Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,894
- 20,375
Wadau, amani iwe kwenu.
Kumekuwepo na matamshi ya hawa ndugu zetu wa upinzani kuwa wanaonewa na kwamba polisi inatumika kukandamiza upinzani. Wamekuwa wakisema kwa mbwembwe zote kwamba hawapo tayari kuona jeshi la polisi likitumika kuwakandamiza na kwamba wapo tayari kupambana nao na wengine wamefikia hatua ya kusema wapo tayari kushtakiwa, kufungwa na hata kufa kwa lengo la kutetea demokrasia.
Ila cha kushangaza, hakika yametokea mabadiliko makubwa sana ya kauli za wapinzani. Alianza Lowasa kuwa hatambui matokeo ya Urais mpaka anaingia kaburini. Huyu hajahojiwa lakini ishara zote zinaonesha kuwa amemkubali Rais na sasa ameufyata.
Akaja Zitto Kabwe na madai kuwa Rais ni dikteta na alienda Rwanda kujifunza jinsi ya kukandamiza wapinzani. Baada ya kuhojiwa na polisi, huyu naye ameufyata na sasa amebaki kutweet tu kwenye twitter.
Tundu Lissu aliongea kwa mbwembwe pale Kisutu na madai yake ya Rais Uchwara. Naye licha ya kuahidi kuwa ataendelea kupaza sauti, ni zaidi ya wiki sasa hajaonekana kwenye media.
Freeman Mbowe pia alitokwa mapovu kule kanda ya Ziwa ambako walilenga kufanya fujo. Baada ya kuhojiwa na polisi, hakika amekuwa wa baridi kama maji mtungini.
Kuna Mmasai mmoja anaitwa Ole Sosopi. Huyu ndiye aliyewaamrisha BAVICHA kupambana na Polisi mitaani. Alipokamatwa na kuhojiwa, eti leo hii amekuwa rafiki wa polisi na anasema atashirikiana nao kukwamisha mkutano wa CCM. Leo pia anahojiwa na nina hakika kuwa baada ya hapo atapotea kabisa kwenye majukwaa.
Nilipongeze jeshi la polisi kwa kufanya kazi zao kwa ufasaha na weledi mkubwa. Hawa wapinzani wanajua kuwa wanatenda kosa ila wanatafuta tu kick ya kujulikana mitaani. Nimpongeze pia Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba kwa kuliagiza jeshi la polisi kushughulika na wale tu vinara wa uchochezi na si wafuasi wao. Njia hii inaonekana kufanya kazi kwani tayari wameshaufyata.