simon mato
JF-Expert Member
- Sep 27, 2015
- 926
- 485
Ndugu wanajamvi;
Nikiwa kwangu nachukua muda kidogo natafakari hali ya nchi yangu kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni najikuta najuta sanaa na pengine kwenda mbali na kumlaumu Mola kwanini aliniweka kwenye ardhi yenye nuksi na mambo ya ajabu namna hii ila ghafla napatwa na ujasiri ukiniambia tulia neema inakuja "je hii neema ninayoambiwa ndo ukombozi ule ambao tunausubiri baada ya miaka 50 au? Yangu macho!
:UJASIRI WA LEMA NI FAIDA NA YA WATANZANIA:
Mwalimu. J. K Nyerere alishtakiwa na walowezi kwa makosa mengi ya kichochezi yote akiwa anapigania uhuru wa Tanganyika, hayati Nelson Mandela alitiwa hatiani kwa miaka 27 na makaburu yote alikuwa anapinga ubaguzi wa rangi.
G. LEMA yupo kisongo kwa kosa la uchochezi! Namsihi Lema kuwa ujasiri wake ndio kimbilio la wanyonge na Mwanasiasa yoyote yule anayepinga udhalimu anatakiwa asiogope kulala kisongo au kisutu. Ushujaa wa Lema unakuja pale kwenye kusimamia ukweli wa anachokiamini na kuiweka hadharani.
Katika mapambano ya sasahivi yaliyojaa uonevu wa kila aina tunamuitaji mtu jasiri kama G. Lema ambaye amung'unyi maneno, ambaye haogopi kulala kisutu au kisongo, ambaye haogopi kufilisiwa, ambaye yupo kufa kwa kile anachokiamini.
:MAFASHISTI WAONDOKE TUBAKI NA WATU WENYE FALSAFA NA DAMU YA UKOMBOZI:
Mwaka 2015 Kuna genge fulani bila kujali maslahi ya Taifa lilitaka kufanya uhuni ambao kwangu niliukataa tokea mwanzo ndipo tofauti zetu zilipoanza na baadhi ya wanajamii wezangu. mengi yamesemwa pengine ata kuzidi ninavojua mimi lakini "ALL IN ALL" kwa maoni yangu imetosha imetosha hili genge lingewaachia wenye sifa waongoze mapambano juhudi zao tumeziona zimetosha waachie wengine.
Baada ya uchaguzi wa mwaka 2015 tulitegemea strategies za kuomba msamaha kwa makosa ambayo yalifanyika chini ya MBOWE lakini la asha! Ndipo alipoendelea kuwatusi watanzania ya nguoni, kwamba leo hii E. lowasa na F. Sumaye wanaijua chadema kumzidi E. Wenje, J. Nasari mpaka wateuliwe kuwa wajumbe wa mkutano mkuu na CC ya chama watu ambao kuja kwao chadema bado imeacha giza nene mpaka leo wanafika tyuu na kuabudiwa kama sakramenti takatifu.
Huu ndio unyani ambao alikemea mch. Mtikila, mimi sijaona alilolifanyia Tanzania E. Lowasa la maana mpaka baadhi ya watu mnamuabudu kiasi hiki, bora ata mara 100 hayati Moringe Sokoine. Lowasa hana damu na dhamira ya dhati ya ukombozi ata figisu figisu zake za kuondoa katiba ya Warioba tuliona kwanini tumwabudu kiasi hiki vijana wezangu! Huu ni unyani wa hali ya juu.
Utakuta ata humu JF kila siku hakukosi post kuhusu E. Lowasa kwenye hili jukwa, ni nani huyu na kaifanyia Tanzania nini? Maana ata mwl. Nyerere hakuna post zake mda mwingine lakini huyu hukosi!! Huu pia ni Unyani wa hali ya juu. Yaani tunageuka kuwa watumwa wa watu, badala ya kuwa wa kwanza kuukemea huu utumwa unaotumaliza serikalini kupitia katiba mbovu unaotukandamiza.
-Lema yupo anasota kisongo kwa ajili ya kutetea watu wanyonge ila mafashisti na mabwenyenye wanakimbilia kugawana vyeo kule Nyasa, wao wapo kwa akiji ya vyeo.
-Ben Saanane kapotea kwenye mazingira ya kutatanisha hakuna majibu yanayoridhisha baada ya kuiwekea mkazo wa kumjua halipo mafashisti wanakimbilia kupeana vyeo kule nyasa
_Huyo mnayemwabudu kama sakramenti takatifu ndo vile kama hajui kuwa Ben Saanane kapotea, ndo hajui kabsaa kuwa Lema yupo jirani na yeye Kisongo pale yeye yupo busy mikoani kutafuta watu wanaomlaki na kumtukuza kama Yohana mbatizaji.
Hatuna tume huru ya uchaguzi ila watu wanakimbilia mkoani kulakiwa na kupokelewa na kuimbiwa na nyimbo za kutukuzwa baada ya kuishinikiza serikali tupate Tume huru kuna swala la katiba mpya hilo ndo wameshaisahau kabsaa.
Ila kwangu mimi naamini CCM imechoka na haina pumzi tena ya kuiletea maendeleo ndo maana kuna mambo ya ajabu kwelikweli hivo tuwe na subira tyuu mda si mrefu ukombozi unakuja ombi langu kwenu na kuwapinga na kuwaondoa hawa mafashisti kwenye mapambano ili tupunguze maadui kwenye hii vita.
Tunawataka vijana wenye fighting sprit kama Lema, Heche, Malisa, mnyika, zito, na, wengine tuuh ila wengine hawa huu ndio mlango wa kutokea kwa sababu wanamitego ya hatari usipotegua na wewe unakuwa nyani unaanza kuwatukuza na kuwaimbia. Angalia Lisu alichotufanyia watanzania kaingia mtegoni bila kujua na Msigwa hivohivo sasa hivi wanamtumikia OSANA bila kujua.
Sauti za wanyonge zimechoka kulia na ipo siku mungu atawajibu ila ni vyema tujifunze namna ya kukabiliana hili genge kabla kwenda kwenye field battle kwenyewe ili tupunguze maadui na mizigo mizito tuliyoibeba hii itatusaidia kushinda vita hii kwa haraka mno!
Ni wako kijana mtiifu, mzalendo na mwanaharakati wa kweli Tanzania.