Inanitisha nisaidieni!!!!!!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Inanitisha nisaidieni!!!!!!!!!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mvaa Tai, Jan 20, 2012.

 1. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #1
  Jan 20, 2012
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  [FONT=&amp]Wana jamvi mimi siyo mwandishi mzuri, wa Story ndefu ila nataka kushea kidogo changamoto/Tatizo nililo nalo na kunisaidia mawazo nini nifanye kwasababu hapa nilipo nimejawa na hasira lakini pia natamani kumuona kwa macho yangu baba yangu mzazi.[/FONT]

  [FONT=&amp]Wadau mwenzenu mpaka sasa nina umri wa miaka 34 nimelelewa na mama yangu toka mdogo mpaka nilipofika form three, nikiwa form three ndipo mama yangu alifariki dunia, wakati wa uhai wake nilishawahi kumuuliza mara mbili kuhusiana na yu wapi baba yangu, mara ya kwanza nilimuuliza nikiwa form one alinijibu kwamba baba yangu yupo mbali sana(kwa maana ya nje ya nchi) ipo siku nitamuona, nilipomuuliza tena nikiwa form two kwamba baba yangu atakuja lini na mbona hata haandiki wala barua? Akanijibu kwa hasira kwamba baba yangu yupo Tanzania ila nimsahau nijikite zaidi katika masomo nikisha kuwa mtu mzima atanipa full story basi sikumuuliza tena.[/FONT]

  [FONT=&amp]Baada ya kifo cha mama nikachukuliwa na kulelewa na Mjomba wangu ambaye amenisomesha mpaka nilipofikia kujitegemea naye alifariki mda mfupi baada ya mimi kuanza kazi. Wakati wa uhai wake mjomba nilimuhadithia kwamba mpaka mama anafariki dunia hajanionyesha baba yangu japo alidai yupo hapa nchini, Mjomba alinijibu kwamba yeye anamfahamu tena hata mama akiwa hai baba yangu alikwenda nyumbani kwake mara kadhaa kuomba radhi na kutaka anichukue akanilee lakini akadai wao walikataa kata kata kutokana na kwamba baba yangu siyo mtu mzuri na ilikuwa ni hatari sana kwa mimi kuishi naye nikiwa bado mdogo ila na yeye pia aliniahidi kwamba nikisha kuwa mtu mzima na familia yangu atanipa full story.[/FONT]

  [FONT=&amp]Mara kadhaa nimekuwa namuomba mama mdogo anipe story kuhusiana na Baba yangu kwani hata yeye anamfahamu na ndiye mtu pekee aliyebaki mtu mzima katika familia yao anayeweza kufahamu hili, lakini huwa ananigomea anadai hiyo ni ishu kubwa sana hawezi yeye akaniambia kwasababu naweza ku-react nikafanya maamuzi ya kutisha then yeye hataeleweka katika jamii, sana sana huwa ananisihi nimpotezee tu niendelee na ishu zangu.[/FONT]

  [FONT=&amp]Hivi karibuni nilienda mkoani kwetu nikafika kijijini wanakotoka marehemu bibi na babu yangu nilikutana na bibi mmoja(niliambiwa alikuwa rafiki yake na marehemu bibi) mama mdogo akanitambulisha kwa huyo bibi, yule bibi akastuka na kuonyesha kanikumbuka then akaanza kulia. Kuna watu wazima wawili wakamchukua pembeni sijui walikuwa wanaongea naye nini kimyakimya, baadaye akarudi akiwa halii tena ila kuna kila dalili kwamba alikuwa anajizuia kufanya hivyo na kuna jambo baya sana amekumbuka. [/FONT] [FONT=&amp]

  Majuzi nimepigiwa simu na mtu mzima mmoja anadai anaomba nitafute siku tukutane popote pale ana mazungumzo na mimi ya mda mrefu sana, nilipomuomba aniambie yeye ni nani akajibu yee ni baba yangu, nikastuka sana ila nikajikaza kiume nikamwambia mimi simfahamu baba yangu, akanijibu una haki ya kusema hivyo ila ni habari ndefu sana nijitahidi nifanye tuonane tuzungumze, nikamuahidi nitampigia nikipata mda, bila kuchelewa nikampigia simu mama mdogo na kumtaarifu hili suala, yeye akastuka na akanijibu kwa kuhamaki kwa kifupi tuu kwamba niwe makini na huyo mtu siyo mtu mzuri, akanipa story ndefu ya kutisha kwa kifupi ni kwamba baba yangu alifanya jaribio la kunitoa kafara nilipokuwa mchanga kwa ajili ya biashara zake kwasababu yeye ni miongoni watu wenye imani za hivyo, sitaweka kila kitu hapa natakiwa niandike kitabu. Ila mama mdogo kanishauri kwasababu nimekuwa mtu mzima nichanganue mwenyewe.

  Hii imenistua naogopa sana kuonana na huyu mtu.[/FONT]
  [FONT=&amp]Nisaidieni wanajamvi hili suala nili handle vipi?[/FONT]
   
 2. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #2
  Jan 20, 2012
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Pole sana Ezam ninachoweza kukwambia sasa kwa sababu wewe ni mtu mzima 34 years unajua jema na baya,
  Kama una nia ya kumuona baba yako wewe panga nae mkutane ,ila sehemu yenyewe iwe ya wazi na mazingira yaliyo na watu kabisa ama unamwambia hata rafiki yako anakuwa katika mazingira utakayokuwepo,
  Inawezekana sasa baba yako alishagundua alilotaka kufanya halikuwa sahihi na moyo wake unamsuta
  Anaweza kuwa anakutafuta akuombe samahani..Jipe moyo wa kiume na ukubali wito,ili angalau moyo wako uwe free na uweze kumjua baba yako.
   
 3. M

  MUMY A JF-Expert Member

  #3
  Jan 20, 2012
  Joined: Jan 10, 2012
  Messages: 234
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  umesema alikua antaka kukutoa kafara???yawezekana bado ana nia hiyo,so ukionyesha pua yako tuu,bas na jina lako litabadilishwa.......cha msingi kaa nae mbali ikiwezekana na namba ya simu badilisha maana anaweza kukutumia msg za vitisho
   
 4. Gaga

  Gaga JF-Expert Member

  #4
  Jan 20, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,565
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Loooo jamani haina maana ya kuonana na mtu ambaye hakuona thamani yako kama mtoto wake, sasa hivi ndio ataonaje umuhimu wako, endelea na maisha yako achana naye, hata Mungu hatakuhukumu kwa hilo
   
 5. Keren_Happuch

  Keren_Happuch JF-Expert Member

  #5
  Jan 20, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 1,880
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Pole sana Ezan.

  Naungana na FL1, ni ushauri mzuri. Usiache kumshirikisha Mungu kwa swala hili.
   
 6. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #6
  Jan 20, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,036
  Trophy Points: 280
  mmmh......onana nae lakini iwe sehemu ya wazi na uwataarifu baadhi ya watu wako wa karibu kuhusu mkutano huo....
   
 7. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #7
  Jan 20, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  Shika imani yako asije mwovu akaichukua.
  Huna haja ya kuogopa, akiyezuia asikutoe kafara ukiwa defensiless atakusaidia na leo.
   
 8. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #8
  Jan 20, 2012
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,076
  Likes Received: 1,812
  Trophy Points: 280
  Mpotezee ....
   
 9. Annael

  Annael JF-Expert Member

  #9
  Jan 20, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 13,340
  Likes Received: 10,444
  Trophy Points: 280
  Sasa hapa kunakitendawili. wewe nenda ukasikie anachosema. Nadhani hayo mambo yakwamba alitaka kukutoa kafara achana nayo wala usiyaweke moyoni. Maana kama agetaka kukutoa kafari agekutoa tu zamani. Unajua si kilakitu unachoambiwa uamini. Inawezakuwa ugomvi wao tu.

  Nenda ukamuone sawa?
   
 10. Cantalisia

  Cantalisia JF-Expert Member

  #10
  Jan 20, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 5,229
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Pole sana mkuu
  Kiukweli inaogopesha sana tu na sio kidogo,
  Ila muweke mungu mbele nenda kaonane naye but ukiwa na watu wa karibu yako maeneo hayo mtakapokutania,
  Itakuwa vizuri ikiwa sehemu ya wazi,msikilize nae upande wake km ulivosikia kwa upande ule mwingine,
  Kwa kuwa ww ni mtu mzima na kwa maongezi yake hope utajua upime vp hizo pande zote mbili,
  Ila tu uwe makin km wadau walivosema na uepuke kutoa detail zako mapema km sehemu unapoishi,oficn na kadhalika mpaka utakapoiridhisha nafsi yako juu ya mtu huyo.
   
 11. Edward Teller

  Edward Teller JF-Expert Member

  #11
  Jan 20, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,818
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  kama muda wote huo amekiuwa kimya na maisha yako yamekwenda vyema-sioni haja ya wewe kumtafuta,maana uanweza umuone then akuongezee matatizo zaidi,ujute kwa nini ulijichichanganya naye,kama kila mtu anamuogopa,atakuwa ni mtu hatari,na abdo hujui kuwa adhima yake ya kukutoa kafara ipo au alishaifuta,
  kumbuka kama ni mpenda ushirikina sana,kama aliwapa ahadi hao wakuu wake kuwa atakutoa wewe-basi hana budi kufanya hivyo.
  TAKE CARE
   
 12. isamilo1982

  isamilo1982 Member

  #12
  Jan 20, 2012
  Joined: Jan 17, 2012
  Messages: 55
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kataa neno kubali wito lakini kuwa mwangalifu pamoja na yote yaliyopita huyo ataendelea kuwa baba yako tu mvua inyeshe jua liwake,akili ku mkichwa!!!!!!
   
 13. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #13
  Jan 20, 2012
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Hicho kitu ndo kinachanganya Ubongo wangu, huwezi amini sipati usingizi
   
 14. Keren_Happuch

  Keren_Happuch JF-Expert Member

  #14
  Jan 20, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 1,880
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Unahitaji kumtegemea Mungu zaidi kwa ulinzi wake. Kwake hakuna mchawi atakayekuloga. Otherwise, with that fear in you, things will not be ok! All the best.
   
 15. M

  Marsy Member

  #15
  Jan 20, 2012
  Joined: Dec 14, 2011
  Messages: 49
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mpangie mahali pa kukutana na iwe karibu na nyumbani

  kabla ya kwenda nenda kwa walokole wakuombee na kukuzungushia ulinzi ndipo uende

  pili jaribu kuondoa hasira na kumuona na mtu mzuri vinginevyo hasira zako zinaweza kumfanya ashindwe kukueleza ka uadui ukaongezeka
   
 16. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #16
  Jan 20, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  punguza hasira
  what if hiyo story ni ya uwongo ili tu umchukie baba yako?
  nenda kamuone na umwambie hiyo storu huku unamtazama usoni ili ujue ukweli...
  kabla ya kumkasirikia si bora usikie na story ya upande wake???????
   
 17. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #17
  Jan 20, 2012
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo ni bora nijikalie mbali tu. Maana nisiwe muongo ni kweli namuogopa sana huyu mtu
   
 18. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #18
  Jan 20, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  tatizo lako wewe hujui kupambana na ushirikina
  ndo maana ume panick na kuogopa....

  mimi nna ndugu pia washirikina kuliko huyo baba yako...na mpaka leo nikiwaona nawasalimia....

  ili mradi nimewapiga marufuku kuja kwangu na mimi siendi kwao..
  lakini tukikutana njiani tunasalimiana tu....

  hawanitishi hata siku moja....
   
 19. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #19
  Jan 20, 2012
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Kaka nakupata uzuri sana, ila jaribu kuvaa viatu vyangu....mpaka sasa sijaamua kama nionane naye au lah, ila inatisha
   
 20. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #20
  Jan 20, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Ezan,

  Fanya hima ukaongee na mzee wako, anaweza akaja akafa ukajutia maisha yako yote.

  HIzo mambo hata kama ni kweli ni 34 Years sasa, wewe unaogopa nini ushakuwa mtu mzima nendeni mtafute chobingo muongee

  Huyo mtu amesha apologize mara nyingi at least wewe uchukue hatua ya kumsamehe uwajue na ndugu zako wengine

  Mtu mzima hatolewi kafara, wala usiende na wapambe nenda wewe mwenyewe
   
Loading...