Inakuaje mwanaume unasikiliza taarabu??

Inakuaje mwanaume unasikiliza taarabu??

Ni namna unavyoona wewe.
Usitake kila mtu afanane na wewe.

Wapo wapenda hiphop, wengine wapenda bongo fleva, wengine blues, wengine taarabu.
Zote ni choice za watu na wana haki ya kuchagua.
Hatuwezi kufanana wote mkuu, iwe ni dini kila mtu anachagua iwe ni mademu kila mtu anachagua, siasa kila mtu anachagua.
Suala la ujinga na ujanja ni mtu mwenyewe.
Sebene flani hivi amazing ndo hunivutia kusikiliza taarabu na sio mashairi yao! Taarabu ikiwa imepoa haina sebene siwezi kusikiliza aisee! Na Unaposema burudani inahususisha vitu vingi, sio mashairi tu, wengine wanaweza kupenda vinanda, beat za mziki na k. sasa nacho ona walio wengi wamejikita kwenye mashairi ya wimbo, wamesahau kuna midundo, vinanda na k. z
 
jamaa wa mikoani banna sasa si mziki kama mwingine. zamani nilikuwa naenda twanga ya kina banza pale mango. shemeji yenu tukawa tunaenda pale traventine magomeni kuwaona jahazi ya mzee yusufu. na wimbo ninao upenda kwahilo hujanikomoa wa joha khassim. nyie wa mikoani njooni kwenye kumbi za taarabu muone mabinti pini na wenye chura. kustafu kwa mzee yusufu mziki umeyumba. japo machoko hawakosekani ni tabia ya mtu tu
 
Anaanzaje sasa [emoji19]huko ndo sehemu yao.
Hawa wahivi huwa tunawachoma moto haki....
FB_IMG_1536178823330.jpg
 
Kama mada inavyojieleza
Nauliza inakuaje wewe mwanaume kamili rijali unakaa na kuanza kusikiliza nyimbo za taarabu??
Wakati nimesimama pale mataa ya Buzuruga naskia music mnene wa taarabu kutoka gari la jirani,kuchungulia ndani nawaona masela ndo wanaskiliza tena kwa furaha kweli kweli

Music wa taarabu unapendwa na wambea,wanawake na mashoga sasa wewe dume komavu unapata wapi hisia za kusikiliza nyimbo zilizojaa vijembe na gubu?

Mwanaume sikiliza HIP HOP,Bolingo ndomboro ya solo,hizo taarabu waachie wadada na mashoga.

Mawazo ya mfamaji. Machoko hata kwenye slow wapo, hip hop wapo, sebene wapo. kwa iyo wote wanaosikiliza hizo nao ni machoko. Acha kuwa na mawazo ya mtoto wa miaka 9.
 
Ule ni mziki wa pwani ni sawa na mdundiko segere na nyinginezo huwezi kukuta asili ya kwenu na kuicha ndio maana wengi mnaiga mpaka yasiyoigwa kuangalia vitu wanavyofanya majuu huko na kuleta nchini na kudharau vya kwenu
Taarab kuna zile za kusutana na kuna zile zenye maadhi ya mapenzi ni wewe msikilizaji ujichagulie tu
Asant mkuu
 
Mim huwa nasikiliza mziki wowote uliopangiliwa vizuri,saut na tunes,napenda miziki ya Colombia ,taarabu za zaman kina bibi kidude nasikiliza ,hiphop ngumu nasikiliza pia,naona haiona effect yoyote ,mziki ni zaid ya maneno ,mbona vijana wengi wanasikiliza hip hop za kimarekan wakat English hawajui
 
Taarab Asilia ni nzuri sna na inameneno mazuri yaliosanifiwa katika kila ubora,wacheni kujazana sumu waskilize culture musical naad akhwan safaa nakina sinti binti saad utaelewa uzur wa taarab.
Hizi modern ntaarab mbwembwe nyingi kma bongo fleva.
 
Ukipenda kuwa huru na kufuata kitu unachokipenda, basi penda na wengine wawe huru na kufuata vitu wanavyovipenda.

Ilimradi ana maisha yake kajichagulia burudani yake, na wewe una ya kwako umejichagulia.

Kuheshimiana na kuheshimu maisha ya wengine ni kuzuri zaidi, kuliko kuponda hivyo.

Muziki hauna jinsia
 
Kama mada inavyojieleza
Nauliza inakuaje wewe mwanaume kamili rijali unakaa na kuanza kusikiliza nyimbo za taarabu??
Wakati nimesimama pale mataa ya Buzuruga naskia music mnene wa taarabu kutoka gari la jirani,kuchungulia ndani nawaona masela ndo wanaskiliza tena kwa furaha kweli kweli

Music wa taarabu unapendwa na wambea,wanawake na mashoga sasa wewe dume komavu unapata wapi hisia za kusikiliza nyimbo zilizojaa vijembe na gubu?

Mwanaume sikiliza HIP HOP,Bolingo ndomboro ya solo,hizo taarabu waachie wadada na mashoga.
Unajua asili ya taarabu?huu ni muziki wa mwambao,ulitungwa,na kupigwa na jinsia zote huko visiwani,ukanda wa bahari ya Hindi,sasa unataka kutuambia kwamba hao wahenga walikuwa,mashoga,wambea,?acha kukurupuka ndugu,matumizi ya kitu,hayafanyi kitu kiwe kibaya,mbaya hapa ni yule anayekitumia,
Kuna watu hawawezi kusikiliza bolingo,wanataka,hardnock hiphop,ukisikiliza bolingo,wanakushangaa,
Huo ni mtazamo wao,
Mzee yusufu,ameimba taarabu,sio kusikiliza,je ni shoga? Je mashoga wote wanasikiliza taarabu,?vipi kuhusu vijana tunaowaona huku mtaani,wengine tunapiga nao GYM,lakini malinda hawana?au na hao wamearibiwa na Taarabu
 
Jaribu kufanya kitu moyo unapenda,kusikiliza taarabu si dhambi,shida kama utamezwa na miondoko ya taarabu
 
Hii mada imenikumbusha mbal kdogo kipnd ambacho nipo college coz kuna mdau mmoja tulikuwa wote room moja so nyimbo zake za kusikiliza ni taarab had tukawa tunampga big stop kwa hilo aisee
 
mi ni mpenzi wa music almost genre zote..ila taarabu nilast ..least in the least...labda wimbo mmoja tu au mblili za taarabu nazipenda..moja ni hiphop humo humo Nasma Hamis and Gnagwe MObb...apart labda sijui ipi ila taarab kwa ujumla sipendi kabisa....ila njoo hip hohop rap pop rnb soul country classic jazz...fresh..baridaa.....
 
Kuna Mashoga,Wanawake wanaosikiliza hiyo miziki unayoisema ya wanaume..
 
Enzi za vigodoro Taarabu zimetuokoa sana unakuta ikipigwa sebene amsha amsha warembo wote waliojikunyata pembeni wanaingia kati wahuni tunabambia. Hapo tu nilipendaga hz ngoma japo sikuizi siyo member tena wa vigodoro na taarabu sizikumbuki tena ila nikiisikia inapigwa uko naenjoy the memories
 
Mbona hawa wa manyimbo yenu
Alina Ashlay wanaingia kwenye taarab na mnasikiza
Hujaona subalkheri mpenzi waonaje hali yako
Inavyopigwa na kusikizwa kila kona?
Mziki ni wowote unaokugusa
Taarab nyingine zina ujumbe mzito na ukosikiza unapata kausingizi
Tafuta nyimbo selelea
Usikilize ujumbe Wake kama una mpenzi wako lazma umtumie
Nakupa kipande kidogo tu
Nikumbatie wenye wivu wajinyonge
Nikumbatie wanione walalame
Nikumbatie wasojua wanijue
Nikumbatie roho zao ziwaume
Ukiisikiza ina ujumbe mzito wa mappenzi na mziki mtamu
Usipoupenda kajinyonge
 
Back
Top Bottom