Inakuwaje Awamu ya Pili ya JK imebadilika sana na kuanza kuogopa maandamano ya wapinzani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Inakuwaje Awamu ya Pili ya JK imebadilika sana na kuanza kuogopa maandamano ya wapinzani?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zak Malang, Sep 2, 2012.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Sep 2, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Wakati wa Mkapa tuliona jinsi utawala huo ulivyokuwa unatumia nguvu ya polisi kuthibiti maandamano ya upinzani, ya NCCR na CUF, watu kuumizwa na wengine hata kufa etc etc. Hata Waisilamu maandamano yao yalikuwa hayavumiliki na mifano ni yale matukio mawili ya Mwembechai mwaka 1998 na 2002.

  Alipoingia JK katika Awamu yake ya kwanza mambo yalibadilika sana, aliruhusu maandamano ya upinzani bila kubughudhiwa. Nakumbuka CUF walifanya maandamano yao makubwa mwaka 2006 hata sisimizi mmoja hakufa. Wote tuliona hivyo ndivyo ilivyokuwa inatakiwa -- ukomavu wa kisiasa katika kuvumiliana.

  nakumbuka ilifikia mahala ambapo hata vyama vilianza vyenyewe kuchoka na hayo maandamano.

  Lakini Awamu ya Pili ya JK mambo yalibadilika ghafla. Uzalendo ulishindikana na maandamano ya upinzani yakaanza kuonekana ni uhalifu mkubwa.

  Serikali inatumia nguvu nyingi, nyenzo katika kuzuia maandamano, ambapo askari wachache tu wangetumika kuyalinda.

  Leo hii naambiwa kuwa magari zaidi ya 10 ya FFU kutoka Iringa, Njombe, Mbeya yalikwenda Nyololo kuzuia maandamano ya CDM. Nauliza: Kwa kitu gani hasa? Kwa tija gani hata kwa upande wa CCM?

  Kisingio cha sensa ni dhaifu mno kwa sababu sensa per se imeisha. Siku walizoongeza si kwamba makarani watapita majumbani tena, isipokuwa wale wasiojiandikisha wao ndiyo waende kutoa taarifa.

  Kwa nini polisi wanashindwa kutumia common sense, na badala yake wanacheza kamari na maisha ya watu? Mtu akifa wanatumia nguvu kubwa kufunika!


  Nawaomba polisi wawaruhusu Chadema kufanya maandamano bila ya hato wao polisi kuyalinda. Naamini hata sisimizi hataguswa. Si ilishatokea Arusha wakati wa kuaga miili ya wale wafuasi wa CDM waliouwawa na polisi? Polisi walisusia hayo maandamano na hakuna hata mtu alipata mchubuko wowote.
   
 2. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #2
  Sep 2, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Siyo nguvu tu, bali pia gharama kubwa kutoka hela za walipa kodi zatumiwa na polisi kudhibiti maandamano na harakati nyingine dhidi ya upinzani, na serikali wala haishituki matumizi hayo mabaya ya fedha.

  Chukuwa mfano wa lile tukio la Mbowe kupelekwa Arusha chini ya ulinzi mkali wa jeshi la polisi kwa gharama kubwa kwani ndege ya JWTZ ilitumika kumpeleka Arusha tena usiku -- kwa kosa tu eti aliruka dhamana ya mahakama!!!

  Na walipofika Arusha yule hakimu aliwaaibisha akina Chagonja na Kova (waliosuka na kusimamia suala hilo) baada ya kumuachia Mbowe ndani ya dakika 10 tu baada ya kufikishwa mahakamani.

  Hivi ilikuwa lazima polisi kufanya vile? Mbowe angetorokea wapi?
   
 3. O

  OgwaluMapesa JF-Expert Member

  #3
  Sep 2, 2012
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 10,948
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  hasa watu wake wanaotaka urais 2015 kama membe,sita,nchimbi ndo wanamdanganya kuhusu kutumia nguvu kumaliza mandamano ya m4c,ili next electn wapate mteremko,.watauwa sana,watapiga watu sana but mabadiliko ni lazima,polisi nao nawashanga mishahara yao midogo kinyama,wanaish maisha ya shida vibaya mno stl wanashabikia serikali hi ya baba riz 1.
   
Loading...