Inakuaje mpaka mtu anafeli O'level?

Inakuaje mpaka mtu anafeli O'level?

Mkuu hii ni kwa advance ndo nimesoma tuition but kwa nature ya masomo ya O'level ukisoma huwezi kushindwa kuondoka na division 3
Kaka issue Ni mazingira Kuanzia primary mpaka secondary yametofautiana mtu mmoja na mwingine any way Kila mtu anamtazamo wake Kama unaona upo sahihi okay shida haipo
 
Yeah mkuu kumbuka akili watu wanapewa na Mungu kama huamini katika ilo fanya mapinduzi ya kisayansi kupitia bachela yako ya udsm utukumboe watz na technology za abroad.
Kaka nadhani unajua nature ya maswali ya O'level? Inawezekanaje mwanafunzi akashindwa kujibu mpaka akachora picha za mazombi
 
Kama mtu unakuta dume zima halitaki kusikia pysics, chemistry , wala hesabu ya aina yoyote toka form one linajiita mimi ni H e Chi Ji Ero ujue hilo ni vivu ra kutumia ubongo na uwezekano wa kuferi hata hayo ma H e Chi Ji Ero ni mkubwa. Yaani ri mtu harikaki kusikia chochote kinachohusisha hesabu.......>>> KIRAZA>>>
 
Kaka issue Ni mazingira Kuanzia primary mpaka secondary yametofautiana mtu mmoja na mwingine any way Kila mtu anamtazamo wake Kama unaona upo sahihi okay shida haipo
Watz Hali zetu zinajulikana mkuu hata mm nimezaliwa familia maskini na shule zote nimesoma za serikali.

Kwa nature ya mitihani ya O'level, inawezekanaje mwanafunzi akashindwa kujibu mpaka akachora picha za zombi kwenye mitihani?
 
Tena Mimi sikuwa mbinafsi honestly kwa masuala ya kusaidia majibu au kumfundisha mtu ninapojua.
Ndgu mm Sina tatzo na advance kwa michepuo ya sayansi huko lolote linawezekana issue kwa nature ya maswali ya O'level ni ya mtu kupata zero kweli?
kama ulipta o level Na haukuwa Na umimi(ego) unachangamana Na wote(weny uwezo Na wsio) hilo swali lako lilijibiwa kitambo
 
Kiukweli inanishangaza sana ni kwa kivipi Hawa watoto na wadogo zetu wanafeli mitihani yao ya kidato Cha nne, Kwa wale walioenda shule haswa watakubaliana na mimi kidato Cha kwanza mpaka Cha nne kwa mtu alienda shule kusoma ni vigumu Sana kufeli, inakuaje mpaka mtu anakosa hata kupata credit O'level?.

Nakumbuka kipindi nasoma hii level sio kwamba najisifia lakini ilikuwa ni vigumu kunikuta nje ya alama 70+ kwa masomo ya Sanaa na "A" kwa masomo ya physics, maths na chemistry na hii ilikuwa simple tu kwangu kupata one ya 13 na point 4 kwa PCM nilipangwa minaki advance but nikabadili na nikakubaliwa kwenda benjamini mkapa high school kwa PCM.

Nakumbuka siku ya kwanza niliingia kwa mbwembwe Sana maana nilikuwa najiamini Sana kwamba Niko fiti na Comb. niliyochagua ni sahihi na naimudu, kulikuwa na mwalimu anaitwa kiumbe ( nadhani ni Jina la utani) kwa A. maths alikuwa vizuri somehow na kila week kulikuwa na mtihani wa kupimana uwezo kwa F5 na F6 iliyokuwa inatolewa na huyu mwalimu, mwanzo kwa advance kila mtu alikuwa na Moto kweli maana wengi Olevel tulikuwa vizuri tulishibishwa vya kutosha na tuition za mchikichini kwa mood na hidden.

O'level ishu ya physics na maths ilikuwa ni simple Sana kwangu yaani hata ukiniamsha usingizini ukanipa mtihani wa physics nikikosa "A" Basi nitapata "B" inayokaribiana na "A", na hesabu kulikuwa hamna namna ya kupata "B" vyovyote vile lazma nipate "A", the same to chemistry.

Sasa kadri siku zilivyoenda nikiwa advance nikagundua " Physics is not easy again" Kama nilivozoea...Hapa nilikuwa nafundishwa darasani natolewa na mifano naona niko fiti kwelikweli nikikamata KITABU Cha "CHAND" na "FUNDAMENTAL OF ENGINEERING" kusolve maswali najiona mweupe na shida ikaanza pale nilipokuwa naenda mchikichini kufanya mitihani ya kila wiki iliyokuwa inatolewa pale shule ya msingi mchikichini ( mwalimu wa tuition aliyekuwa anatoa hii mitihani Nimemsahau) nakumbuka siku ya kwanza kufanya hii mitihani nilipata 15 ya 100 hapa zilikuwa topic3 tu( projection, Error na Friction).

Nikamfuata mzee nikamueleza kuhusu kunilipia tuition ( mzee hakuwa na shida maana aliujua uwezo wangu), Kama sikosei moody kwa phyisc kwa topic fupi ilikuwa ni15,000/= na Heat na electromagnetic,Modern na zingine ndefu Kama hizi ilikuwa 20,000/ = kwa kila topic na A. Maths kwa Mwalami ilikuwa ni 10,000/= na 15,000/= kwa topic fupi na ndefu, Baada ya kumpigia hesabu mzee kulingana na vipeperushi vilikuwa vimetolewa ilikuwa Kama 450,000/= kwa topic hizi za masomo mawili mpaka zote zinaisha.. mzee akanipa 500,000/=.

Nikaingia tuition nikaaanza topic za mwanzo kabisa, seriously A.maths na chemistry hazikunipa shida kwa asilimia kubwa lakini physics japo niliipa mda wa 70 asilimia kulisoma lakini bado sikuweza kupata "B" NECTA but NECTA nilifaulu kwa division one advance nikiwa na "C" ya physics, nikajiunga chuo udsm kusoma computer engineering. Leo ukiniuliza nirudi kusoma physics Advance ni kitu kitu ambacho siwezi kukubalia " Yaani shule nitarudi ila sio kwa advance physics".

Huwa najiuliza inakuaje mtu anafeli elimu ya kidato Cha nne(4) yaani anapata div.0 au division 4 inawezekana vipi?, Kwa advance haswa kwa masomo ya PCM, CBG, PGM,PCB inawezekana Tena kirahisi Sana kwa walio soma hizi comb. Watanielewa Sana, Ila kwa Hawa O'level inawezekanaje mwanafunzi akakosa Cha kujibu mpaka akapata division 0?.

Kiukweli Mimi huwa simuelewi mtu anaefeli kidato Cha nne, hakuna namna ya mtu aliyesoma vizuri akapata zero au four kidato Cha nne.HAKUNA, mitihani ya level hii inaeleweka na kujibika vizuri mno kwa mtu aliyejiandaa.

Labda Niko wrong nisaidieni kujua inakuaje Hawa watoto na wadogo zetu wanafeli kidato Cha nne?
Ulivyoiona physics ya A level kuwa huwezi kupata A,na wenzako wanaiona ya O level hawawezi kupata hata C,unakuta walikua wazuri sana shule ya msingi,waliweka 150/150 yaan masomo yote matatu walipiga 50,50,50

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mazingira tunayosomea tunatofautiana

Mfano nimelelewa na mama wa kambo kutoka shule unafikia shughuli kemkem nyumbani chakula siku nyingine hupewi.......unakiona kitanda saa sita usiku hata kujisomea haiwezekani saa kumi na moja alfajiri uwe macho ....unaacha umefanya kazi zote za ndani ili mama akiamka ni yeye na vikao vya masengenyo mtaani,
usipoosha ukirudi toka shule anakutundika kwenye dari kichwa chini miguu juu unalamba stick.......


Na hapo utazuiwa wiki nzima hakuna kwenda shule unatumikia adhabu ya kumfanyia kazi zote

Kama ni shamba akipewa hela ya vibarua anaila then mi ndo napewa adhabu ya kulima

Ukifaulu piga goti shukuru kuna wengine akili zimo lakini mazingira ni magumu mno kufaulu

Ila sikufeli nimekuonyesha kuwa kama inawezekana ni rahisi kufaulu basi hata kufeli ni rahisi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kiukweli inanishangaza sana ni kwa kivipi Hawa watoto na wadogo zetu wanafeli mitihani yao ya kidato Cha nne, Kwa wale walioenda shule haswa watakubaliana na mimi kidato Cha kwanza mpaka Cha nne kwa mtu alienda shule kusoma ni vigumu Sana kufeli, inakuaje mpaka mtu anakosa hata kupata credit O'level?.

Nakumbuka kipindi nasoma hii level sio kwamba najisifia lakini ilikuwa ni vigumu kunikuta nje ya alama 70+ kwa masomo ya Sanaa na "A" kwa masomo ya physics, maths na chemistry na hii ilikuwa simple tu kwangu kupata one ya 13 na point 4 kwa PCM nilipangwa minaki advance but nikabadili na nikakubaliwa kwenda benjamini mkapa high school kwa PCM.

Nakumbuka siku ya kwanza niliingia kwa mbwembwe Sana maana nilikuwa najiamini Sana kwamba Niko fiti na Comb. niliyochagua ni sahihi na naimudu, kulikuwa na mwalimu anaitwa kiumbe ( nadhani ni Jina la utani) kwa A. maths alikuwa vizuri somehow na kila week kulikuwa na mtihani wa kupimana uwezo kwa F5 na F6 iliyokuwa inatolewa na huyu mwalimu, mwanzo kwa advance kila mtu alikuwa na Moto kweli maana wengi Olevel tulikuwa vizuri tulishibishwa vya kutosha na tuition za mchikichini kwa mood na hidden.

O'level ishu ya physics na maths ilikuwa ni simple Sana kwangu yaani hata ukiniamsha usingizini ukanipa mtihani wa physics nikikosa "A" Basi nitapata "B" inayokaribiana na "A", na hesabu kulikuwa hamna namna ya kupata "B" vyovyote vile lazma nipate "A", the same to chemistry.

Sasa kadri siku zilivyoenda nikiwa advance nikagundua " Physics is not easy again" Kama nilivozoea...Hapa nilikuwa nafundishwa darasani natolewa na mifano naona niko fiti kwelikweli nikikamata KITABU Cha "CHAND" na "FUNDAMENTAL OF ENGINEERING" kusolve maswali najiona mweupe na shida ikaanza pale nilipokuwa naenda mchikichini kufanya mitihani ya kila wiki iliyokuwa inatolewa pale shule ya msingi mchikichini ( mwalimu wa tuition aliyekuwa anatoa hii mitihani Nimemsahau) nakumbuka siku ya kwanza kufanya hii mitihani nilipata 15 ya 100 hapa zilikuwa topic3 tu( projection, Error na Friction).

Nikamfuata mzee nikamueleza kuhusu kunilipia tuition ( mzee hakuwa na shida maana aliujua uwezo wangu), Kama sikosei moody kwa phyisc kwa topic fupi ilikuwa ni15,000/= na Heat na electromagnetic,Modern na zingine ndefu Kama hizi ilikuwa 20,000/ = kwa kila topic na A. Maths kwa Mwalami ilikuwa ni 10,000/= na 15,000/= kwa topic fupi na ndefu, Baada ya kumpigia hesabu mzee kulingana na vipeperushi vilikuwa vimetolewa ilikuwa Kama 450,000/= kwa topic hizi za masomo mawili mpaka zote zinaisha.. mzee akanipa 500,000/=.

Nikaingia tuition nikaaanza topic za mwanzo kabisa, seriously A.maths na chemistry hazikunipa shida kwa asilimia kubwa lakini physics japo niliipa mda wa 70 asilimia kulisoma lakini bado sikuweza kupata "B" NECTA but NECTA nilifaulu kwa division one advance nikiwa na "C" ya physics, nikajiunga chuo udsm kusoma computer engineering. Leo ukiniuliza nirudi kusoma physics Advance ni kitu kitu ambacho siwezi kukubalia " Yaani shule nitarudi ila sio kwa advance physics".

Huwa najiuliza inakuaje mtu anafeli elimu ya kidato Cha nne(4) yaani anapata div.0 au division 4 inawezekana vipi?, Kwa advance haswa kwa masomo ya PCM, CBG, PGM,PCB inawezekana Tena kirahisi Sana kwa walio soma hizi comb. Watanielewa Sana, Ila kwa Hawa O'level inawezekanaje mwanafunzi akakosa Cha kujibu mpaka akapata division 0?.

Kiukweli Mimi huwa simuelewi mtu anaefeli kidato Cha nne, hakuna namna ya mtu aliyesoma vizuri akapata zero au four kidato Cha nne.HAKUNA, mitihani ya level hii inaeleweka na kujibika vizuri mno kwa mtu aliyejiandaa.

Labda Niko wrong nisaidieni kujua inakuaje Hawa watoto na wadogo zetu wanafeli kidato Cha nne?
Uzi wako umebeba mengi ila pamoja na nia ya kutaka kujua inawezekanaje kufeli o'level pia kuna kaunafiki na majigambo by the way Mimi nilifeli form two na form four nikascore div 4 wakati tunaendelea kutafuta majibu ni vizuri tukawa tunatafakari inawezekanaje degree holder akakosa ajira na pia akashindwa kutumia elimu yake kusurvive maisha mtaani.?
 
Ulivyoiona physics ya A level kuwa huwezi kupata A,na wenzako wanaiona ya O level hawawezi kupata hata C,unakuta walikua wazuri sana shule ya msingi,waliweka 150/150 yaan masomo yote matatu walipiga 50,50,50

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu kwa advance ni issue Kama umepita hasa kwa masomo ya sayansi utakubaliana na mm.

O'level masomo yake ni meupe Sana hata maswali yake yako wazi pia inawezekanaje kupata zero huku? Hilo ndo swali langu
 
Kama mtu unakuta dume zima halitaki kusikia pysics, chemistry , wala hesabu ya aina yoyote toka form one linajiita mimi ni H e Chi Ji Ero ujue hilo ni vivu ra kutumia ubongo na uwezekano wa kuferi hata hayo ma H e Chi Ji Ero ni mkubwa. Yaani ri mtu harikaki kusikia chochote kinachohusisha hesabu.......>>> KIRAZA>>>
Kwa uandishi huu ndo unasimanga wenzako kweli!!!! Kuna watu hata pai hawaijui wanafanya biashara zao vizuri na wamefanikiwa kimaisha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uzi wako umebeba mengi ila pamoja na nia ya kutaka kujua inawezekanaje kufeli o'level pia kuna kaunafiki na majigambo by the way Mimi nilifeli form two na form four nikascore div 4 wakati tunaendelea kutafuta majibu ni vizuri tukawa tunatafakari inawezekanaje degree holder akakosa ajira na pia akashindwa kutumia elimu yake kusurvive maisha mtaani.?
Haikuwa na nia hiyo mkuu, lakini mawzo yako nayaheahimu Kaka.. Hiyo issue ya bachelor holder kutumia elimu zao kujiajiri kwa Leo Sina jibu mkuu.
 
Watz Hali zetu zinajulikana mkuu hata mm nimezaliwa familia maskini na shule zote nimesoma za serikali.

Kwa nature ya mitihani ya O'level, inawezekanaje mwanafunzi akashindwa kujibu mpaka akachora picha za zombi kwenye mitihani?
Kama kweli ulisoma shule za serikali hukutakiwa kuja kuuliza humu sababu za kutofanya vizur kwa ngazi ya kidato cha NNE. Sample unayo wewe mwenyewe kwa sababu najua hamkufaulu wote ,,,sasa tuambie kwanini mlifaulu wachache ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu kwa advance ni issue Kama umepita hasa kwa masomo ya sayansi utakubaliana na mm.

O'level masomo yake ni meupe Sana hata maswali yake yako wazi pia inawezekanaje kupata zero huku? Hilo ndo swali langu

ingekuwa jf wanaruhusu matusi nngekutukanaa
 
Kwa uandishi huu ndo unasimanga wenzako kweli!!!! Kuna watu hata pai hawaijui wanafanya biashara zao vizuri na wamefanikiwa kimaisha

Sent using Jamii Forums mobile app
Issue sio biashala ni ukiraza!!! wewe kweri hata 4figure hujui kuitumia? haya basi hata log? basi yawezekana huku kwenye Dx , dy na calliculus kwa ujumla ukasema kichwa kinawaka moto basi hata faraday na bernoulli zinakushinda si utakuwa unaibiwa tu na wafanyakazi wako?
 
Hapo unasema inawezekanaje kufeli wakati watu wanafeli kila mwaka, halafu kufeli mitihani sio kufeli maishani.

Angalia waliopasua na kuwa matajiri wakubwa leo walifeli O levels kama kina Alan sugar, Rchard Branson pia alishindwa na kukimbia akiwa na miaka 16
Hata Simon Cowell pia
Aisee lakini leo ndio famous people
Na wewe nikukute silicon valley sawa
Sio wote wana uwezo wa kukariri shuleni

Wengine wamebadilishwa kazi jana na leo angalia wanavyounguruma utafikiri wameambia wakasimamie dunia nzima


Sent from my SM-G570F using Tapatalk
 
Back
Top Bottom