Inakuaje mwanaume unasikiliza taarabu??

Inakuaje mwanaume unasikiliza taarabu??

Hajar nakubaliana ma AmorEy kwa asilimia mia. Siku hizi hakuna taarabu bali uchafu na uchafuzi tu wenyewe wanaita Taradance!

Wasikilize Culture na Nad Ikhwan Swafaa au Malindi ukipenda, kisha rudi nyuma enzi za kina Almarhum Shakila Said, Mwanahela
Asma Hani, Sharmila, Ursulla kwenye mashairi ya kumtoa nyoka pangoni(sio nyoka yule lakini) na sauti za vinanda haswaa

Nenda nchi jirani ya Kenya utafute nyimbo za kina Matano Juma, Juma Bhalo(Mungu Amrehemu), Maulid Juma, Zuhura Swaleh na wengineo uone utajiri wa muziki wa taarabu asilia

Siku hizi hakuna kitu na ndio wanatukanisha Taarabu hao
Kweli kabisa Mkuu,ila swezi kumlaumu mtoa mada kwasababu inaonesha dalili tosha kua sio mtu wa pwani.
 
Taarabu na Hip Hop hazina tofauti kwenye maudhui ya mashairi yao! Tofauti ipo kwenye namna ya kughani.

Mwana Hip Hop anaposema ana mchana mtu flani kwa mistari si taarab hiyo?
 
Kama mada inavyojieleza
Nauliza inakuaje wewe mwanaume kamili rijali unakaa na kuanza kusikiliza nyimbo za taarabu??
Wakati nimesimama pale mataa ya Buzuruga naskia music mnene wa taarabu kutoka gari la jirani,kuchungulia ndani nawaona masela ndo wanaskiliza tena kwa furaha kweli kweli

Music wa taarabu unapendwa na wambea,wanawake na mashoga sasa wewe dume komavu unapata wapi hisia za kusikiliza nyimbo zilizojaa vijembe na gubu?

Mwanaume sikiliza HIP HOP,Bolingo ndomboro ya solo,hizo taarabu waachie wadada na mashoga.
Rijali ni uwezo wa kupiga mashine kikamilifu haihusiani kabisa na usikilizaji wa taarab..usipangie watu cha kusikiliza
 
Kila MTU ana Uhuru wa kuchagua apendacho.. Japo kushangaa inaruhusiwa.. Mimi huwa nashangaa kwa kweli Dume zima lisikilize taarabu..

Lazima kutakuwa na walakini
 
me binafsi hata mwanamke mwenzangu akiwa anapenda taarabu sana namshangaa
 
Back
Top Bottom