Inakuaje unachunguza simu ya mumeo?

Inakuaje unachunguza simu ya mumeo?

Kushika simu ya mke/mume ni kosa kubwa sana ndio chanzo cha ndoa nyingi kuvunjika kila mtu abaki na simu yake kingine simu ya mkononi ni mali ya mtu mmoja sio ya kikundi ili ndoa au mahusiano yenu mnataka yadumu basi kila mtu abaki na simu yake kinyume na hapo mahusiano lazm yavunjike
 
Nadhani umeoa, lakini bado una mentality ya bachelor. Ungeelewa kwamba kukubali kuoa kunamaanisha ku-surrender sehemu kubwa ya hizo unazoziita faragha zako, wala lisingekushughulisha. Je, na yeye akiwa na faragha na ma-X zake halitokuumiza? Kama jibu lako ni ndio, basi unajua unachopaswa kufanya
Acha ubishi. Sio busara kwa mwanamke kukagua simu ya mumewe. Mimi sijaoa ila simu ya mpenzi wangu hata password siijui. Simu yangu ashaniuliza sana password lakini siwezi kumtajia na sio kwamba namcheat ila kuna masuala ya kifamilia, chattings za washkaji zinazohotaji usiri n.k hapaswi kuzijua. Akili yako isiishie kwenye michepuko ya mumeo tu
 
Za asubuhi.

Inakuaje mwanamke unakuwa busy kupekua simu ya mumeo na kuanza kusoma message kuanzia jamiiforum ,fb hadi normal text.

Wakuu niko na mwanamke ninayeishi naye sijamuoa Ila treatment anazonifanyia ninaweza nikafanya awe singo mama.

Nimemkataza kutoshika simu yangu lakini aelewi zaidi ya kugombana kila siku.

Ananuna muda wote.

Hamuwezi mkakaa mkafurahi kama wanavyofanya wanafamilia wengine.

Ana Gubu.
Mi wa kwangu nilishawaambia simu ni mali yangu. Ukiishika ukakuta yasiyokuhusu usiniambie. Chukua maamuzi yako maana mimi sipendi malumbano.

Hawathubutu kuigusa wala kuiangalia maana nlishawaambia kabisa kuna madudu watakutana nayo afu watadedi kwa presha....
 
A
Nadhani umeoa, lakini bado una mentality ya bachelor. Ungeelewa kwamba kukubali kuoa kunamaanisha ku-surrender sehemu kubwa ya hizo unazoziita faragha zako, wala lisingekushughulisha. Je, na yeye akiwa na faragha na ma-X zake halitokuumiza? Kama jibu lako ni ndio, basi unajua unachopaswa kufanya
Angalau wewe unajitambua! Kama bado unahitaji uhuru wako, acha kuoa. Utaishi upendavyo ila ukioa, jua huna siri kwa mkeo na mkeo hana siri kwa mume wake.
 
Sasa mwanamke unaongea naye nini inategemea. Slogan ni ile ile hamna urafiki kati ya mwanaume na mwanamke.

Sasa huyo mwanamke unayeongea naye ni nani na mnaongea kuhusu kazi au mambo ya urafiki tu?

Wewe ukisikia mke wako anaongea na wanaume ambao sio kaka yake au baba yake utachekelea?
Utoto raha, hawa hayajawakuta!
 
Mkuu, data za siri zinatunzwa kwenye simu? Tena peupe tu ambapo mtu yeyote anaweza access? Data za siri si zingetunzwa kwenye hidden/secret folders au apps ambazo zingehitaji passwords na fingerprints na patterns kuzifungua?
Simu zina data - mfano ni number ya mteja, jina lake, mawasilino yake kwa njia ya text, whatsap, email etc- yote hayo yamo kwenye simu na ndio maana ina password. Yeye anenda kutafuta nini humo mpaka kutaka ku- access simu ya mwenza wake bila kibari chake... kujua password ya ATM haimaniishi kwamba ndio utaenda kuzikomba hela zote kwenye cash machine. Simu ni legal device ambayo ina mambo mengi sana- na hivyo an unathorised access yaweza mpeleka mtu jela kimasiala. haya ni mambo ya data protection na hata kama uko kwenye ndoa, usiyachukulie kirahisi namna hiyo... na huyo anayetaka kuchungulia data za mwenza wake- atakutana na nini ambacho hakihusiani na yeye? je ana authority ya kuchungulia au kudukua? haya mambo si ya juu juu ndugu yangu.
 
Hizo gubu na ugomvi siwezi ingilia, ana paswa kubadilika

Ila suala la kushikiana simu fresh tu, ukiona anakuchunguza ujue ana mashaka, akichunguza asipokuta kitu atakuwa mpole tu..

We kwanini hutaki simu yako isishikwe, ina nini?
Una machafu yako play smart,uwe unafuta, kuna raha kuwa na mtu halafu kwa asilimia zaidi ya 90 unamuamini, huoni dalili za usaliti.
 
Nilishamkataza kukagua simu yangu.

Kuna faragha hata kama yeye ni mke wangu aruhusiwi kuzijua .

Nilishampa warning since day one.

Anavuka mipaka .

Halfu anataka ndoa kwa mtindo huu
Hii nayo ni changamoto, huyu atakupa msongo wa mawazo na utaishi kama digidigi if you cannot draw a line. Mipaka lazima iwepo, sio unatoka tu kazini , yeye anakimbilia simu yako....nchi nyingine hii ni domestic abuse, controlling behaviours na manipulation ambazo haziruhusiwi kisheria.
 
Mke wangu nimeishi nae for 5yrs sikuwahi kushika simu yake kabisa,kuna Sikh alikuwa nje simu kaacha ndani nikafunga mlango wa chumba kisha nikachukua simu yake -sijui ni machale yalimcheza vile naanza kuishika tunnikasikia MTU anahangaika kufungua mlango.

Bahati mbaya password nikikuwa siijui sasa nikawa nabuni buni miaka ya watoto kuzaliwa au mwaka wake wa kuzaliwa.Hui muda niliokuwa natumia alitoka nje na jiwe kubwa akavunja mlango-siku hiyo ndio niliona Mke wangu ananguvu.

Mimi bila iana, alipovilunja tu mlango nikaona hapa isije kuwa ugomvi nikamkabidhi simu yake.tokea siku hiyo nilianza kuwasha indicators juu yake,MTU hadi anaamua kuvunja mlango lazima kuna madudu tu.
 
Karoho kabaya tu na peponi utapasikia tu.

Kuna siku nilimpa mtu bana namba yangu. Hakuwa na lengo la kunitongoza ni baba wa mwanafunzi wangu. Nikajua ni mtu mzima anajitambua.

Hee si akanipigia simu saa 4 usiku. Namba ni ngeni nikapokea nikajua ni yeye nikaikatia sikioni. Maana baby angeniuliza hata kama ni mambo ya shule ndio mida hii?

Mara akapiga tena nitafanyaje nikapokea eti linaniuliza “sasa mbona unakata simu tena” . Sasa nikajiuliza kama amegundua nimekata simu kwanini arudie kupiga. Nilitamani nimtukane. Nikamwambia nakusikiliza eti “umeshalala nini au nimepiga muda mbaya”?

Huo ugomvi alioniachia yule ndio nilijifunza tokea hiyo siku.
 
Nipende kukuambia kama ww hujawahi kagua simu yake na yeye ndio kinara wa kukagua yako muweke chini mwambie akiendelea achiliambali hilo fuko la misumari. Simu zinaharibu sana mahusiano tena muda mwingine unakuta hauna makando kando ila zile hisia mbaya zinafanya ndani hakuna amani
 
Nipende kukuambia kama ww hujawahi kagua simu yake na yeye ndio kinara wa kukagua yako muweke chini mwambie akiendelea achiliambali hilo fuko la misumari. Simu zinaharibu sana mahusiano tena muda mwingine unakuta hauna makando kando ila zile hisia mbaya zinafanya ndani hakuna amani
Sipendi mtu aingilie faragha zangu.

Mwanamke kisa unaishi nae anataka akufanye vile anavyotaka yeye.

Mfano usiweke status hata ya kumiwish happy birthday akiwa mwanamke anakasirika tu.
 
Back
Top Bottom