Witmak255
JF-Expert Member
- Feb 5, 2019
- 3,264
- 5,450
- Thread starter
- #181
Sio kwamba kwetu Mambo yalikuwa mazuri, Hapana ni familia za kawaida Sana.Hebu jiulize mtu test tube hajawahi kuiona anaisoma tu, yale majaribio yote ameyasoma tu hajawahi yafanya. Mwalimu wake wiki 1 darasani wiki 3 kufatiria mshahara na stress kibao!.
Wale wa arts nao vitabu havipo shuleni, huyo huyo mtoto akirudi nyumbani chakula ugali au uji!, bado atatakiwa akatafute maji, aoshe vyombo!.
We mwenyewe umesema uliomba 450,000 ukapewa 500,000 ina maana kwenu upepo sio mbaya toka zamani, sasa hao wengine hata hela ya uniform 8,500 kwao ni mtihani ukiacha peni ya 200 inayoweza isha mpaka aibe za wenzie kuipata nyingine!.
Shukuru umekulia pazuri, ukasomeshwa pazuri!..
Unaijua Buruma secondary?, Kwa kifupi
Hii shule iko porini, kijijini mno huko musoma vijijini ina walimu4 form one mpaka4, nenda kaangalie matokeo yake