In case You missed it: Watch Darwin's Nightmare!

In case You missed it: Watch Darwin's Nightmare!

Nimeangalia filamu yote. Nilichokiona hakina tofauti na wale wanaookota makopo ya maji kujipatia fedha. Ila filamu hii imeonesha kama mtu mmoja katika mahojiano alivyosema kuhusu dunia, na kwa Tanzania ni nchi ya "Law of the Jungle". Kuna watu wacahche sana wanaifidika na rasilimali na wale walio nje ya system ya rasilimali ndiyo wanabaki kuwa wakusanya mabaki.

Mambo yaliyo nikwaza katika filamu hii na kuitupia lawama Serikali
  1. Kuruhusu watu kutumia ma-pank kama sehemu ya kujipatia chakula, ina maana kuwa hatuna mabwana afya, hatuna authorities yaani hii inanikumbusha na stori ya watu kuuziwa mizoga ya ng'ombe waliokufa. Mapank mpaka yanatoa funza watu wanayaandaa na kuyarudisha sokoni hili limenikwaza sana
  2. Mazingira ya uvuvi ziwa Victoria ni mabovu sana, hali ya uchafu na afya za wakazi wanaozunguuka maeneo hayo ni tishio kwa biashara hiyo nje ya nchi.
  3. Ugonjwa wa Ukimwi unaonesha unasambaa kwa kasi sana kwenye jamii za wavuvi.

Pia inaonesha kuna more than biashara ya samaki, haiwezekani ndege ije empty kutoka Europe kwa ajili ya kubeba samaki. Ningetarajia consumer goods zingekuwa zinaingizwa ila kwa style inavyoonekana kuna illegal arms deals associated with business na viongozi wa nchi probably wanafahamu kila kitu.

Haitoshi tu kwa JK na wabunge kulaani filamu kwa kuwa inawavua nguo viongozi wanaotakiwa kuhakikisha wananchi wanaishi maisha bora bali wachukulie filamu hii kama changamoto ya kuyashughulikia matatizo ya wananchi na kuwatoa katika dimbwi la umasikini
 
Ahhh jamani mbona mnanitia uchungu makusudi hivi nilisha anza kusau Nightmare hii..Yaani wee acha tu.
 
Back
Top Bottom