G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,772
- 36,664
Hili jambo huwa linajirudia na likishatokea basi kiongozi wa shirika anakuwa kafara hapo hapo na mara zote rais Magufuli amekuwa akimuunga mkono waziri husika.
Alianza Dr. Mwele Malecela wa NIMRI dhidi ya waziri wake Ummy Mwalimu na waziri akatangaza hadharani kuwa hakushirikishwa kwenye utafiti thidi ya homa us Zika nchini. Hali hiyo ilipelekea kuondolewa kwenye nafasi yake kama mkurugenzi wa taasisi hiyo iliyoko chini ya wizara ya afya.
Juzi kwenye swala la umeme ndugu Sospeter Muhongo naye akatangaza kuikana hadharani EWURA na TANESCO kuwa yeye kama waziri hakushirikishwa kwa namna yoyote ile dhidi ya upandishwaji wa bei ya umeme. Waziri huyo akaenda mbali zaidi akiwatuhumu viongozi watendaji wa TANESCO kwa kufanya makusudi kulihujumu shirika. Hali hiyo ikapelekea ndugu Engineer Mramba Feleschemi kung'olewa kwenye nafasi yake hiyo kama mkurugenzi mtendaji wa shirika hilo lililoko chini ya waziri Sospeter Muhongo.
Nini tatizo? Je ni kweli kuwa hawashirikishwi?
Mawaziri huwa wanapanga bajeti za kila mwaka na ndiyo hasa wanaofuatilia utekelezwaji wa bajeti hizo kwenye taasisi zilizo chini ya wizara zao. Sasa watueleze na wao kuwa bajeti zao wanazopanga ni hewa kwakuwa hawashirikiani na viongozi wa mashirika yaliyo chini ya wizara zao? Huenda bajeti ya Sospeter Muhongo aliyoitoa katikati ya mwaka jana ikawa ni bajeti hewa kwani pengine hasa angekuwa amekaa na menejimenti ya TANESCO basi hata swala la gharama za umeme lingejadiliwa kwa kina. Nasema hivyo kwakuwa bei elekezi ilitolewa baada ya bajeti kusomwa.
Kwenye wizara ya afya pengine ndiyo maana kuna hadi matatizo ya chanjo muhimu, yote haya yakiwa ni matokeo ya bajeti hewa isiyoendana na hali halisi ndani ya wizara hiyo na pengine ni matokeo ya mawaziri kutokushirikiana ipasavyo na viongozi wa taasisi zilizo chini yao.
Mwisho niseme kuwa waziri kutoka hadharani na kumkana msaidizi wake wa chini kwenye taasisi anayoingoza yeye tena baada ya kila kitu kuwekwa hadharani ni udhaifu mkubwa na inaonyesha ama kuna usaliti kwa maslahi ya kisiasa ama uzembe wa hali ya juu! Kumvumilia waziri wa aina hii ni sawa na kuhifadhi "kinyesi" kwenye nguo ya ndani kisha ukatembea nacho! Kitakuwa kinaendelea kutoa harufu kali na mbaya na mwisho ile harufu itazoeleka kwa usugu!