Inakuwaje pamoja na mbwembwe zote kila mpinzani anayetoka kuhojiwa polisi anaufyata?

Hata hilo nalo hulijui. Kwa sababu ni wapenda amani na wanafuata sheria bila shuruti. Kubambakiziwa kesi hakuna mtu anaweza kuepuka lakini ukishaeleweshwa hili halitakiwi ndio unarudi kwaenye mstari
Nasoma post uchwara na kushushia pop corn
 
Hata hilo nalo hulijui. Kwa sababu ni wapenda amani na wanafuata sheria bila shuruti. Kubambakiziwa kesi hakuna mtu anaweza kuepuka lakini ukishaeleweshwa hili halitakiwi ndio unarudi kwaenye mstari
Hahahahahaaaaa! Kuwahimiza BAVICHA kupambana na polisi mitaani ni kupenda amani?
 
Uwa huna hoja nyingine ya kupost badala ya hizi siasa za utapiamlo? post za majunguu tu ! namhurumia aargh!
 
Uwa huna hoja nyingine ya kupost badala ya hizi siasa za utapiamlo? post za majunguu tu ! namhurumia aargh!
Mkuu, kwani hili si jukwaa la siasa? Sasa unataka masuala ya mapenzi nipost huku?
 
Kumbe lizabon ni mtoto wa kiume hahahahah siku zote hizi nilikuwa najua ni mdada na mada zake za kitaarabutaarabu
 
Kumbe wewe ni mtu mdogo kama piritoni kwenye chama. Maana ungekuwa na unaeleweka, sasa hivi ungekuwa uko wilayani kama DC au DAC ukinunua mahitaji yako kwa ajili ya makazi mapya.
 
Mimi bado sijawaona wapinzani waukweli tanzania hii hawa wote makanjanja tu
 
Nadhani wanasubiri aendelee kujichanganya. Ila jamaa machale yanamcheza. Akiona jinsi vijana wake wanavyoshughulikiwa hakika analazimika kujificha
Hakuna haja; hata wao wanajua wanabwekabweka tu kujitafutia ulaji/umaarufu hakuna mwenye ubavu wala mkakati wa kumkomboa mtu masikini katika wapinzani wote ninaowajua. Nafuu hata huyo Magufuli ashaonyesha uelekeo hata akikwamishwa tutakuwa tushamuelewa
 
Mimi bado sijawaona wapinzani waukweli tanzania hii hawa wote makanjanja tu
Una maanisha wapinzani wanasiasa au wapinzani wananchi?maana kama wananchi tupo na tunajitoa kweli kwa nchi yetu kwa kuchagua upinzani ila serikali yenu inaweledi mkubwa wa kuwadhulumu wananchi wanaoegemea upinzani -rejea uchaguzi wa Zanzibar na uchafuzi wake wa marejeo!
 
Ndugu yangu usiombe kuhojiwa na Polisi, kwani wahojiwa wengine hunusurika kutoa machozi ya damu. Mara nyingi wanajifanya wajanja wakiwa na sisi raia lakini wakiwa kwenye chumba maalumu cha mahojiano wanakuwa wadogo kama punje ya ulezi. Ndiyo maana wakitoka kuhojiwa hawathubutu kurudia tena kuropoka ropoka ovyo.
 
Wadau, amani iwe kwenu.

Kumekuwepo na matamshi ya hawa ndugu zetu wa upinzani kuwa wanaonewa na kwamba polisi inatumika kukandamiza upinzani. Wamekuwa wakisema kwa mbwembwe zote kwamba hawapo tayari kuona jeshi la polisi likitumika kuwakandamiza na kwamba wapo tayari kupambana nao na wengine wamefikia hatua ya kusema wapo tayari kushtakiwa, kufungwa na hata kufa kwa lengo la kutetea demokrasia.

Ila cha kushangaza, hakika yametokea mabadiliko makubwa sana ya kauli za wapinzani. Alianza Lowasa kuwa hatambui matokeo ya Urais mpaka anaingia kaburini. Huyu hajahojiwa lakini ishara zote zinaonesha kuwa amemkubali Rais na sasa ameufyata.

Akaja Zitto Kabwe na madai kuwa Rais ni dikteta na alienda Rwanda kujifunza jinsi ya kukandamiza wapinzani. Baada ya kuhojiwa na polisi, huyu naye ameufyata na sasa amebaki kutweet tu kwenye twitter.

Tundu Lissu aliongea kwa mbwembwe pale Kisutu na madai yake ya Rais Uchwara. Naye licha ya kuahidi kuwa ataendelea kupaza sauti, ni zaidi ya wiki sasa hajaonekana kwenye media.

Freeman Mbowe pia alitokwa mapovu kule kanda ya Ziwa ambako walilenga kufanya fujo. Baada ya kuhojiwa na polisi, hakika amekuwa wa baridi kama maji mtungini.

Kuna Mmasai mmoja anaitwa Ole Sosopi. Huyu ndiye aliyewaamrisha BAVICHA kupambana na Polisi mitaani. Alipokamatwa na kuhojiwa, eti leo hii amekuwa rafiki wa polisi na anasema atashirikiana nao kukwamisha mkutano wa CCM. Leo pia anahojiwa na nina hakika kuwa baada ya hapo atapotea kabisa kwenye majukwaa.

Nilipongeze jeshi la polisi kwa kufanya kazi zao kwa ufasaha na weledi mkubwa. Hawa wapinzani wanajua kuwa wanatenda kosa ila wanatafuta tu kick ya kujulikana mitaani. Nimpongeze pia Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba kwa kuliagiza jeshi la polisi kushughulika na wale tu vinara wa uchochezi na si wafuasi wao. Njia hii inaonekana kufanya kazi kwani tayari wameshaufyata.

Hawa wanaojiita wapinzani inabidi waache mizengwe na drama zao kabisa...wakae kimya waangalie jinsi presidaa anavyopiga kazi bhana, alafu 2019 waje sasa na hoja zao...la sivyo jamaa atawasafisha kabisa, tutakimbiana jukwaani hapa mana jamaa hataniii....na sa hvi amekumbatia vyombo vya dola na taratibu anawasogeza wajanja wa kiisraeli...mnyika alishaliona hilo akapiga kimya, dk slaa mbele, zitto na unafiki wake aende kwao kg, lissu akakamue alizeti huko kwao, mbowe aendelee kusimamia miradi yake ila akumbuke kulipa kodi, na lowasa aende kwao monduli akachunge
 
Back
Top Bottom