In case You missed it: Watch Darwin's Nightmare!

In case You missed it: Watch Darwin's Nightmare!

Mzee Es

Kwenye hili ninakungoja sana usee lako la mwish ukiwa tayari lakini naona umeanza kuchukua side maana umeanza kuhoji sana ujaji wa mzungu huyu Tanzania na tabia za wazungu .Ila nasema ukweli ni mwingi sana katika filamu ile na ni 98%
 
Ni kweli nimeanza kuchukua side,

Maana sielewi huyu mfaransa alivyoshindwa kutengeneza cinema ya jinsi wazungu wenziwe wanavyowaumiza vijana wa kiaarabu huko kwao, ambapo tuliona dunia nzima wakati wa machafuko, sasa ningetegemea huyu mzungu angekuwa na more interest kuionyesha dunia kuwa hao waarabu hawaonewi na yeye na serikali yake ya France,

lakini akavuka bahari na milima, miti, nchi mbali mbali mpaka kufika Mwanza na akayaona mapanki tu? Halafu kule US niliulizwa mara nyingi na African Americans jinsi nilivyokwenda uchi na kupewa nguo Airport!

Ndio maana tayari nimeanza kuchukua side!
 
Mzee Es said:
Ni kweli nimeanza kuchukua side,

Maana sielewi huyu mfaransa alivyoshindwa kutengeneza cinema ya jinsi wazungu wenziwe wanavyowaumiza vijana wa kiaarabu huko kwao, ambapo tuliona dunia nzima wakati wa machafuko, sasa ningetegemea huyu mzungu angekuwa na more interest kuionyesha dunia kuwa hao waarabu hawaonewi na yeye na serikali yake ya France,

lakini akavuka bahari na milima, miti, nchi mbali mbali mpaka kufika Mwanza na akayaona mapanki tu? Halafu kule US niliulizwa mara nyingi na African Americans jinsi nilivyokwenda uchi na kupewa nguo Airport!

Ndio maana tayari nimeanza kuchukua side!

Mzee ES!

Naona wewe mgumu kuamini. Nafikiri bado unataka kurudi miaka ishirini nyuma enzi za bodi ya pamba, kahawa, chai, n.k. Hawa wakulima walijitahidi kuinua maisha yao lakini at the end of the day, wakuu wa bodi ndio walionufaika. Wakulima wenyewe hata tofali hawakuweza kununua. Natumaini ulivyokuwa US kama tunavyosikia Starbucks huwezi kunywa kahawa kama ulipwi vizuri. Ninachotaka kusema ni kwamba, Tanzania tuna rasilimali kibao, lakini zinaishia mikononi mwa wachache. Huyo jamaa aliyechukua hiyo film kwa mawazo yangu aliona MAENDELEO Tanzania lakini inategemea hayo maendeleo unayapima vipi. Yeye aliona maendeleo yanaenda chini (downfall and not improvement). Naweza kukupa mifano mingi sana toka mkoloni aondoke hakuna chochote kilichoendelea zaidi ya nyumba za wakubwa kuwa na vitu vya kifahari ambavyo mshahara wa mfanyakazi au meneja hawezi kuwa navyo siajabu maishani. Sio maji mijini kuwa shida, umeme eti bwawa halina maji, hospital hakuna vifaa hata vitanda, shule hazina vifaa, vyuo vina-computer za kuhesabika, list ni kubwa sana.

Fungua macho uone.
 
Pengine hata Forrest Whitaker na "The Last King of Scotland" yake atalaumiwa kwa vile yeye sio Mganda...

sense of the word “art” is roughly as an abbreviation for creative art or “fine art.” Here we mean that skill is being used to express the artist’s creativity, or to engage the audience’s aesthetic sensibilities, or to draw the audience towards consideration of the “finer” things...The purpose of works of art may be to communicate ideas, such as in politically-, spiritually-, or philosophically-motivated art, to create a sense of beauty (see “aesthetics”), to explore the nature of perception, for pleasure, or to generate strong emotions. The purpose may also be seemingly nonexistent...An art form is a specific form for artistic expression to take, it is a more specific term than art in general, but less specific than “genre.” Some examples include, but are by no means, limited to:

* painting
* drawing
* sculpture
* music
* poetry
* architecture
* CINEMA (here comes Hurbert Sauper's Darwin's Nightmare!)
 
Unjua cinema inayohusu Idd Amin, an-African inapoitwa The Last King of Scotland, ninakuwa na wasi wasi tayari hata kabla ya kuiona!

Ndugu Tatu,

Kwanza karibu ndugu yangu, halafu nimekuskia isipokuwa samahani kwenda shule maana yake ni kuanza kuangalia mambo kwa objectiveness, sikatai uliyoyasema, ila hata huko majuu yapo, kwa hiyo sio mbaya sana, kiasi ulichosema!
 
1.Idi Amin Dada (c. 1924–August 16, 2003) was an army officer and President of Uganda (1971–1979). His tenure witnessed much sectarian violence, including the persecution of the Acholi, Lango, and other ethnic groups as well as Christians in Uganda. The death toll during Amin's regime will never be accurately known. An estimate from the International Commission of Jurists is that it was not less than 80,000 and more likely around 300,000. Another estimate, compiled by exile organisations with the help of Amnesty International, put the number killed at 500,000.

He gave himself the title "His Excellency President for Life Field Marshal Al Hadji Dr. Idi Amin, VC, DSO, MC, King of Scotland, Lord of All the Beasts of the Earth and Fishes of the Sea and Conqueror of the British Empire in Africa in General and Uganda in Particular."

2.The Last King of Scotland is a UK film based on Giles Foden's award-winning debut novel of the same name. It was adapted by screenwriters Peter Morgan and Jeremy Brock, and directed by Kevin Macdonald. It received a limited release in the United States on September 27, 2006, with a UK release set for January 12, 2007 and German release for May 17, 2007.

Forest Whitaker stars as the Ugandan dictator Idi Amin, and James McAvoy as Dr. Nicholas Garrigan; Gillian Anderson as the health-aide wife of the doctor (Adam Kotz) with whom Garrigan first works in Uganda; Kerry Washington, one of Amin's wives, and Simon McBurney a British diplomat.
Co

http://www2.foxsearchlight.com/thelastkingofscotland/
 
Kwa hiyo mzee wangu ilikuwa ni lazima iitwe hilo jina, kwa nini isingeitwa "The Man who bought Real Estate In New York", yaani lile jengo alilonunua pale karibu na UN na ambalo leo linaipatia taifa la Uganda hela za kutosha kuendesha Foreign ministry yao, na mission yao pale UN?

Je hii part ipo kwenye hiyo movie?
 
Sijafika New York ila nimesikia hivyi..

Kutokana na mambo mengi mabaya aliyofanya Iddi Amini. Kuna mengine mazuri kafanya ambayo yatamfanya akumbukwe tuu mpaka leo.

Moja ni kwamba.. kuna jengo kubwa katengeneza New york. yani sio kakodi ila kanunua kiwanja na akajenga na ndio mahali ubalozi wa Uganda ulipo sasa. sasa hii nasikia mara ya pili kutoka kwako Mzee ES.

Vipi, unaweza kutuelezea kidogo kuhusu hilo jengo..

Asante

JeiKei..
 
Oh Yah! Hili jengo lipo pale 44Th, street na First Avenue, sio hadithi mimi nimeshaliingia mpaka ndani na kuna maofisi ya mabalozi mengi ya kiafrika yanakodi kuwemo humo kwa serikali ya Uganda, na linaitwa Uganda House, linaangaliana na UN building ambako ndani kuna executive suite ya katibu wa UN,

sasa ninasubiri part ya hii issue ya Idd Amini alipoikuwa analinunua hili jengo na ninawaomba wale wote mtakaoiona hii movie mtusaidie maana unaiweza kuja Afrika imekatwa katwa vipande!
 
Mimi sina hakika kwanini director wa "The Last King of Scotland" aliamua kutumia title hiyo,lakini nakumbuka kwenye enzi za sekondari mwalimu wa Literature alituambia kuwa the more satiric,ironic and eye-catching a filamu title is,the more curiosity and interest it generates among movie-goers.Moreover,kwenye cut-throat competition iliyopo in the movie industry,mtengeneza filamu inambidi afanye kila jitihada kuwa-convice waenda sinema why should they watch filamu yake.By the way,baadhi ya wafuatiliaji wa mambo ya filamu wameshaanza kumtabiria Whitaker na filamu hiyo kwenye next Academy awards (refer http://www.star-ecentral.com/news/story.asp?file=/2006/10/5/movies/20061005084611&sec=movies)
 
Part: 1

Cinema ya Mapanki, iligharimu jumla ya Euro 323,000 ambazo zililipwa na kampuni ya CNC, na pia kampuni ya Arte/WDR, za Ufaransa, ambapo kampuni ya kwanza ilitoa Euro 160,000 na zingine kumaliziwa na kampuni ya pili.

Nia na madhumuni yake, ilikuwa kuonyesha jinsi Watanzania wanavyoishia kupewa mabaki yaliyooza ya vichwa, na mifupa ya samaki wa aina ya sangara, huku minofu yake ikipelekewa wazungu huko Ulaya.

Tatizo ni kwamba, wakaazi wa Mwanza huwa hawali samaki wa aina ya SANGARA maana hana ladha kabisaaa, bali hula samaki waitwao SATO! Halafu kuuhusisha umasikini wa baadhi ya wananchi wa Mwanza kwa kutumia mapanki ni kutowapatia haki wananchi hao, na taifa letu kwa ujumla.

Pia samaki hao wa aina ya SANGARA, ni samaki wa kupandikizwa kwa ajili ya biashara na sio wa asili kama SATO, kwa hiyo samaki hao wa aina ya SANGARA, ni samaki wanaofahamika na jamii nzima ya MWanza kuwa ni wa biashara tu ya kuwauzia waliokuja kuwapandikiza, yaani Wazungu, na si kwa ajili ya chakula chao, na wanachi huwaangalia samaki hao kwa mashaka makubwa over the fact kwamba ni wa kupandikizwa na wazungu, sasa iweje leo wawe ndio chakula chao tena waliooza na hasa vichwa? Hivi ni kweli this makes a sense?

In a contrary, Biashara hiyo ya minofu ya samaki imeiletea Mkoa wa Mwanza mafanikio makubwa kimaendeleo, na sasa ni wazi kuwa taifa letu linahitaji kuweka mkazo wa kujenga viwanda vya kusindika samaki katika maeneo hayo ya ziwa, lakini hatuhitaji Mzungu toka Ufaransa kuja kutuambia hilo!

NEXT: Biashra ya ukahaba na silaha!
 
Habari wakuu!! Mwaka 2005 kama siyo 2006 nikiwa o-level pale St.Kayumba nilikuwa nikisikia issue fulani kuhusu filamu ya "DARWIN'S NIGHTMARE" ikiyotengenezwa na HURBERT SAUPER ila kwa vile nilikuwa bado kinda nilikuwa sielewi chochote kuhusu filamu hiyo.Leo katika pekuapekua katika magazeti ya enzi hizo hapa home nikakutana na habari inayoihusu hii filamu ila mengi ya magazeti haya yalikuwa yakiiponda sana so nikashindwa kuelewa chochote.Kwa vile nina ki-nokia changu cha 6030b ambacho kina~support net nikaamua ku~GOOGLE nikagundua kuwa filamu hii inazungumzia kuhusu minofu ya samaki wa ziwa viktoria inavyosafirishwa kwenda nchi za Ulaya na kuuzwa katika maduka na shoprite za Ulaya huku wenyeji wanaozunguka ziwa hilo wakila mabaki ya samaki waliokwisha ondolewa minofu maarufu kama mapanki,pia inaelezea kuhusu ndege zinazotoka Ulaya kuja kuchukua minofu hiyo kuwa huwa haziji tupu bali huja na silaha baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa Mwanza silaha hizo husafirishwa kwenda kwa waasi wa nchi za Kongo,Rwanda,Burundi na Uganda nyakati za usiku.Pia inazungumzia kuhusu wananchi wa Tanzania walivyo masikini huku maliasili zao zikiliwa na wachache ambapo kutokana na umasikini wadada wa maeneo hayo wamegeuka kuwa machangudoa n.k.Baadaye nikajiuliza maswali yafuatayo:1)Hivi haya yanayoongelewa katika filamu hii yana ukweli ndani yake?.2)Kama ni kweli TANZANIA inawezaje au inathutu vipi kuruhusu viwanja vyake vya ndege kutumika katika jambo la hatari kiasi hiki?.3)Sheria za kimataifa zinasemaje kuhusu suala la kusafirisha silaha kwenda kwa waasi kupitia nchi fulani?.OMBI:kwa yeyote mwenye details zaidi kuhusu filamu hii aongezee hapa.Pia naomba nisaidiwe kupata majibu ya maswali hapo juu(ni katika kujifunza tu).SOURCE~wikipedia& darwinnightmare.com.NAWASILISHA
 
Dah! Ahsante kwa info me mwenyewe ndio nimeanza kutambu. Thanks God JF inanipa hoja za kuchangamshia vijiwe vya Shule (Sangu High) pale muda wa Break.
 
Kikwete alikanusha kwamba Sauper hajauonyesha ulimwengu ukweli, eti Mwanza hawali mapanki, CCM waliandamana kuunga mkono hotuba hiyo.
 
Pamoja na CCM kuandamana,je hii ilikuwa na ukweli japo kidogo?
 
Back
Top Bottom