farfat
Senior Member
- Jun 10, 2021
- 158
- 265
Tupo katika kipindi cha toba kwa dini zote, Islamic na Christian tupo katika Ramadan na Kwa Resma, ni matumaini yangu mnashirki vyema na Mungu awabariki.
Kwa hakika mahusiano hayajawahi kuwa rahisi iwe katika uchumba ama ndoa. Kuna ups n down nyingi za kukatisha tamaa, ila wakudumu wanadumu na wakuachana wanaachana.
Lengo hasa la kuleta uzi huu kwenu wanajukwaa wenzangu ni kutaka kujua, huwa mnatumia njia gani kujipooza na maumivu ya kuachana na mwenzi kwa sababu yoyote ile na huchukua muda upi kuanza kutafuta mpenzi mpya wa kuanza nae mahusiano mapya?
Najua fika changamoto ni nyingi na haziishi, hata mpenzi mpya nae huja na changamoto zake (no body is perfect ). Je, kuna haja ya kutafuta mpenzi mpya kwa haraka ili aje ku kuziba nafasi ya mwenzi alietoka?
Vipi kwa ME na KE, uharaka na utayari wa kuanza upya umekaaje?
ANGALIZO: Mpenzi unaemtaka wewe hutengenezwa na wewe mwenyewe na sio jambo rahisi kumtengeneza huyo mtu na ndio maana maumivu huwa makali mtu huyo mkiachana.
Muwe na mfungo mwema.
Alamsik.