Inakuwaje mawaziri kudai hadharani kuwa hawashirikishwi kwenye maamuzi na viongozi wa mashirika yao?

Ungeweka hicho kipengele kinachompa madaraka ya kutoa maamuzi ndo tungekuelewa! Ina maana unapopewa taarifa kama imepinda wewe unakaa kimya tu mpaka watu wafanye maamuzi ndo na wewe ukurupuke kutoka huko utokako? Kwa mfano hiyo barua unayosema pengine ilizungumzia habari za kupandisha umeme kwa nini hakupinga hapo hapo kwamba haiwezekani umeme upandishwe sasa hivi? Yeye zoba anaacha mchakato unaenda mpaka mwisho ndo anazinduka usingizini? Shame on him!
Hapana sheria ya nishati haimruhusu kuzuia mchakato.
 
Tatizo hayo mawasiliano yao wanafanya kwa kiingereza kama vile maombi wanapeleka UNDP kumbe ni EURA tu hapa, matokeo yske sisi wananchi wa kawaida tunashindwa kuwatetea kuwa mkurugenzi hajajiamulia mwenyewe kupandisha umeme alitoa taarifa EURA na wadau walijadili hivyo Rais hapaswi kumtumbua angeagiza tu kwamba umeme usipande kwa sababu jambo la kutaka umeme upande TANESCO hawakufanya kwa kificho. Lakini kwa sababu wanajua sana viingereza kila kitu wanaandika kwa kiingereza mawasiliano yao kwa umma yanaoneka niya kificho ndo maana wanapotumbuliwa hatuwatetei
 
Sheria ya nishati haisemi hivyo mchakato ni tendo huru haliingiliwi na mamlaka yoyote waziri kapewa madaraka hayo na sheria ya ni nishati no 3. Hapo unapingana na mimi na domo langu au unapingana na sheria ya nishati?


Hyo sheria itakuwa na mapungufu sana au tafsiri yako kwa hyo sheria ndo ina mushkeri.

Sheria impe waziri mamlaka ya kupinga matokeo ya mchakato lakini isimpe mamlaka ya kuingilia mchakato hata kama mchakato huo unalitia taifa hasara???

Hizi sheria inabidi ziangaliwe upya
 
Hyo sheria itakuwa na mapungufu sana au tafsiri yako kwa hyo sheria ndo ina mushkeri.

Sheria impe waziri mamlaka ya kupinga matokeo ya mchakato lakini isimpe mamlaka ya kuingilia mchakato hata kama mchakato huo unalitia taifa hasara???

Hizi sheria inabidi ziangaliwe upya
Mchakato hauwezi kuutia hasara taifa kwa sab maamuzi yake hayawi effective mpk waziri aridhie. Ukizuia mchakato ni kuingilia utawala wa sheria na ndio maana sheria imezuia kwani sio kila maamuzi ya mchakato husika yatakuwa mabaya. Na hakuna mazingira ya mchakato kulitia hasara taifa kwa sab mchakato hapa maana yake ni mikutano ya bodi za tanesco na ewura huwezi kuizuia bali unazuia maamuzi yake sasa mikutano(mchakato) hii itaitiaje hasara taifa?
 
Nchi ya wadanganyika ina changamoto zake aisee kw imani yangu wajinga na maskini wakifa hawaendi Mbinguni
 
Hili jambo huwa linajirudia na likishatokea basi kiongozi wa shirika anakuwa kafara hapo hapo na mara zote rais Magufuli amekuwa akimuunga mkono waziri husika.

Alianza Dr. Mwele Malecela wa NIMRI dhidi ya waziri wake Ummy Mwalimu na waziri akatangaza hadharani kuwa hakushirikishwa kwenye utafiti thidi ya homa us Zika nchini. Hali hiyo ilipelekea kuondolewa kwenye nafasi yake kama mkurugenzi wa taasisi hiyo iliyoko chini ya wizara ya afya.

Juzi kwenye swala la umeme ndugu Sospeter Muhongo naye akatangaza kuikana hadharani EWURA na TANESCO kuwa yeye kama waziri hakushirikishwa kwa namna yoyote ile dhidi ya upandishwaji wa bei ya umeme. Waziri huyo akaenda mbali zaidi akiwatuhumu viongozi watendaji wa TANESCO kwa kufanya makusudi kulihujumu shirika. Hali hiyo ikapelekea ndugu Engineer Mramba Feleschemi kung'olewa kwenye nafasi yake hiyo kama mkurugenzi mtendaji wa shirika hilo lililoko chini ya waziri Sospeter Muhongo.

Nini tatizo? Je ni kweli kuwa hawashirikishwi?

Mawaziri huwa wanapanga bajeti za kila mwaka na ndiyo hasa wanaofuatilia utekelezwaji wa bajeti hizo kwenye taasisi zilizo chini ya wizara zao. Sasa watueleze na wao kuwa bajeti zao wanazopanga ni hewa kwakuwa hawashirikiani na viongozi wa mashirika yaliyo chini ya wizara zao? Huenda bajeti ya Sospeter Muhongo aliyoitoa katikati ya mwaka jana ikawa ni bajeti hewa kwani pengine hasa angekuwa amekaa na menejimenti ya TANESCO basi hata swala la gharama za umeme lingejadiliwa kwa kina. Nasema hivyo kwakuwa bei elekezi ilitolewa baada ya bajeti kusomwa.

Kwenye wizara ya afya pengine ndiyo maana kuna hadi matatizo ya chanjo muhimu, yote haya yakiwa ni matokeo ya bajeti hewa isiyoendana na hali halisi ndani ya wizara hiyo na pengine ni matokeo ya mawaziri kutokushirikiana ipasavyo na viongozi wa taasisi zilizo chini yao.

Mwisho niseme kuwa waziri kutoka hadharani na kumkana msaidizi wake wa chini kwenye taasisi anayoingoza yeye tena baada ya kila kitu kuwekwa hadharani ni udhaifu mkubwa na inaonyesha ama kuna usaliti kwa maslahi ya kisiasa ama uzembe wa hali ya juu! Kumvumilia waziri wa aina hii ni sawa na kuhifadhi "kinyesi" kwenye nguo ya ndani kisha ukatembea nacho! Kitakuwa kinaendelea kutoa harufu kali na mbaya na mwisho ile harufu itazoeleka kwa usugu!
kwa sababua hawafanyi kazi wala kufuatilia kinachoendelea, kwa ujumla hawajui wafanyalo.
 
Mchakato hauwezi kuutia hasara taifa kwa sab maamuzi yake hayawi effective mpk waziri aridhie. Ukizuia mchakato ni kuingilia utawala wa sheria na ndio maana sheria imezuia kwani sio kila maamuzi ya mchakato husika yatakuwa mabaya. Na hakuna mazingira ya mchakato kulitia hasara taifa kwa sab mchakato hapa maana yake ni mikutano ya bodi za tanesco na ewura huwezi kuizuia bali unazuia maamuzi yake sasa mikutano(mchakato) hii itaitiaje hasara taifa?


Kwenye hvo vikao vya bodi si ndo wanalipana mamilioni ya posho au...hzo posho si zingetumika kwa mambo mengine au??
 
Kwenye hvo vikao vya bodi si ndo wanalipana mamilioni ya posho au...hzo posho si zingetumika kwa mambo mengine au??
Sasa vikao vimewekwa kwa mujibu wa sheria kwa ajili ya kujadili suala lilopewa baraka na sheria ya nishati waziri hawezi ku pewa madaraka ya kuzuia kikao haiwezi kuwa mantiki hata kidogo ni vizuri sheria yenyewe izuie vikao hivyo.
 
Back
Top Bottom