linaeleweka. Lakini usimhukumu kwa maneno ya kusikia. Kutana nae na msikilize anasema nini unless kama na wewe unaamini sana ushirikina. Then, from there unaweza kufanya maamuzi ya busara na hekima.

Lakini kama walivyoshauri wengine kutana nae kwenye mazingira yaliyo ya wazi na sehemu yenye watu. Ikiwezekana kutana nae in some sort of a meeting na ndugu wengine. Ukiona anasita then jua ana lake. Lakini akikubali msikilize. Hata watu walioua wanapewa haki ya kusikilizwa.

Ukiamua kutokutana nae kama bado ana nia mbaya, bado anaweza kukupata tuu. kwani alipataje namba ya simu yako? Na kama ukiamua kutokutana nae, hakikisha vyombo husika vinajua, just in case anything bad happens to you. Lakini kama nikivaa viatu ningeona kumwona. It is emotional and scaring lakini ni better to find out nini hasa kilitokea.

Kama ukienda tungependa sana kama utatupa feedback.
 
Hahaha, eti kafara...Kwani wewe umekuwa kondoo.

Mimi naona hapo kuna big deal, mama yako mdogo anaificha.
 
Muamini sana Mungu,mimi nakushauri uende kuonana nae ili usikie the other side of the story!lakini uwataarifu ndugu zako na uwape hata namba za huyo anaejiita baba yako.I wish u all the best my dear,May the grace of the lord be with u.
 
Ni kweli inatisha, ni kama mamdogo wako alikwambia ukweli, ni kwanini wasite kukwambia kilichotokea hadi huyo anayejiita babako awasiliane nawe? hivyo basi mimi ningekushauri ukubali wito muonane naye, ila kwa angalizo iwe ni sehemu ya wazi, its better the devil u know than the angel u dont know.
 
Usipoonana naye utakaa na duku duku
Just follow 'the rules' changanya na za kwako
And it will be okay.

Kaka nakupata uzuri sana, ila jaribu kuvaa viatu vyangu....mpaka sasa sijaamua kama nionane naye au lah, ila inatisha
 
Kama wewe ni mkristo, Mwambie mkutane Kanisani chini ya usimamizi wa mchungaji/Padri!

Wewe kuwa jasiri nenda kakutane na baba yako, mungu yuko kila sehemu. Huyo amejuta anataka kuungama kwako na kukupatia wosia kabla mola hamjachukua.
 
Pole sana Mkuu. Japokuwa umeambiwa kuwa alikuwa anataka kukutoa kafara, lakini huna udhibitisho kama ni kweli. Inaonyesha kama alitaka kukuona tokea mapema lakini ndugu zako hawakumpa hiyo nafasi.

Definitely, utakuwa na mixed feelings za kumwona na hilo ni sawa kabisa hasa kutokana na uliyoambiwa. Hilo linaeleweka. Lakini usimhukumu kwa maneno ya kusikia. Kutana nae na msikilize anasema nini unless kama na wewe unaamini sana ushirikina. Then, from there unaweza kufanya maamuzi ya busara na hekima.

Lakini kama walivyoshauri wengine kutana nae kwenye mazingira yaliyo ya wazi na sehemu yenye watu. Ikiwezekana kutana nae in some sort of a meeting na ndugu wengine. Ukiona anasita then jua ana lake. Lakini akikubali msikilize. Hata watu walioua wanapewa haki ya kusikilizwa.

Ukiamua kutokutana nae kama bado ana nia mbaya, bado anaweza kukupata tuu. kwani alipataje namba ya simu yako? Kama ukienda tungependa sana kama utatupa feedback.

Mkuu, hizi sehemu nilizoziwacha zinahusika na maoni mabayo ningetoa.
Ezan Mkuu, angalia haya aliyoyasema EMT. Hapa umesikia hadithi ya upande mmoja tu toka kwa wazazi na jamaa zako, lakini hujui chochote toka upande mwengine. Lakini kwa maoni yangu, hadithi uliyopewa na jamaa zako inaficha ukweli wote. Hilo la kuwa alitaka kukutoa kafara inaonesha ni kauli ya chuki juu ya kile baba yako alifanya, kauli ambayo kama ukimwambia mtoto mdogo anaweza kuamini na kuogopa, lakini wewe ni mtu mzima, na sidhani kama unaamini ushirikina. Kama kweli baba yako alitaka kukutoa kafara, sioni kwa nini alishindwa na anashindwa mpaka leo kufanya hivyo. Kwa kuwa alipata nambari yako ya simu, uelewe kuwa anakujua hata unapokaa na nyendo zako zote. Usiogope Mkuu.

Unaweza kufanya yafuatayo:
- Kama unataka kulitatua kwa haraka, nenda kamwone na msikilize, bila ya uoga, wala kumweleza kile ambacho uliambiwa. Sioni mantiki ya kwa lazima uende kumwona mahali palipo na watu, isipokuwa kama huyo baba ni kichaa kweli kweli.
- Kama una wakati wa kufuatilia zaidi, rejea kijijini kwenu na kumwona huyo rafiki wa bibi yako, anaweza akawa na ukwli tafauti na ulioelezwa.
- Njia nyengine, muambie wazi kuwa mnataka mkutane kukiwa na wakuu wa dini au imani yako, iwe kanisani, msikititni au popote.
Mwisho, kama ilivyokwisha semwa, usiwache kumwona bado yupo hai. Kwa vyovyote, huyo ni baba yako.
Kila la heri.

-
 
Ezan,

Fanya hima ukaongee na mzee wako, anaweza akaja akafa ukajutia maisha yako yote.

HIzo mambo hata kama ni kweli ni 34 Years sasa, wewe unaogopa nini ushakuwa mtu mzima nendeni mtafute chobingo muongee

Huyo mtu amesha apologize mara nyingi at least wewe uchukue hatua ya kumsamehe uwajue na ndugu zako wengine

Mtu mzima hatolewi kafara, wala usiende na wapambe nenda wewe mwenyewe
wewe usimpotoshe mwenzio,watu wazima wanatolewa kafara vizuri....na mtu kama anania mbaya na wewe hata kama itapita miaka 50.stil atakifanya alichokikusudia!!
 
Kwa hiyo ni bora nijikalie mbali tu. Maana nisiwe muongo ni kweli namuogopa sana huyu mtu

Ezan:
Mimi nafikiri you dont need kuogopa. Hata kama uamini Mungu, hebu chukua ushauri wa The Boss. Usiogope, ukifanya hivyo unampa nafasi adui kufanya kile apendacho. Kuna wengi wamesema usiende, lakini mimi nasema ni vizuri ungeenda ukamsikiliza. You are a big boy bana, hawezi kukubeba juu juu! Cha muhimu kakutane naye mahali pa wazi ambapo unakuwa na amani. Pole na kila la heri.
 
Kwa kuwa umesikia hadithi za upande mmoja tu na umepata malezi ya upande mmoja tu na sasa ni mtu mzima, ni wajibu wako kuonana nae.

Kwa mtazamo wangu, angekuwa ni mtu mbaya kiasi cha hadithi ulizosikia upande mmoja, asingeweza kushindwa kukupata na kukudhuru kama ingebidi. Ili uwe kwenye amani inabidi uonane nae, msikilize anachotaka kukuambia.

Hata kama alikuwa ni mbaya kweli, binaadam hubadilika. Si vyema kama hautokutana nae na itakutesa zaidi na uoga hautokuishia, uoga utakuishia pale tu utapokutana na kuuona upande wa pili wa shilingi.

Onana nae.
 
  • Thanks
Reactions: EMT

Nimekupata vema Faiza
 
Back
Top Bottom