Uchaguzi 2020 Inakuwaje Magufuli anatupangia tumchague nani na nani tusimchague?

kagoshima

JF-Expert Member
Dec 31, 2015
2,631
5,137
Hii ni zamu yetu wananchi kuamua nani tumchague na nani tusimchague kwenda kutuwakilisha.

Maajabu sasa huyu Rais anayemaliza muda wake amesikika akiongea kwa jazba kuwaamrisha wananchi nani wamchague. Hii si sawa maana legitimacy ya uongozi ni baada ya approval ya wenye nchi.

Hivi kumbe siye raia wa nchi si lolote wala chochote.

Je, ni CCM nzima inadharau na kubinya haki ya wananchi kushiriki kuchagua viongozi wawatakao? Au ni hulka tu na udhaifu wa mgombea wao John Pombe Magufuli kutuona siye raia hatuna haki yoyote ya kufanya maamuzi?
 
Kwanza alisema kazi ni ngumu, pili anatufokea wapiga kura, tatu anataka kuongoza Hadi akili zetu na fikra zetu, nne anatupangia tuchague nani, tano hatufai, sita akajiajiri, saba tunataka mtu mwingine atakaefanya kazi nasio kulala na mafile kitandani.
 
Hii ni zamu yetu wananchi kuamua nani tumchague na nani tusimchague kwenda kutuwakilisha .

Maajabu sasa huyu Rais anayemaliza muda wake amesikika akiongea kwa jazba kuwaamrisha wananchi nani wamchague. Hii si sawa maana legitimacy ya uongozi ni baada ya approval ya wenye nchi.
Hii ni mbaya kwa viwango vingi sana. rais anayemaliza muda kama mgombea anaomba kuchaguliwa, hajui kama atashinda au la, wakati huo huo anatishia kuadhibu watu wasipochagua watu wake.

kama hakuna uhuru wa kuchagua, maana yake hakuna uchaguzi hapo.
 
[SUP]Kwanza alisema kazi ni ngumu, pili anatufokea wapiga kura, tatu anataka kuongoza Hadi akili zetu na fikra zetu, nne anatupangia tuchague nani, tano hatufai, sita akajiajiri, saba [/SUP][SUP]tunataka mtu mwingine atakaefanya kazi nasio kulala na mafile kitandani.[/SUP]
Kaharibu sana kwa maneno yale. Naamini kuwa jiwe hawezi siasa na ndiomana alikuwa radhi kutumia trilions of money kuua upinzani ili ajimilikishe nchi. Kadri mida unavyozidi kwenda nia yake ovu inazidi kujipambanua.

Lissu endelea kupiga spana tumjue vizuri huyu.
 
Hawezi siasa, kisha katiba inatoa madaraka makubwa sana kwa rais kiasi kwamba anaweza kuyatumia vibaya atakavyo. Hii ndio maana ninasema, chini ya Magufuli hakuna uchaguzi, bali ni maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura.
 
Magufuli si mwanasiasa, ye ni mwanascience, na ndo maana akiahidi anatekereza, mambo kama hayo ni kawaida kwa raisi anaejiamini na haperekeshwi
 
Magufuli si mwanasiasa, ye ni mwanascience, na ndo maana akiahidi anatekereza, mambo kama hayo ni kawaida kwa raisi anaejiamini na haperekeshwi
Kama sio mwanasiasa anafanya nini kwenye siasa? Si arudi University of Dar akafundishe science
 
Labda ni katika kuandaa mazingira ya wazo la Juma Nkamia (5+5+5+5+n...)
 
Kwanza alisema kazi ni ngumu, pili anatufokea wapiga kura, tatu anataka kuongoza Hadi akili zetu na fikra zetu, nne anatupangia tuchague nani, tano hatufai, sita akajiajiri, saba tunataka mtu mwingine atakaefanya kazi nasio kulala na mafile kitandani.
Pia alisema anatamani kuwa IGP.
 
Bado wanafikiri Tanzania ni ile ya zamani ya kuimba zidumu fikra.
 
uhuru_na_maendeleo.jpg
 
Back
Top Bottom