Uchaguzi 2020 Inahitaji juhudi ili kurusu uchaguzi kuendelea

ZALEMDA

JF-Expert Member
Aug 15, 2017
1,647
1,884
Tangia tumeanza process ya kuingia kwenye uchaguzi wa mwaka 2020, kumekuwepo maneno mengi yanayoashiria uvunjifu wa Amani, vitisho kutoka nje ya nchi hasa pale mgombea fulani anapomshutumu mwenzake kuwa serikali yako ndiyo ilinipiga risasi, serikali yako imeteka na kuua Watu nk.

Tumeona barua nyingi kutoka Kwenye kampuni ya uwakili inayosimamiwa na mr Robert Amsterdam ikimtisha Rais wa sasa wa Tanzania ambaye ni mgombea urais kwa tiketi ya chama Tawala.

Sababu za kuomba uchaguzi uahirishwe ni hizi zifutazo

1.Kutoa maneno mabaya juu ya rais JPM ni kuhatarisha usalama wa Rais Magufuli wakati kampeni zikianza kwa sababu Watu watakuwa na hasira wakiamini kuwa mgombea wao ni mremavu kwa sababu ya awamu ya Tano.

2. Kutoa maneno mabaya juu ya awamu ya tano ni kuhatarisha usalama wa mgombea anayeishutumu serikali ya awamu ya tano kwamba inahusika na yaliyomtokea mgombea wa upinzani kwa kupigwa risasi

3. Nchi za magharibi na CHADEMA ni kama wameshamuandaa mr Robert Amsterdam kutumika kuvuruga amani ya nchi pale anapotoa vitishisho juu ya Mh Rais J P Magufuli.

4. Kwa maneno yanayotoka kinywani mwake ni kama mgombea urais wa upinzani hayuko tayari kupokea Matokeo ikiwa atakuwa ameshindwa: Nitaamrisha maandamano.

Ili kuruhusu uchaguzi kuendelea inaitajika juhudi kubwa kuhakikisha yafutayo yanafanyika:

1. Kuondoa maneno ya kushutumiana kuwa wewe uliagiza nipigwe risasi, umeteka na kuua watu. Wagombea wajikitetea katika kunadi sera za vyama vyao na si vingevyo.

2. Huyu anayejiita mtetezi wa mgombea urais kwa tiketi ya CHADEMA mr Robert Amsterdam aache mara Moja kumtisha Rais Magufuli na nchi yetu, vinginevyo tutajua kuwa mteja wake ametumwa kuvuruga amani ya taifa letu, kama walivyofanya Libya, Iraq, Liberia, Siria nk.

3. Usalama wa taifa wahakikishe wagombea wote na hasa mh Magufuli na Tundu Lissu wanalindwa vilivyo kwa sababu anything that may happen involving one the above will result into a war as it happened in Rwanda, Burundi, Libya, Iraq, Sudan, Somalia, Syria etc

4. NEC isisite kumchukulia Hatua kali mgombea atayehubiri chuki. Hapa tusimuogope Mr Amsterdam Bali tuilinde nchi yetu kwa nguvu zote.

5. Usalama wa taifa wanatakiwa kuhakikisha kuwa nchi yetu iko salama wakati wowote kabla na baada ya uchaguzi .Mipaka iko salama ,majirani wasitumike kuwa base ya Adui wa taifa letu.

6. Viongozi wa dini kuendelea kuliombea taifa letu wakati huu mgumu wa uchaguzi.Ikiwezekana Kusitokee Dini Yoyote itakayohubiri Siasa au kuegemea upande wowote.

Nawatakieni Jumapili njema na uchaguzi mwema.
 
Our intelligence services TISS iliwahi kupambana na BOSS ya makaburu time za vita vya ukombozi na tukawashinda.

Dunia nzima inajua lazima JPM ashinde huyo Amsterdam ni nothing kwa nchi yenye historia kubwa kama Tz

Ni vigumu saana kwa watanzamia kuingia kwenye civil war sababu tunapendana by nature
 
Mbona umeandika kwa hila? Umepindisha ama kubadili maneno. Je umenikumbusha maneno ambayo shetani alitumia kumjaribu Bwana Yesu, shetani yaani ibilisi aliondoa au kuruka mistari ya maandiko.

1. Mgombea amesema anataka uchaguzi huru nawa haki, na amesema atakubali kushindwa iwapo Tume itaendesha uchaguzi huru nawa haki. Shetani ameondoa maneno haki, huru n.k

2. Maneno ya risasi hayo yanahitaji tu common sense kujua who orchestrated that attempted murder. However, lakini common sense is not that common, hivyo umesamehewa.

3. Kampuni ya nje ya uwakili inasisitiza haki haki. Amani bila haki, hiyo siyo amani.

4. Siasa ni ushindani wa hoja. Jibuni hoja zake.
 
Kwanini usiseme ili kuepuka vita KUWE NA TUME HURU YA UCHAGUZI NA POLISI WAACHE KUTUMIKA???

Kwanini usiseme ili kuepuka vita wanaochochea kupigana mitama kama NAPE WAKAMATWE??

Mjinga mkubwa wewe. Umekomaa na Amsterdam unaacha kukomaa na vitu vinavyosababisha uvunjifu wa amani
 
WATU WAMEGAWANYIKA SANA

Kuna mtu ambaye yeye binafsi ni tatizo, huyu ni hatari sana maana yeye ndiye tatizo lenyewe. Umuonapo mtu huyo, ujue unaona tatizo, na ukiwa karibu naye maana yake uko karibu na tatizo, na ukijipendekeza kwake ujue unajipendekeza kwa tatizo, na kujipendekeza kwa tatizo maana yake hauko sawa.

Kuna mtu mwingine yeye ana matatizo huyu anahitaji msaada, hasa kama anajua ana matatizo na anahitaji msaada. Mbaya ni pale watu wanapojua kwamba yeye ana matatizo na anahitaji msaada, lakini yeye hajui kwamba ana matatizo na anahitaji msaada.

Kuna mtu ambaye yeye si tatizo wala hana tatizo, bali yeye ni msababisha matatizo. Huyu anaweza kutafutiwa dawa ya kumpunguza spidi, kwa kumpa ushauri au kuadhibiwa, maana yeye kila nafasi apatayo husababisha tatizo.

Mtu wa mwisho ni mtatua matatizo, hawa ni wale wenye hekima na akili.

HIVI NDIVYO TULIVYOGAWANYIKA JUMAPILI NJEMA
 
Tatizo kubwa ni Jpm kutosimama kama rais wa watanzania wote kipindi chote cha miaka mitano.Yeye muda wote anaact kama rais wa wanaccm.Tangu lissu ameingia nchini ameshindwa hata kumjulia hali na kumpa pole kama mmoja wa RAIA wake.pia ameshindwa kuagiza vyombo vinavyohusika kuchunguzwa tukio La kushambuliwa mbunge Dodoma mchana kweupe.Binafsi kadiri Siku zinavyosonga sielewi uzalendo wa Jpm umesimama wapi.kazi kuu ya rais wa nchi ni kuliunganisha taifa, lakini jpm kashindwa vibaya sana.Taifa ni zaidi ya chama.Chama in kundi tu LA watu ambalo laweza sambaratika muda wowote.Tanzania itadumu daima.
 
Yaani kabisa useme mtu atakaa aamini matokeo ya NEC, wakati wao wenyewe wana idadi ya wapiga kura ya kubumba? Tanzania ina wananchi wanaokaribia 60m, inawezekana vipi nusu yake ndio wawe wamejiandikisha kupiga kura? Kwa mujibu wa NEC wapiga kura ni 29m+, yaani kila watanzania wawili mmoja kajiandisha kupiga kura, na inawezekana vipi watu wenye miaka 18+ wawe idadi sawa na walio chini ya miaka 18? Kama kweli nusu ya watanzania wote wamejiandikisha kupiga kura, ina maana kila mtu mwenye miaka 18+ ana kitambulisho cha kupigia kura, jambo ambalo sio kweli kabisa. Sasa mnapoleta mabandiko marefu huku tunaona wazi kuwa tume ina idadi ya uongo, matokeo yatakuwaje ya kweli? Chanzo cha machafuko nchi hii itakuwa ccm na NEC.
 
Hahahaaa! Relax mkuu, hakutakuwa na vita wala kinachofanana na vita, uchaguzi utaisha vizuri na maisha yataendelea kama kawaida. Tatizo huyo Lissu mnamkuza kuliko uhalisia. Lissu ni wa kawaida sana hawezi kusababisha taharuki yoyote kwa nchi. Lissu hamfikii Lowassa hata robo kwa umaarufu -- kama unaelewa ninachozungumza.
 
our intelligence services TISS iliwai kupambana na BOSS ya makaburu time za vita vya ukombozi na tukawashinda

Dunia nzima inajua lazima JPM ashinde huyo Amsterdam ni nothing kwa nchi yenye historia kubwa kama Tz

Ni vigumu saana kwa watanzamia kuingia kwenye civil war sababu tunapendana by nature


JPM lazima ashinde au lazima tume ya uchaguzi imtangaze mshindi?
 
Hahahaaa! Relax mkuu, hakutakuwa na vita wala kinachofanana na vita, uchaguzi utaisha vizuri na maisha yataendelea kama kawaida. Tatizo huyo Lisu mnamkuza kuliko uhalisia. Lisu ni wakawaida sana hawezi kusababisha taharuki yoyote kwa nchi. Lisu hamfikii Lowassa hata robo kwa umaarufu -- kama unaelewa ninachozungumza.

Lowassa hakuwa mpinzani, bali alikuwa mgombea wa CCM kupitia upinzani.
 
Unyanyasaji, utekaji, mauaji, lazima viwe ni ajenda kwenye uchaguzi huu maana vinahusu haki ya mtu kuishi. Sasa unataka wagombea wasiongelee kuhusu wasiojulikana then waongelee kuhusu nini?

Serikali iliacha kuchunguza kupotea kwa Azory Gwanda, Ben Saanane, kupigwa risasi Lissu, maiti za kwenye viroba, Masheikh huko mikoa ya kusini kutekwa na baadhi kurudi wamejeruhiwa vibaya hata kutiwa upofu halafu unataka isiwe ajenda ya uchaguzi?

Pole sana ndugu, Hii ni ajenda muhimu sana ya kuing'oa CCM madarakani
 
Relax mkuu naamini huyu mjinga mmoja hawezi kuvuruga amani ya nchi wetu, Naamini inteligency iko stable ivo JPM bado atakuwa mshindi tena kwa kishindo tu
Hapo ndipo mnapofeli mataga.
Taasisi zinazompenda JPM zimemwambia wazi kuwa kushinda kwake "kihalali" ni 50% kwa 50%.
Wasaidizi wake wanaomdanganya ndio nyinyi mnaomwambia "Mh, utashinda kwa kishindo,usiwe na hofu".
Ukweli halisi ambao haujapakwa virembeshi na ambao yeye Mh. Rais anaujua ni kuwa uchaguzi huu,bila ya kutumia figisu kama za NECccm, POLIccm, TISsccm na uzandiki, uharamia na figisu, basi atakuwa rais wa kwanza wa awamu moja TZ.
 
Mimi nadhani hakuna haja ya kuwa na wasiwasi, siasa ni mchezo mchafu, msitake leo uwe mchezo msafi!

Uchaguzi utafanyika na maisha yataendelea kama kawaida! Haya yanayoendelea ndicho kinachoitwa homa ya uchaguzi kupanda!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom