Impala Hotel, Leopard Tours Offices kuvunjwa

DaveSave

JF-Expert Member
Joined
Nov 20, 2010
Posts
444
Reaction score
654

Habari za mida hii wandugu?

Katika kile kinachoonekana kuendana na kasi ya Rais wa awamu ya tano ndugu JPM, Manispaa ya jiji la Arusha imeanza operesheni ya kurudisha maeneo ya serikali yaliyohodhiwa na watu binafsi kinyume na sheria kwa kuandikia barua uongozi wa Hoteli maarufu jijini Arusha pamoja na Kampuni ya Leopards Tours Safaris kwa kuingia kwa kiasi fulani eneo lililokuwa la shule ya msingi ya serikali.

Najaribu kuambatanisha barua hiyo katika jukwaa hili.
 
Last edited by a moderator:
Kama serikali inatoa vibali watu wanajenga kuna haja gani kuwafata hao hao tena kuchukua vibali maana wanaendelea kutoa vibali watu wanajenga harafu hao tena wanakuja kuvunja...
 
pale ni karibu na shule kabisa asiyejua lazima abishe. mafisadi ni hatari.
 
Impala hotel hii ni ya lowasa,

Revenge at work,
Hamna lolote,
 
Kwa wote au wachache...??ulishawahi kusoma kitabu kiiywacho ANIMAL FARM...??

Haidhuru ilimradi umelitamka wewe ila ni lazima malengo ya serikali yafikiwe na sheria ikate. Wewe ulitaka zivunjwe ngapi ndo uridhike?
 
Nadhani kwa sababu ilikuwa ni enzi za Mkapa hivyo mamlaka tofauti ndio ilitoa kibali.Na unavyoelewa katika Nchi za ki-Afrika kujuana(nepotism) ni kwingi.This is Magufuli era,some will win while others will loose too.
 
Leopard kuna mjengo bado haujamalizika lile eneo lote mali ya shule ya msingi Kijenge.Kama mimi serekali mwakani wanafunzi wote wa darasa la kwanza wanaingia mjengoni bila chenga.
 
Rweye....siyo swala la mimi kuridhika...bali msumeno ukate mbele na nyuma.Je itawezekana au tufanye subira.
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…