Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 20,915
- 30,259
INAKUWAJE MTU KWA VIGEZO VYOTE NI MWENYE AKILI ZA ZIADA KUMBE MJINGA?
Toka udogo wangu nikipenda senema.
Baba alikuwa na "prejector" nyumbani lakini ni ile "silent," haitoi sauti na filamu zake zilikuwa nyembamba.
Lakini katika miaka ya 1960 na utoto kwangu ile ilikuwa mashine niliyoipenda sana kupita kiasi.
Baba siku akifurahi ataitoa uani na kutuonyesha mimi na rafiki zangu filamu za Charlie Chaplin.
Nakumbuka moja ya filamu tuliyokuwa tunaipenda ni Charlie Chaplin kwa udogo wa mwili aliokuwa nao anaingia ulingoni katika masumbwi kupambana na jitu lililoshiba vizuri.
Charlie Chaplin anashinda pambano kwa "knock out."
Niko Nairobi nakaa 680 Hotel katikati ya mji.
Miaka hiyo hapa nyumbani hali ilikuwa ngumu kidogo na ukifika Nairobi unashangazwa na kila kitu.
Ilikuwa umemtoa mtu upande wa Mashariki wa Ukuta wa Berlin ukamshusha upande wa Magharibi.
Naangalia gazeti la Nation upande wa matangazo ya burudani.
Nikaona kuna movie "Heritage Africa," inacheza Nairobi Cinema.
Hii ilikuwa "theatre" ya sifa enzi hizo.
Nikaenda kuangalia movie hii na hadi leo imenikaa kichwani mwangu.
Kisa cha kijana aliyejaaliwa akili zisizo za kawaida na akasoma vizuri Ghana iliyokuwa chini ya ukoloni wa Waingereza akafika hadi Uingereza.
Kijana akashika nafasi ambayo Mwafrika kabla yake hakupata kufikia.
Kichwa kikatuna akawa Mzungu Mwingereza kupita Mwingereza mwenyewe.
Huyu kijana mama yake alipoona mwanae kafika juu kuliko mategemeo ya mtu yeyote akafunga safari kuja Accra mjini kumkabidhi kijana wake mikoba ya wazee wake waliomtangulia ambao walikuwa watu wakubwa wa kuheshimika katika jamii.
Hii mikoba ilikuwa kitu chenye thamani kinachobeba historia ya ukoo toka enzi na enzi kutoka kizazi kimoja hadi kingine.
Mama akamsisitizia mwanae ahakikishe kuwa hakimtoki anakitunza hadi mwisho wa maisha yake.
Akamwambia katika ukoo wao hiyo ni hazina isiyomithilika na ilipatikana kwenye vita kubwa aliyopigana huyo ambae yeye kachukua jina lake.
Ambacho mama hakujua ni kuwa mwanae hakuwa kama babu zake wakuu waliopita.
Yeye alikuwa Mzungu Mweusi aliyekwisha uhama Uafrika.
Aliitazama ile kinga aliyopokea kwa mama yake na kwake alichokiona ni hazina ya thamani kutoka ustaarabu wa kale wa babu zake unaopashwa kuwa katika maonyesho London, British Museum siyo nyumbani kwake ati ndiyo kinga yake.
Huyu kijana kwa kujipendekeza akampelekea ile hazina District Commissioner (DC) ili aifikishe London kwa wataalamu wa mambo ya kale.
Haukupita muda akavamiwa nyumbani kwake na wazalendo wapigania uhuru kwa nia ya kumuua kwa kuwa yeye alikuwa adui wa wananchi sawa na wakoloni.
Bahati nzuri kwake alinusurika kifo.
Mama yake aliposikia mwanae kanusurika kuuawa akaja mjini kumwangalia.
Akamuuliza, "Kile kitu nilichikupa unacho?"
Kijana akajibu, "Sinacho mama nimempa mkubwa wangu Mzungu akipeleke Uingereza."
Mama alishika kichwa machozi yakimbubujika, "Mwanangu katika ukoo na jamii yetu hapajatokea mtu aliyekuwa na akili zako.
Umeongoza darasani kuanzia darasa la kwanza hadi umekwenda kusoma Ulaya vipi utakuwa mjinga kiasi hiki kukabidhi kinga yetu kwa Mzungu?"
Haukupita muda mrefu kijana aliuliwa na yule yule DC Mzungu aliyempa hazina ya ukoo.
Alikwenda kwake usiku kuidai kinga yake na katika majibizano silaha zilitolewa na ndugu yetu ndiye aliyeuawa kwa kupigwa risasi.
Msomaji wangu hujapata kuona mambo ukajiuliza vipi hili likatendwa na huyu ambae jamii ikimuona ni mtu aliye na akili?
Vipi katenda haya kama jitu ambalo halina elimu yoyote?