Inaashiria kuwa CCM imepoteza umaarufu

mzamifu

JF-Expert Member
Mar 10, 2010
6,379
3,826
kwa kuchunguza kwa makin,i kuna ishara kuwa CCM imepungua umaarufu kwa kasi.
Zamani CCM ilikuwa maarufu sana kiasi kwamba mtu yeyote akiteuliwa kugombea nafasi ya uongozi kupitia CCM alikuwa na nafasi kubwa ya kushinda.
Kwa sasa mtu ndani ya CCM ndiye aweza kuwa maarufu pekee sio chama tena.
ushauri kw CCM ni kuwa katika chaguzi zijazo itabidi kitafute watu maarufu wanaokubalika na wapiga kura la sivyo kitabwagwa tu.
Pia chama kiwe makini tangu sasa kujua ni nani anatazamiwa kugombea urais ili aanze taratibu kujenga imani kwa wananch. Bila hivo CCM wajiandae kuondoka madarakani maana bila mtu makini na mwaminifu ndani ya CCM hakuna nafasi tena ya kutawala.
 
kwa kuchunguza kwa makin,i kuna ishara kuwa CCM imepungua umaarufu kwa kasi.Zamani CCM ilikuwa maarufu sana kiasi kwamba mtu yeyote akiteuliwa kugombea nafasi ya uongozi kupitia CCM alikuwa na nafasi kubwa ya kushinda. Kwa sasa mtu ndani ya CCM ndiye aweza kuwa maarufu pekee sio chama tena.ushauri kw CCM ni kuwa katika chaguzi zijazo itabidi kitafute watu maarufu wanaokubalika na wapiga kura la sivyo kitabwagwa tu.Pia chama kiwe makini tangu sasa kujua ni nani anatazamiwa kugombea urais ili aanze taratibu kujenga imani kwa wananch. Bila hivo CCM wajiandae kuondoka madarakani maana bila mtu makini na mwaminifu ndani ya CCM hakuna nafasi tena ya kutawala.
Umaarufu wa CCM unashuka kwa kasi ya ajabu sana. Mbaya zaidi kwenye chaguzi hata zile kura za vijijini zimeanza kupungua, hii ni hatari kubwa sana kwa hiki chama. Hali mbaya kiliyonayo hivi sasa imechangiwa kwa kiasi kikubwa sana na udhaifu mkubwa sana wa mwenyekiti na mtandao wa 2005. Kwanza mwenyekiti hana uwezo wa kuongoza chama chake vizuri ikiwemo ukosefu wa ujasiri wa kuwajibisha wanachama wake wenye kashfa na wale wasio na uwezo kiutendaji! Anaongoza ki-shikaji zaidi. Pili makundi tofauti tofauti yanayohasimiana ndani ya chama hiki yanazidi kukimaliza. Makundi haya yalisababishwa na mtandao uliomwingiza mwenyekiti wao madarakani. Mpaka sasa hivi hakuna ambaye anaonekana anaweza kukinusuru chama hiki kwani kwa style yao ya kuchukia yeyote mwenye kusema ukweli na kukemea maovu wanazidi kujichimbia kaburi. Hata wale vijana ambao tulitegemea walete mabadiliko kama nape, Januari, Nchemba na wengine nao ni hovyo kuliko maelezo! Mtu kama Lusinde unategemea msaada gani kwa chama chake kama sio kukimalizia kabisa!!!! Hawana mbinu mpya wala ubunifu wa kukirudishia chama chao mvuto! CCM kwa heri 2015!! CDM Karibu sana!!
 
Ebwana iyo kali kweli kuna famili zenye ufahamu cjui kwa lio utapiamlo wa ccm nawapa pole, kwa maana watoto wengi wanakua vibaka kutokana na wizi wa mali za umma unafanywa na baba zao kwailo kwakel wanahitaji dawaaaaaaaaaaaaaaaaa.
 
kwetu ukitaka watu wa kugombea balozi za ccm inabidi uwakamate kama enzi za kodi ya kichwa.
 
CCM haina chake tena. Mpaka watoto wa chekechea hawaipendi ccm. Vijana wa sekondari ndo kabisaaaa! Nakumbuka kijana wangu wa pili alipokuwa na miaka 2 aliipenda CDM kila akisikia muungurumo wa ndege yeye alijua ni Mbowe tu! Utasikia anasema Mbowe, Mbowe, Mbowe. Sasa hivi wanamtania mama yao kwamba ccm yao imefulia!
 
Hata wakimweka msafi ka malaika CCM ni kansa hata yy ataugua tu,cha msingi ni kumwondoa huyu mdudu CCM na vizalia vyake vyote ili maisha yaweze kuwepo
 
SIKONGE kuna ka mti kanaitwa MNYANGALA na ukikagusa na kukaambia wewe ni CCM, Kananywea kabisa kama kamekufa.
 
Mi mtoto wangu aliota ndoto mbaya yaani kama zimwi linamkaba lilimtesa sana, alipoamka asubuhi akanihadithia nikamwambia ni li ccm hilo, sasa hadi leo hana hamu na li ccm anasema ccm ni wauwaji walitaka kumuua,
 
Chama chenyewe kimebaki ni cha viongozi na wanafamilia wao.
Sie wengine tumeamua kuwaachia ili tuone watafika wapi na uroho wa kututawala milele.


KADI YA CCM INAUNGUA_1.jpg
 
Mtoto wangu (3yrs) ukimwambia yeye ni CCM...anasusa hata kula mpaka umuombe msamaha....

Hii ya kwako inaweza kuwa ni utani lakini mtoto wangu ukweli ni kwamba akiambiwa CCM oyee anajibu people's powa; ana miaka 3 na miezi mi 4. Anajiita Kamanda; Ni habari za kweli.
 
Back
Top Bottom