Inakuaje mpaka mtu anafeli O'level?

Inakuaje mpaka mtu anafeli O'level?

Witmak255

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2019
Posts
3,264
Reaction score
5,450
Kiukweli inanishangaza sana ni kwa kivipi Hawa watoto na wadogo zetu wanafeli mitihani yao ya kidato Cha nne, Kwa wale walioenda shule haswa watakubaliana na mimi kidato Cha kwanza mpaka Cha nne kwa mtu alienda shule kusoma ni vigumu Sana kufeli, inakuaje mpaka mtu anakosa hata kupata credit O'level?.

Nakumbuka kipindi nasoma hii level sio kwamba najisifia lakini ilikuwa ni vigumu kunikuta nje ya alama 70+ kwa masomo ya Sanaa na "A" kwa masomo ya physics, maths na chemistry na hii ilikuwa simple tu kwangu kupata one ya 13 na point 4 kwa PCM nilipangwa minaki advance but nikabadili na nikakubaliwa kwenda benjamini mkapa high school kwa PCM.

Nakumbuka siku ya kwanza niliingia kwa mbwembwe Sana maana nilikuwa najiamini Sana kwamba Niko fiti na Comb. niliyochagua ni sahihi na naimudu, kulikuwa na mwalimu anaitwa kiumbe ( nadhani ni Jina la utani) kwa A. maths alikuwa vizuri somehow na kila week kulikuwa na mtihani wa kupimana uwezo kwa F5 na F6 iliyokuwa inatolewa na huyu mwalimu, mwanzo kwa advance kila mtu alikuwa na Moto kweli maana wengi Olevel tulikuwa vizuri tulishibishwa vya kutosha na tuition za mchikichini kwa mood na hidden.

O'level ishu ya physics na maths ilikuwa ni simple Sana kwangu yaani hata ukiniamsha usingizini ukanipa mtihani wa physics nikikosa "A" Basi nitapata "B" inayokaribiana na "A", na hesabu kulikuwa hamna namna ya kupata "B" vyovyote vile lazma nipate "A", the same to chemistry.

Sasa kadri siku zilivyoenda nikiwa advance nikagundua " Physics is not easy again" Kama nilivozoea...Hapa nilikuwa nafundishwa darasani natolewa na mifano naona niko fiti kwelikweli nikikamata KITABU Cha "CHAND" na "FUNDAMENTAL OF ENGINEERING" kusolve maswali najiona mweupe na shida ikaanza pale nilipokuwa naenda mchikichini kufanya mitihani ya kila wiki iliyokuwa inatolewa pale shule ya msingi mchikichini ( mwalimu wa tuition aliyekuwa anatoa hii mitihani Nimemsahau) nakumbuka siku ya kwanza kufanya hii mitihani nilipata 15 ya 100 hapa zilikuwa topic3 tu( projection, Error na Friction).

Nikamfuata mzee nikamueleza kuhusu kunilipia tuition ( mzee hakuwa na shida maana aliujua uwezo wangu), Kama sikosei moody kwa phyisc kwa topic fupi ilikuwa ni15,000/= na Heat na electromagnetic,Modern na zingine ndefu Kama hizi ilikuwa 20,000/ = kwa kila topic na A. Maths kwa Mwalami ilikuwa ni 10,000/= na 15,000/= kwa topic fupi na ndefu, Baada ya kumpigia hesabu mzee kulingana na vipeperushi vilikuwa vimetolewa ilikuwa Kama 450,000/= kwa topic hizi za masomo mawili mpaka zote zinaisha.. mzee akanipa 500,000/=.

Nikaingia tuition nikaaanza topic za mwanzo kabisa, seriously A.maths na chemistry hazikunipa shida kwa asilimia kubwa lakini physics japo niliipa mda wa 70 asilimia kulisoma lakini bado sikuweza kupata "B" NECTA but NECTA nilifaulu kwa division one advance nikiwa na "C" ya physics, nikajiunga chuo udsm kusoma computer engineering. Leo ukiniuliza nirudi kusoma physics Advance ni kitu kitu ambacho siwezi kukubalia " Yaani shule nitarudi ila sio kwa advance physics".

Huwa najiuliza inakuaje mtu anafeli elimu ya kidato Cha nne(4) yaani anapata div.0 au division 4 inawezekana vipi?, Kwa advance haswa kwa masomo ya PCM, CBG, PGM,PCB inawezekana Tena kirahisi Sana kwa walio soma hizi comb. Watanielewa Sana, Ila kwa Hawa O'level inawezekanaje mwanafunzi akakosa Cha kujibu mpaka akapata division 0?.

Kiukweli Mimi huwa simuelewi mtu anaefeli kidato Cha nne, hakuna namna ya mtu aliyesoma vizuri akapata zero au four kidato Cha nne.HAKUNA, mitihani ya level hii inaeleweka na kujibika vizuri mno kwa mtu aliyejiandaa.

Labda Niko wrong nisaidieni kujua inakuaje Hawa watoto na wadogo zetu wanafeli kidato Cha nne?
 
Shangaa tu engineer. Ila wakifaulu wote serikali itawapeleka wapi
 
Wewe bila shaka ndio yule engineer uliyokuwa unajitapa humu mpaka ukamkimbia Humble African

BTW hakuna mahali paliPoandikwa wote wafaulu Olevel.

Kila mmoja na uwezo wake aliobarikiwa.

Mkuu hapana huo sio mimi, halafu mbna Mimi hakuna MAHALI nimejitapa mm nauliza inawezekanaje mtu kufeli O'level?
 
Kwanini hukupata one ya Saba???
Mda huo wewe unapewa pesa ya tuition mwenzako hata hiyo hela hapewi ada yenyewe inatakiwa apambane kufanya vibarua ili alipe ada na matumizi yake binafsi. Kaka maisha yapo tofauti Sana ukifanikiwa shukuru mungu usimcheke asiye fanikiwa tumetofautiana sana
 
Kwanini hukupata one ya Saba???
Mda huo wewe unapewa pesa ya tuition mwenzako hata hiyo hela hapewi ada yenyewe inatakiwa apambane kufanya vibarua ili alipe ada na matumizi yake binafsi. Kaka maisha yapo tofauti Sana ukifanikiwa shukuru mungu usimcheke asiye fanikiwa tumetofautiana sana
Mkuu hii ni kwa advance ndo nimesoma tuition but kwa nature ya masomo ya O'level ukisoma huwezi kushindwa kuondoka na division 3
 
Halafu pamoja na 0 yake maprofesa na maDr wanam-salute hahaha...watu wa hivi ndio wanashusha thamani ya Elimu yetu kabisaaaa
Mkuu hata Tukisambaraika leo tukimbilie Msumbiji, Angola ect unaweza kufuatia vyeti vyako na maisha yakaendelea. Sasa wale wa hisani ya Godfather ndiyo watajua kuwa maharage si mboga.
 
nna division 4 ya form 4,mwana nilifeli now nna degree na nipo kwenye kufanya research kwa ngazi ya master +my own company ambayo naiongoza swali kwako mleta mada hyo 1 yako ya form 4 imekufanyia nn?


Sent from my iPhone using JamiiForums
Mkuu issue ya mafanikio Mimi sijaleta hapa kwa sababu hatufahamiani hivo sitaki kulizungumzia Hilo kiundani.
Mm nimeuliza inakuaje mtu anafeli.. hapa ndo ungetupa uzoefu wako
 
Back
Top Bottom