Awali ripoti ya wenye vyeti feki ilipotolewa pale Dodoma nilijua ile ndiyo report ya wafanyakazi wote wa serikali. utafiti mdogo niliyofanya ni kuwa kuna baadhi ya taasisi au wizara ambazo hazijakumbwa na hilo zoezi. Nilitegemea katika ripoti iliyotolewa pale Dodoma na waziri husika wa mambo ya utumishi ieleze bayana kuwa uhakiki ule umehusisha wakina nani na nani wameachwa kwa sababu zipi. Sijaona sababu za msingi za kuharakisha ripoti ile kama kulikuwa na sehemu ambazo hazijahakikiwa. Mwanya huu ulioachwa unaweza kusababisha wale ambao wana vyeti vya kughushi watumia kila walezalo kuhakikisha wanajihami. Naamini hili rais hajalijua maana kwa alivyosimama kidete na zoezi hili asingekubali kwani bila kuhakikiwa watumishi wote ni dhahiri kuwa zoezi hili litakuwa ni la kibaguzi.