In case You missed it: Watch Darwin's Nightmare! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

In case You missed it: Watch Darwin's Nightmare!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Willo, Apr 20, 2006.

 1. W

  Willo Member

  #1
  Apr 20, 2006
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 17
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Naomba wenzangu kama mkipata nafasi mngejaribu kuangalia documentary movie kuhusu uvuvi wa smamaki mkoani Mwanza. Mimi nieiangalia na kuna mengi sana nimegundua yanatakiwa yajadiliwe

  Nchi yetu utafikiri haina uongozi,yaani utafikiri bado tuko katika karne za kale sana ambazo zilikuwa hazijali kutafuta ufumbuzi wa matatizo yanayowakabili raia wake.Nimetishika sana mambo niliyoyaona mle ndani hii inaonyesha jinsi gani JK alivyorithi matatizo mengi kutoka kwa rais BM amabaye hakutaka kuyatatua katika kipindichake cha uongozi.

  Kama kuleta mabadiliko ninaomba rais JK aangalie kwa kina zaidi biashara nzima ya samaki ziwa victoria badala ya kuachia wahindi wachache pamoja na warusi wakiendelea kunufaika kwa kupitia migongo ya wazawa.

  Inatisha na kuhuzunisha sana naombeni muitafute hiyo document ambayo hivi sasa imeishatoka kwenye DVD. Kazi kwenu wakubwa.

  Peace!!!
  Willo

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 2. Kitila Mkumbo

  Kitila Mkumbo Verified User

  #2
  Apr 21, 2006
  Joined: Feb 25, 2006
  Messages: 3,347
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Willo: Inapatikana wapi hiyo hasa kwa sisi tulioughaibuni?

  Ningependa kuiona hiyo maana kwa jinsi ulivyoandika, inaonekana inasikitisha.

  Lakini umenisikitisha pale unapomtoa JK katika kundi la kina Mkapa. Kumbuka yeye alikuwa kiongozi tena katika ngazi ya uwaziri tangu kipindi cha mzee Ruksa. Na hayo uliyoyaona yalianza tangu kipindi cha mzee Ruksa. isitoshe JK amekuwa mjumbe wa Kamati Kuu tangu enzi. Na hiki ni kikao cha sera cha serikali ya ccm. So, JK as much as he can be a part to the solution, he was and has always been a part of the problems Tanzania is facing.

  At the end of the day, the problem is not the driver, it is the car he is driving. We may have had good drivers, but they have been driving bad cars that cannot be repaired and they indeed need to be changed. If you think JK is a good driver, I am afriad he is driving an unrepairable car called CCM.

  In the long run, Tanzanians need to buy a new car.
   
 3. W

  Willo Member

  #3
  Apr 22, 2006
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 17
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kitils, kama upo North America nenda kwenye blooooockbuster yeyote ile au Rogers utaweza kuipata hiyo documentary film tayari imewekwa kwenye DVD ,inasikitisha sana mambo niliyoyaooooona humo ndani ni masikitisho matupu jinsi hali za wanannchi zinzvyozidi kushuka chini wakati wageni wanaendeelea kujinufaisha kupitia katika migongo ya wazawa.

  Vile vile watanzania hawahitaji kuwa na magari mapyya ,labda ungesema tunahitaji mafundi wazuri sana wa kuyatengeneza magari hayo yaliyochoka.Vile vile JK kama waziri katika serikali ya Mkapa ilimuiuwia vigumu sana kutoa mawazo ya kuleta mabadiliko nchini ukizingatia tabia ya Mkapa yakutoooosikiliza mtu.

  NI huyu huyu JK ndiye aliyelalamika kwa Mkapa kuhusu yule professor wa wizi (Mahalu) na majibu yalikuwa mabaya sana kutoka kwa mheshimiwa Mkapa yaani hakupenda Kikwete kuhoji kuhusu Mahalu JK nayoyafanya hivi sasa ni mambo ambayo alishindwa kumshauri Mkapa kuyafanya wakati akiwa rais kwa hiyo kujaribu kumwingiza waziri yeyote aliyefanyakazi chini ya Mkapa na kumpa lawama za Mkapa ni makosa.

  nawaombeni mtafute hiyo dooooocumentary film na baadaye kuna mengi ya kujadili baada ya kuona uchafu uliokuwemo ndani yake.

  peace!!!
   
 4. M

  Mkira JF-Expert Member

  #4
  Oct 3, 2006
  Joined: May 10, 2006
  Messages: 425
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
 5. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #5
  Oct 3, 2006
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,065
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
 6. t

  tafiti then jadili Senior Member

  #6
  Oct 3, 2006
  Joined: Aug 24, 2006
  Messages: 119
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  unaweza pia kuiona through this web kwa kusearch under DARWIN'S NIGHTMARE

  www.youtube.com
   
 7. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #7
  Oct 3, 2006
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  Ndugu zangu sina uhakika na hii hadithi yote kwa ujumla, isipokuwa nimekutana na baadhi ya wabongo walioshiriki kwenye hiyo cinema na nimeziona mpaka risiti za hela walizolipwa na mzungu aliyetayarisha cinema hiyo,

  lakini bado nitaifuatilia, hii issue kwa makini maana sasa nitakuwepo huko North kwa muda mrefu, katika kufuatlia kesi ya ubunge ya mshikaji wangu Charles,

  sasa sijawahi kutoa comment kuhusu hii issue ya hii cinema, kwa sababu nilikuwa nataka ukweli kwanza, na bado sitoi my final comments mpaka niione ukweli ulipo, nimeishi US kwa muda mrefu sana, ninawajua wazungu na tabia zao za kuwaambia Africans Americans kuwa sisi waa-Afrika huwa tunakwenda majuu uchi na kupewa nguo Airport,

  Halafu bado kuna maswali ninajiuliza kuhusu huyu Mzungu aliyetengeneza hii movie, nia na madhumuni yake ilikuwa ni nini? Alitokea Europe kwa ndege akatua Dar kabla ya kwenda Mwanza, je toka siku alipotua Dar, mpaka kufika Mwanza, kitu cha maana alichokiona ni Mapamnki tu? Maendeleo yote tuliyonayo between Dar mpaka Mwanza, hakuyaona ila akaona mapanki tu na yakamwingia mpaka kuamua kuyafanyia cinema? Halafu kwa wale wakazi wa Mwanza, eti ni kweli Mwanza kuna masikini wa kufikia hatua ya kula samaki wabovu? Mbona watu wa huko North ya bongo ni watu proud sana, ikawaje hata wakakubali kuingia kwenye cinema ya kuwadhalilisha kiasi hicho?

  I smell Something not to be right na hii cinema, btu nitarudi na ukweli hapa hapa!
   
 8. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #8
  Oct 3, 2006
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Mzee ES,
  Mzungu huyo hakuwa mgeni Tanzania. Nadhani ameishi na kufanya kazi huko kwa miaka kadhaa. Mimi binafsi picha nimeiona. Eneo yanakotupwa yale mapanki nimepaona, nje tu ya Mwanza kwenye barabara ya kuelekea Musoma. Mimi nadhani tatizo ni kwamba baada ya wawekezaji kuanza kuuza samaki nje, ( kumbuka hawa wawekezaji si Watanzania) bei ya samaki ilipanda kote Mwanza na Musoma kiasi kwamba raia wa kawaida hakuweza kumudu bei yake. Hata kama Watanzania walilipwa ( hasa yule watchman) sidhani kuwa walikuwa coached on what to say. Ione kwanza picha halafu tujadili kwa kirefu.
   
 9. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #9
  Oct 3, 2006
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Halafu sikiliza mahojiano yangu na huyo mtengeneza filamu!
   
 10. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #10
  Oct 4, 2006
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  Mzee Jasusi,

  Heshima yako mkuu, ninaondoka kesho asubuhi kwa hiyo nitasikiliza mawazo ya mtu yoyote yatakayo nisaidia kule na ninashukuru kwa huo ujumbe wako kwani nitafika kote huko, na mjumbe yoyote mwenye ushauri wa namna ya kufuatilia kule kwa urahisi, nitayachukua na kuyafanyia kazi,

  Na Mzee Mwanakijiji, nafasi ya kusikiliza mahojiano sasa hivi imenipungua, lakini na unajua huko ninakokwenda umeme ndio hivyo, lakini nitayasikiliza nitakaporudi! na Ahsante!
   
 11. J

  JeiKei Member

  #11
  Oct 4, 2006
  Joined: Sep 29, 2006
  Messages: 51
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii Ndio Historia fupi ya bwana Sauper Kuja hapa nchini..

  Sauper alikuja kama Scientist, Researcher and Missonary.

  Alipokuja kama Scientist. Wizara ya Maliasili na Utali walimlinda sana. Alisema anataka kuchukuwa picha kwajili ya kutengeneza movie ya ziwa victoria. Kwasababu Wizara ilimuamini wakampa kila kitu. MPAKA POLISI kama mlinzi wake.

  Wakati ana piga shooting kuna baadhi ya watu walimchukuwa na kumfungia baadala yake akawa anapiga simu polisi anafuatiliwa kama vile sijui nani. Alipewa heshima kubwa sana.

  Mara ya pili alikuja kama Scientisit. kwahiyo akaingia katika malibarary ya wizara video clips zile akakopy nini na kila kitu.

  Sasa wakati anatengeneza ile movie. kibali kila kitu serikali ilimpa. serikali haikujua nia yake ni nini. alitengeneza vibali feki vya kuingia airport. alikuwa ana act kama mtumishi wa airport na vitu vingine vingi vya kishenzi.

  Sauper yani mtengenezaji Film alikuwa amejianda saaana. serikali haiwezi ikampiga vita..
   
 12. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #12
  Oct 4, 2006
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  Wazee wangu ninaomba samahani kwamba safari yangu huko North, ambayo ilikuwa pamoja na mengine kwenda kuifuatilia hii kesi, pamoja na mambo ya mapanki kule Mwanza, imebidi niikatishe baada ya kukaa kwa masaa machache pale Musoma, kutokana na shughuli za dharura hapa Dar, inayotokana na issue ya jirani zetu Kenya.

  Anyway, ninaahidi kuwa pindi tu nitakapopata nafasi, nitakwenda tena, jana nilidandia lift ya ndege ya jeshi, na hatimaye kurudi nayo, lakini tutazifuatlia hizi issue hata kwa mbali kwa makini, na kuuweka ukweli hapa hapa!
   
 13. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #13
  Oct 5, 2006
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,065
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Nadhani Michael Moore angekuwa Bongo saa hizi angeshatupwa Segerea kwa kutengeneza Fehrenheit 9/11.Kwa mtizamo wangu binafsi,documentary ya Sauper imeweza kueleza kile ambacho sie kama Watanzania hatuwezi kukifanya.Unajua acha Wakenya watuseme,sie tumezidi sana kujikomba kwa viongozi (hata humu kwenye forum wapo wanaojikomba kwa watawala...siwalaumu sana,mkono shurti uende kinywani).Mapanki kule mwanza ni sawa na tanzanite kule mererani,dhahabu huko chunya,mchele kule ifakara,mahindi in the "big four",nk nk.Documentary ya Sauper inaelezea ukweli mmoja ambao wengi tunaufahamu lakini hatuusemi.Asilimia kubwa ya wanaonufaika na utajiri wetu sio sisi,na kile tunachobaki nacho ndio sawa na mifupa ya samaki huko mwanza.Makaburu,Wathailand na wageni wengine ndio wanufaika wakubwa wa biashara ya madini,huku wenyeji wakiachiwa mashimo tupu (pindi mwamba ukiishiwa madini),TB (kwa kuchekecha mchanga wa madini) na STDs kwa akinadada wanaokwenda kutafuta maisha kwenye migodi.

  JK ni mnafiki kujifanya anamtolea macho Sauper baada ya kupata Urais,kwani siku zote alikuwa wapi?Hao waliojikomba "kuifanyia ufundi" tovuti ya documentary hiyo walikuwa wapi siku zote hizi kabla JK hajaiongelea?Ubalozi wa TZ Ufaransa nao ukakurupuka na tamko kuhusu documentary hiyo ilhali wao ndio waliompa visa ya kuja Bongo.hata kama aliwadanganya kuhusu madhumuni ya safari yake,bado wao ndio wako responsible kumwezesha jamaa huyo kuja Bongo.

  Only way to move forward ni kuachana na hii tabia ya kinafiki ya kujikomba kwa watawala.
   
 14. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #14
  Oct 5, 2006
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  Nimekataa kuwa na mawazo ya kitumwa, na ndio maana nikakimbia US, baada ya kumaliza shule tu, nikapanda ndege ya kwanza kurudi kunyumba,

  Eti mzungu akija bongo kutengeneza cinema, basi mimi Mtanzania sipaswi kuhoji the message ya hiyo cinema, na nikihoji ninakuwa ninajikomba kwa viongozi wa nchi yangu? na ninakuwa mnafiki? na unafiki huu unaiangusha nchi yangu?

  Kwa hiyo mzungu akija pale Margott, akatengeneza cinema ya mashoga usiku na kwenda kusema sisi wote wabongo ni mashoga, basi niamke kushangilia tu maana nikihoji ninakuwa ninajikomba kwa viongozi wa juu?

  Nimesema na ninarudia, sijawahi ku-comment kwenye hii issue, lakini baada ya kuonyeshwa risiti za baadhi ya waliolipwa kushiriki kwenye hiyo cinema, nimeamua kuifuatilia lakini sijatoa hukumu yangu ya mwisho, muungwana Jasusi kuheshiku mawazo yangu akaamua kunipa mpaka hints za namna ya kwenda kuzitafuta info vizuri, na mzee Mwanakiji akaniomba nisikilize mahojiano yake na mzungu katika safari yangu ya kutafuta ukweli?

  Sasa eti hapo ninafanya kosa la kuwa mnafiki na kujikomba kwa viongozi?
   
 15. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #15
  Oct 5, 2006
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,065
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Mzee ES,nadhani hii ndio personalisation of a debate.At no point umetajwa kuwa "Mzee ES anajikomba kwa viongozi".Usijishtukie,hujatajwa.Anyway,kwa mtazamo wako kumsapoti Sauper ni mawazo ya kitumwa,lakini still ni mawazo na watumwa ni watu pia.
   
 16. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #16
  Oct 5, 2006
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Mzee ES si mmesikia yale ya waamini kule Mtwara ambao wakaingizwa mjini na "watumishi wa Mungu"? Kisa ni wamarekani!!?
   
 17. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #17
  Oct 5, 2006
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  Umesahau wazungu walivyotushikisha Biblia huku wakigawana ardhi yetu? Maaan usitaje jina langu nasikia kichefu chefu bro, what is your point so far?

  Maana umesema kuwauliza wazungu maswali kwa faida yetu ni kuwa wanafiki? Sasa shule tumeenda ya nini?
   
 18. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #18
  Oct 5, 2006
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  nilikuwa naweka point hiyo hiyo, kuwa wabongo tunaabudu vya wazungu kiasi cha kwamba mtu ananyang'anywa mtoto na yeye anabakia kuchekelea!!
   
 19. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #19
  Oct 5, 2006
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  Great point bro!
   
 20. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #20
  Oct 5, 2006
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,065
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  May be JK na msafara wake pia lilikuwa kundi la watumwa kwenda kuwabembeleza Waamerika kuja kuwekeza Bongo as if that cant be done by watanzania wenyewe.By the way,the current international system essentially creates the masters (G8&co) and the slaves (3rd world countries).

  A satire:kama nchi na kiongozi wake inaamini kwenye utumwa (as definded by some),why not a mere mwananchi!
   
Loading...