Niliyemuazima hakunirudishia miaka mine iliyopita. Sasa sijui kudhalilika kunakujaje. Kifupi,samaki anatolewa minofu inayopakiwa kwenye ndege kwenda kuuzwa nje kwa pesa nyingi! Wanaonyesha,mabaki ya kichwa na mfupa wa kiwiliwili,ndivyo vinavyoliwa pwani ya ziwa Victoria. Na maisha ya pwani hayo, uchangudoa,pombe haramu na za kienyeji, vibanda hasara,watoto wa mitaani wanavuta na kujifunza kunusa petroli,n.k. kisha ndege iliyopeleka nchi za nje minofu, inarudi na silaha[zilikuwa zinapelekwa nchi za jirani kwa waasi]. Darwin anaonyesha bila kuficha sura halisi ya tatizo. Watanzania tuna tatizo la unafiki na kutokuwa wazi. Kufunika chini ya kapeti matatizo.Wakati unapoweka wazi ndiyo mwanzo wa utatuzi wa kudumu.Mfano ajali za meli. Darwin alifanya kazi ambayo ingefanywa na tume ya watu kadhaa,na kulipwa mamilioni,na wakati mwingine wasifichue kila kitu,kwa vigezo dhaifu hivyo hapo juu.. Watanzania tubadilike!