Implementation ya activity za NGO na Tender ya kuimarisha kazi na mawasiliano yake

Barakaeli174

Senior Member
Aug 2, 2015
171
142
Ndugu wana JF

Tunaomba kuwasilisha tangazo hili kama kuna yeyote mwenye uwezo wa kuimarisha kazi na mawasiliano ya NGO ambayo imesajiliwa hapa nchini, kazi yake kubwa ikiwa ni kuboresha sector ya kilimo nchi nzima, ku support ukuaji wa biashara, kuchochea kasi ya baishara, kusaidia kuchochea mazingira ya biashara kwa kuboresha yawe mazuri zaidi ili wengi wapate ajira, yote haya yatafanyika katika ngazi ya kijiji, wilaya, tarafa na mkoa, haya yote kufanyika nchi nzima kwa uangalifu na ufuatiliaji na kwa ukaribu sana, tutashirikiana na serikali popote pale tutakapo hitaji msaada wao.

Toka NGO isajiliwe imeshafanya yanfuatayo:

1. NGO imesajiliwa mwaka 2014 Imeweza kuandaa sera za fedha na manunuzi na document zingine zinazohusiana na malipo.
2. NGO ina bodi ya wadhamini ambao ndio wanakaa na kuamua muelekeo na kuidhinisha matumizi
3. NGO toka ianzishwe imefanya kazi na online volunteers kutoka nchi mbalimbali na kati ya hao wengine walipata sifa ya kuajiriwa baada ya kupata uzoefu mkubwa kutoka kwetu.
4. NGO imeweza kuandaa ripoti ya fedha ya kila mwaka.
5. NGO ina tovuti yake, twitter na facebook (vitatajwa kwa atakayekuwa amechaguliwa au watakao kuwa wamechaguliwa)
6. NGO ina consultative status na Umoja wa Mataifa na imekuwa ikihudhuria vikao vya UN.
7.NGO imetambulishwa kwenye mashirika ya ndani na nje, na ni mwanachama wa Tangonet.

6. NGO imejipanga vyema kwa programu zake ili iweze kuwafikia wananchi nchi nzima sio kwa awabu bali kwa wakati muafaka

Hadi sasa NGO inahitaji kufanya yafuatayo:

1. Kwa miaka 5 ijayo kuanzia mwaka huu NGO inahitaji Kufanya tafiti za kubaini maeneo yenye uhaba wa mnvua na kuangalia uwezekano wa kutoa mafunzo ya mabadiliko ya tabia ya nchi na jinsi ya kukabiliana nayo kwa sababu uzalishaji umepungua kwa kiasi kikubwa na biashara nyingi ya mazao ya kilimo imebainika kupungua au kutoendelea katika maeneo hayo hata hivyo uongezwaji thamani katika vyakula vinavyo zalishwa umeathiriwa haya yatafanyika kwa ngazi zote kijiji, kata, tarafa, wilaya na mkoa.

2. NGO imepanga Kuwajengea uwezo watendani na wasimamizi kuhusu usimamizi na kuhakikisha miundo mbinu yote ya uzalishaji inaendelea kuwa bora na yenye manufaa kwa wananchi na serikali zoezi hili litafanyika ndani ya miaka 10 kuhakikisha nchi nzima katika ngazi zote wanafikiwa pale ambapo serikali na wadau wengine wamefanya tutaboresha zaidi.

3. NGO itatoa mafunzo kwa wakulima wote nchi nzima na si kwa awamu, hili ni katika ngazi zote kuhusu matumizi bora ya ardhi, maji na mbegu kila mahali ambapo kuna uhitaji wa matumizi kwa ajili ya uzalishaji hatuta bagua maeneo na kushauri mbegu sahihi kwa kila shamba kwa ngazi zote hii itaenda sambamba kila mkoa, kijiji, wilaya, kata na kitongoji kwa kipindi cha miaka 10 tunahitaji tanzania iwe mfano wa kuigwa katika uzalishaji ili iweze kuanzisha viwanda vya kuchakata na kufanya biashara ya mazao ya kilimo. Tutaari ma afisa ugavi 2 kwa kila wilaya ya Tanzania bara kwa kazi kubwa ya kutoa mafunzo na ushauri wakishirikiana na ofisi za kilimo za serikali.

4. NGO itatoa mafunzo ya ujasiriamali kwa makundi ya kina mama, vijana na kina baba jinsi ya kuchakata mazao, kuchangamkia fursa ya mikopo na biashara, jinsi ha kuboresha mazingira ya biashara, zoezi hili litafanyika nchi nzima kwa mkupuo kwa kipindi cha miaka 5 kila mwezi katika ngazi zote za kijiji, wilaya, kata, tarafa.

5.Tutakusanya mapendekezo ya wananchi kuhusu maeneo ambayo yanahitaji kuboreshwa kwa ajili ya biashara ili serikali iongeze mapato wanachi wajipatie kipato na mazingira ya biashara yawe mazuri hivyo tuta wasilisha kwa serikali ya eneo husika kwa hatua zaidi, zoezi hili litakuwa la kukusanya maoni kila mwisho wa mwezi ndani ya miaka 5 katika ngazi zote na tutakuwa tunatolea tathmini maeneo ambayo yameboreshwa na serikali na ongezeko la ufanyikaji wa biashara ambayo ndio lengo letu haswa.
6.Tutaendelea kujenga masoko mipakani pote na ambapo ni nyeti panahitaji soko, hivyo hata sehem zenye uhitaji mkubwa wa soko la wakulima ili kuchochea wafanyabiashara kujituma zaidi na kukuza biashara katika ngazi zote, zoezi hili litafanyika kwa kipindi cha miaka 10.
7. Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi


Anayesaidia kazi au atakaye toa fedha zake kwa ajili ya mradi ategemee yafuatayo

1. Kuwa na uzoefu, awe tayari kujituma, kubuni na kutoa huduma nzuri kama atakavyo hitajika,

2. Awe mzoefu wa kuwasiliana na wafadhili na mwenye lugha nzuri hata kama akikwazwa na wananchi anao watumikia ili kuendelea kulinda heshima ya NGO

3. Awe na uwezo wa kuleta fedha ndani na sio ategemee iliyopokuwa ataitumia, ahamasishe fedha (raise fund) kwa ajili ya kazi atakayo ifanya
4. NGO inayotaka kufadhili miradi yetu lazima itoe financial manager na human resource kusimamia rasilimali zao kwetu, mmoja kwa upande wake kwa ajili ya personel and fund management.
Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi.


Masharti kwa anaye saidia

1. Hata ruhusiwa kuwa msemaji hadi hapo atakapo teuliwa kufanya hivyo au atakapo ombwa kumuajiri au kumteua mtu,
2. Hata ruhusiwa kuweka taarifa zetu za fedha mpaka hapo atakapo ruhusiwa kufanya hivyo,
3. Hata ruhusiwa kutoa siri yoyote ila ya ofisi,
4. Hata ruhusiwa kuleta fedha haramu, hataruhusiwa kuingiza siasa za nchi kwenye miradi yetu, hata ruhusiwa kulazimisha na kutekeleza kile anachokitaka bila idhini ya 50% ya bodi ya wadhamini kupitisha.

Uliza maswali hapa inbox, ila kuandika maombi na utume kwenda info@aidfortradelogistics.org
 
Fafanua kidogo mtu wa kujitolea anawezeshwa namna gani mfano mim nina bachelor ya agribusiness, agricultural economic, or agricultural engineering & the related?

Je mnatoa ofa ya chakula?
Mnatoa ofa ya malazi?
Mnatoa ofa ya nauli?

Kujitolea kufanya hizi kazi ni kusaidia jamii and should be two ways. Suala la kupata uzoefu pekee bado halitoshi, motisha kiasi wahitajika, kumbuka watu wamesoma mambo yao kwa Shida sana.
 
Fafanua kidogo mtu wa kujitolea anawezeshwa namna gani mfano mim nina bachelor ya agribusiness, agricultural economic, or agricultural engineering & the related?

Je mnatoa ofa ya chakula?
Mnatoa ofa ya malazi?
Mnatoa ofa ya nauli?

Kujitolea kufanya hizi kazi ni kusaidia jamii and should be two ways. Suala la kupata uzoefu pekee bado halitoshi, motisha kiasi wahitajika, kumbuka watu wamesoma mambo yao kwa Shida sana.
Soma kwa kina uelewe, volunteer tumewahi kufanya nao kazi hilo neno limo kwenye text
 
Back
Top Bottom