Ndoa ni makubaliano ya watu wawili walioridhiana kuishi kwa pamoja, na ukiishi na mwanamke/mwanamume ndani yamiezi sita mfululizo ni mkeo/mumeo hata kama hamjafunga ndoa (awali ilikuwa miaka miwili) na kama mtafunga ndoa iwe kimila, kiserikali au kidini basi ndiyo kabisa umepigilia msumari. Huyo Mary Kileo alishaolewa mwaka 1999 na muwewe akafariki mwaka 2002 na akafunga ndoa mpya na mume huyu mwaka 2008 kwa mkuu wa Wilaya Kahama. Kwangu hii ni ndoa.
Wachagga hapa wanalilia mali tu za huyu dada yao kwani alikuwa ni afisa Ugavi(mambo yao si unayajua tena na chenji). Na kwa kuthibitisha hilo ndugu wa marehemu Mary tayari walishakamata gari japo vielelevyo vya gari anavyo mume wa marehemu.
Hili ni kosa kubwa sana kwa ndugu kutaka kuingilia mali za ndugu marehemu ambaye tayari alishaolewa. Sasa huyo kaka aliko kuzimu sasa amefaidi nini? Kumbuka ukishapokea mahari zinaambatana na mila na kwa wakati mwingine mila huwa ni balaa kuzichezea, makabila mengine mila hizi ni kama mizimu ya kutambikia, sasa wewe unachezea mizimu kisa kijigari, pesa, pengine na mali nyinginezo. Yaani unazembea kujituma kupata mali unasubiri za ndugu akifariki? Sasa basi naamini kuwa kaka yao marehemu alikuwa na mke, basi na waende tena mahakamani wakadai kuwa si mke halali ili wafaidi mali za ndugu zao wawili. Kumbuka kuwa ukifa unaacha mali zote ikiwemo pesa, sijui ni nani alishaomba azikwe na nyumba, pesa, vito vya thamani hata mke/mume na watoto hata kama uliwapenda sana. Ifike mahali tuthamini utu zaidi kuliko mali.
Kitendo cha jana ni fundisho kwa makabila yote ambayo yanagombania mali za ndugu. Ni fundisho pia kwetu ambao hatuandiki wosia wa mali zetu na utaratibu mzima wa maziko pindi utakapokufa hasa kama umeoa/olewa na kabila tofauti. Haya yakiwekwa wazi huwa yanapunguza kwa kiasi kikubwa mitafaruku mingi.
Wachagga jana mmetia aibu kubwa mno, mnaonekana ni waroho wa mali na adhabu ikapatikana instantly!!! Sasa leo msiba umehamia wapi? Hata marehemu mwenyewe anahuzunika mnapigania kiwiliwili chake. Je mnafahamu ni kiasi gani ambacho alikuwa anampenda mumewe na leo mnamnyanyasa? Hivi hawa ni wachagga wa eneo lipi? Mwenye kuwafahamu rusha hapa. Shame on You.
hivi watu kwa nini wasitafute kwa jasho mpaka wasubiri marehemu afe ndo waanze kutoa macho kwenye mali zake
Inakera sana
mila na desturi hizo!
mimi nimeona jamaa anaitolea mahari maiti!...ni vitu vidogo sana lakini vina maana kubwa
Maane nakuunga mkono,haya mambo hatuna budi kuyaacha,mali tunazigombania lakini mwisho wa siku tunaziacha hapa hapa. Mimi ni mfano mzuri sana,nimezaliwa katika familia zenye matatizo hayo.
Kuna watu walinidhulumu kila kitu kutoka kwa wazazi wangu, lakini leo hii hao ndugu nawasomeshea watoto wao.Wanaona aibu sana na Mungu amewapa uhai waone maisha yangu kuwa hayakuwa yanategemea mali walizoacha wazazi wangu.
Huyu jamaa aliyekufa ni fundisho kwa watu wote wanaopenda kugombea mali. Huyu mke wa huyu marehemu mpya namuonea huruma sana,maana hii familia kimeo.
Jamani ubinadamu uko wapi tena, kwann watu tunathimini pesa kuliko utu? inabidi tuwe na aibu kidogo tumwogope Mungu ndugu zangu. sasa hawa ndugu watamzika yupi kwanza? Real shame on you!Ndoa ni makubaliano ya watu wawili walioridhiana kuishi kwa pamoja, na ukiishi na mwanamke/mwanamume ndani yamiezi sita mfululizo ni mkeo/mumeo hata kama hamjafunga ndoa (awali ilikuwa miaka miwili) na kama mtafunga ndoa iwe kimila, kiserikali au kidini basi ndiyo kabisa umepigilia msumari. Huyo Mary Kileo alishaolewa mwaka 1999 na muwewe akafariki mwaka 2002 na akafunga ndoa mpya na mume huyu mwaka 2008 kwa mkuu wa Wilaya Kahama. Kwangu hii ni ndoa.
Wachagga hapa wanalilia mali tu za huyu dada yao kwani alikuwa ni afisa Ugavi(mambo yao si unayajua tena na chenji). Na kwa kuthibitisha hilo ndugu wa marehemu Mary tayari walishakamata gari japo vielelevyo vya gari anavyo mume wa marehemu.
Hili ni kosa kubwa sana kwa ndugu kutaka kuingilia mali za ndugu marehemu ambaye tayari alishaolewa. Sasa huyo kaka aliko kuzimu sasa amefaidi nini? Kumbuka ukishapokea mahari zinaambatana na mila na kwa wakati mwingine mila huwa ni balaa kuzichezea, makabila mengine mila hizi ni kama mizimu ya kutambikia, sasa wewe unachezea mizimu kisa kijigari, pesa, pengine na mali nyinginezo. Yaani unazembea kujituma kupata mali unasubiri za ndugu akifariki? Sasa basi naamini kuwa kaka yao marehemu alikuwa na mke, basi na waende tena mahakamani wakadai kuwa si mke halali ili wafaidi mali za ndugu zao wawili. Kumbuka kuwa ukifa unaacha mali zote ikiwemo pesa, sijui ni nani alishaomba azikwe na nyumba, pesa, vito vya thamani hata mke/mume na watoto hata kama uliwapenda sana. Ifike mahali tuthamini utu zaidi kuliko mali.
Kitendo cha jana ni fundisho kwa makabila yote ambayo yanagombania mali za ndugu. Ni fundisho pia kwetu ambao hatuandiki wosia wa mali zetu na utaratibu mzima wa maziko pindi utakapokufa hasa kama umeoa/olewa na kabila tofauti. Haya yakiwekwa wazi huwa yanapunguza kwa kiasi kikubwa mitafaruku mingi.
Wachagga jana mmetia aibu kubwa mno, mnaonekana ni waroho wa mali na adhabu ikapatikana instantly!!! Sasa leo msiba umehamia wapi? Hata marehemu mwenyewe anahuzunika mnapigania kiwiliwili chake. Je mnafahamu ni kiasi gani ambacho alikuwa anampenda mumewe na leo mnamnyanyasa? Hivi hawa ni wachagga wa eneo lipi? Mwenye kuwafahamu rusha hapa. Shame on You.
Yaani jamaa amekufa mahakamani kwa fraha kushinda kesi ya maiti kwa nini haswa watu wanagombea mtu aliye kufa? Wanataka kutambika?
Kuna mchangiaji mmoja wa TBC Taifa amesema kuwa ndugu hawapendi kumuuguza mgonjwa kwa sababu ni mzigo na hasara ila wanagombania maiti kwa sababu ni dili. Nadhani kuna ukweli fulani katika hili....???😕
Hehehehe dah alafu ndugu wangekuwa wanagombania mgonjwa kuuguza mbona wagonjwa wangekuwa wanapona kwa faraja. Lakini utashangaa wkt anaumwa hao jamaa walikuwa mbaali kafa basi wote hao wanagombania ndo maana mm naamini wanagombania kwa ajili ya mambo ya kishirikina zaidi.