Imetosha imetosha! Saa ya ukombozi inakaribia

Waswahili wanakumabia CHARITY START/BEGINS AT HOME......hili uliloandika hapa lingekuwa na maana iwapo na kama TUNGEONA HAMSHA HAMSHA ZA ARUSHA MJINI KUPINGA KUONEWA KWA LEMA....lakini mpaka sasa ni nziiiiiiiii hii inamaana ya kwamba WANA ARUSHA MJINI wameisha muona HUYU KIJANA hana makuzi na hastaili kuwa kiongozi wao.....Naamini na walio wengi wanaamini LEMA ndiye anaeleta picha mbaya ya MKOA wa ARUSHA kuonekana ni mkoa wa VURUGU maana kama angekuwepo mtaani mpaka sasa LAZIMA tu ARUSHA mabomu yangeishakuwa yamerindima LAKINI SASA HIVI ARUSHA NI SHWARI BALAA na watu wanaendelea na shughuli zao za kujipatia kipato AS IF NOTHING HAS HAPPENED.......
 
Maisha yenyewe yanatupelekesha KASI na hii hapa kazi tu. Tutapatia wapi Muda WA kujadili siasa. Wananchi wengi wana fuatilia mambo YOTE haya smart zinasaidia na ndicho kinachoweza kuleta mabadiliko
 
Mimi ni chadema.ila Lema hapana aisee.huwezi kumwita mwenzako shoga.acha kwanza ashike adabu kidogo.yaani ingekuwa kila mtu anatangaza alichokiota basi nchi ingekuwa ya ajabu.

..kuna mwana ccm ameporomosha matusi mazito mazito dhidi ya Maalim Seif Sharrif.

..sasa tunasubiri kuona kama na yeye atatupwa rumande na kunyimwa dhamana kama Godbless Lema.
 
kha, wakati hata maendeleo ya kesi yake watu hawajui! kashasahaulika tyr, very soon atapotea kbs ktk medan za siasa! mfikishie ujumbe huo ukienda mtembelea, kama unakwendaga kweli
 
Mlivyokuwa mnaimba wacha waisome nambaeeee....
Mlitegemea upinzani ndio watakaoisoma?
Mwishowe tunaona namba mnaisoma wenyewe mpaka mmefika mahali leo ETI na nyie mnajiita wana mabadiliko???
Duuu, kama filamu vile.
 
Mkuu kwanza naomba uweke ushaidi kama mimi niliimba ukifanikiwa najitoa rasmi JF! Katika maisha yangu kitu ambacho nakipinga na kumhusudu kumlaki na kumtukuza mtu hivyo kumuimbia mtu mimi kwangu mwiko ila kwa ukweli umeguka kuwa sindano za ganzi tulieni hivohivo muache blaa blaa!!!

Mtu mkubwa huoni aibu kumhusudu na kumtukuza binadamu kama wewe khaaa!!
 
..kuna mwana ccm ameporomosha matusi mazito mazito dhidi ya Maalim Seif Sharrif.

..sasa tunasubiri kuona kama na yeye atatupwa rumande na kunyimwa dhamana kama Godbless Lema.
Maalimu seif akienda mahakamani lazima huyo mtu akamatwe
 
Kwa mada hizi:huu ni ushaidi tosha wa uzalendo wa mleta mada!anaipenda nchi yake na ni muumini wa demokrasia!anakosoa na kujenga kotekote bila kuangalia ukada na ukamanda!

watu badala ya kushambulia hoja wanamshambulia mleta hoja!mleta mada ameandika kweli tupu!
Hawawezi kushambulia hoja ata siku moja kwa kuwa wengi wao ni watumwa kifikra, ndo walewale wakiona sura za viongozi wanaanza kuwahusudu na kuwatukuza kama watakatifu!! Na huu uzi ni imekuwa mwiba kwa watu wa aina hii!! Ila mimi naamini ukweli utabaki kuwa ukweli daima na milele
 
Tunakujua wewe
Focus na Mambo ya chama chenu ya CHADEMA hayakuhusu.
Nyie ndio mlokuwa Mstari wa Mbele kumkebehi Kamanda Lema na kuomba awekwe ndani
Leo eti ndio mnakuja na Hoja Mfu kuchonganisha

===========
By Mag3

Hizi ni baadhi ya mada alizoanzisha simon mato toka ajiunge na JF Sep 27, 2015 akisimulia Ikulu ilivyo mahali takatifu baada ya kukaliwa na shujaa wake

Mwendelezo wa safari ya Rais Magufuli na demokrasia ya wapinzani

SEHEMU YA TATU: SAFARI YA RAIS MAGUFULI NA DEMOKRASIA YA WAPINZANI
Wanaomhujumu Rais Magufuli hawa hapa
Mtandao hatari Tanzania unaoisaka Ikulu usiku na mchana
Mazuri na mabaya kwenye Utawala wa Magufuli haya hapa
List ya wanasiasa mashujaa wenye damu ya mageuzi Tanzania kwa sasa
Hili ndio Bunge la Tanzania, watanzania tustuke
CCM kushinda 2020 kwa kishindo, UKAWA kukumbwa na mtikisiko ambao haujawahi kutokea
Uswahiba wa kisiasa kwanini huwa unaishia kwenye jino kwa jino?

Naomba watakaomjibu wazingatie hii rekodi yake.

Duh Jf kiboko.mkuu umemwacha uchi kabsa
 
Duh Jf kiboko.mkuu umemwacha uchi kabsa
Kaa chini ufikirie kabla kuandika na kupost ameniacha uchi kwa lipi labda! Mimi si mfuasi wa kundi lolote ndio maana kama ni kushambulia kwa facts ni kotekote sasa wewe unajiona bingwa kuwa umeandika la maana!
 
jamaa ni contradictory, anamsifia lema kuwa ni shujaa anayepambana na ufashisti (akimaanisha magufuli ndie fashisti)
Lakini kwenye nyuzi nyingine alikuwa akiponda wapinzani walipokuwa wanadai magufuli ni kiongozi wa kiimla,
Usijifanye mjuaji sanaaa huku hujui lolote unaungaunga tuuh!! Mimi naishi kwa mawazo na fikra zangu siishi kwa kufuata nani anasema nini? Na kafanya nini!! Nyie endeleeni kumuimbia na kumtukuza OSANA
 
Simon umejitahidi kuandika. Yako mafuriko na ya ukoko. Lakini ni pendent kakwambia swala la Lema ni spiritual. Ili kile alichotumwa kukinena kitokee ni lazima kuwa hivyo otherwise Siyo ujumbe wa Mungu
 
Ndugu wanajamvi;

Nikiwa kwangu nachukua muda kidogo natafakari hali ya nchi yangu kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni najikuta najuta sanaa na pengine kwenda mbali na kumlaumu Mola kwanini aliniweka kwenye ardhi yenye nuksi na mambo ya ajabu namna hii ila ghafla napatwa na ujasiri ukiniambia tulia neema inakuja "je hii neema ninayoambiwa ndo ukombozi ule ambao tunausubiri baada ya miaka 50 au? Yangu macho!

:UJASIRI WA LEMA NI FAIDA NA YA WATANZANIA:

Mwalimu. J. K Nyerere alishtakiwa na walowezi kwa makosa mengi ya kichochezi yote akiwa anapigania uhuru wa Tanganyika, hayati Nelson Mandela alitiwa hatiani kwa miaka 27 na makaburu yote alikuwa anapinga ubaguzi wa rangi.

G. LEMA yupo kisongo kwa kosa la uchochezi! Namsihi Lema kuwa ujasiri wake ndio kimbilio la wanyonge na Mwanasiasa yoyote yule anayepinga udhalimu anatakiwa asiogope kulala kisongo au kisutu. Ushujaa wa Lema unakuja pale kwenye kusimamia ukweli wa anachokiamini na kuiweka hadharani.

Katika mapambano ya sasahivi yaliyojaa uonevu wa kila aina tunamuitaji mtu jasiri kama G. Lema ambaye amung'unyi maneno, ambaye haogopi kulala kisutu au kisongo, ambaye haogopi kufilisiwa, ambaye yupo kufa kwa kile anachokiamini.

:MAFASHISTI WAONDOKE TUBAKI NA WATU WENYE FALSAFA NA DAMU YA UKOMBOZI:

Mwaka 2015 Kuna genge fulani bila kujali maslahi ya Taifa lilitaka kufanya uhuni ambao kwangu niliukataa tokea mwanzo ndipo tofauti zetu zilipoanza na baadhi ya wanajamii wezangu. mengi yamesemwa pengine ata kuzidi ninavojua mimi lakini "ALL IN ALL" kwa maoni yangu imetosha imetosha hili genge lingewaachia wenye sifa waongoze mapambano juhudi zao tumeziona zimetosha waachie wengine.

Baada ya uchaguzi wa mwaka 2015 tulitegemea strategies za kuomba msamaha kwa makosa ambayo yalifanyika chini ya MBOWE lakini la asha! Ndipo alipoendelea kuwatusi watanzania ya nguoni, kwamba leo hii E. lowasa na F. Sumaye wanaijua chadema kumzidi E. Wenje, J. Nasari mpaka wateuliwe kuwa wajumbe wa mkutano mkuu na CC ya chama watu ambao kuja kwao chadema bado imeacha giza nene mpaka leo wanafika tyuu na kuabudiwa kama sakramenti takatifu.

Huu ndio unyani ambao alikemea mch. Mtikila, mimi sijaona alilolifanyia Tanzania E. Lowasa la maana mpaka baadhi ya watu mnamuabudu kiasi hiki, bora ata mara 100 hayati Moringe Sokoine. Lowasa hana damu na dhamira ya dhati ya ukombozi ata figisu figisu zake za kuondoa katiba ya Warioba tuliona kwanini tumwabudu kiasi hiki vijana wezangu! Huu ni unyani wa hali ya juu.

Utakuta ata humu JF kila siku hakukosi post kuhusu E. Lowasa kwenye hili jukwa, ni nani huyu na kaifanyia Tanzania nini? Maana ata mwl. Nyerere hakuna post zake mda mwingine lakini huyu hukosi!! Huu pia ni Unyani wa hali ya juu. Yaani tunageuka kuwa watumwa wa watu, badala ya kuwa wa kwanza kuukemea huu utumwa unaotumaliza serikalini kupitia katiba mbovu unaotukandamiza.

-Lema yupo anasota kisongo kwa ajili ya kutetea watu wanyonge ila mafashisti na mabwenyenye wanakimbilia kugawana vyeo kule Nyasa, wao wapo kwa akiji ya vyeo.

-Ben Saanane kapotea kwenye mazingira ya kutatanisha hakuna majibu yanayoridhisha baada ya kuiwekea mkazo wa kumjua halipo mafashisti wanakimbilia kupeana vyeo kule nyasa

_Huyo mnayemwabudu kama sakramenti takatifu ndo vile kama hajui kuwa Ben Saanane kapotea, ndo hajui kabsaa kuwa Lema yupo jirani na yeye Kisongo pale yeye yupo busy mikoani kutafuta watu wanaomlaki na kumtukuza kama Yohana mbatizaji.

Hatuna tume huru ya uchaguzi ila watu wanakimbilia mkoani kulakiwa na kupokelewa na kuimbiwa na nyimbo za kutukuzwa baada ya kuishinikiza serikali tupate Tume huru kuna swala la katiba mpya hilo ndo wameshaisahau kabsaa.

Ila kwangu mimi naamini CCM imechoka na haina pumzi tena ya kuiletea maendeleo ndo maana kuna mambo ya ajabu kwelikweli hivo tuwe na subira tyuu mda si mrefu ukombozi unakuja ombi langu kwenu na kuwapinga na kuwaondoa hawa mafashisti kwenye mapambano ili tupunguze maadui kwenye hii vita.

Tunawataka vijana wenye fighting sprit kama Lema, Heche, Malisa, mnyika, zito, na, wengine tuuh ila wengine hawa huu ndio mlango wa kutokea kwa sababu wanamitego ya hatari usipotegua na wewe unakuwa nyani unaanza kuwatukuza na kuwaimbia. Angalia Lisu alichotufanyia watanzania kaingia mtegoni bila kujua na Msigwa hivohivo sasa hivi wanamtumikia OSANA bila kujua.

Sauti za wanyonge zimechoka kulia na ipo siku mungu atawajibu ila ni vyema tujifunze namna ya kukabiliana hili genge kabla kwenda kwenye field battle kwenyewe ili tupunguze maadui na mizigo mizito tuliyoibeba hii itatusaidia kushinda vita hii kwa haraka mno!

Ni wako kijana mtiifu, mzalendo na mwanaharakati wa kweli Tanzania.
Huyu ni kada wa ccm leo anajifanya ni kada wa chadema!
 
Wewe hunijui na wala ata usijaribu kunijua! Ila tabia yako ya unyani huo nakuomba uiache tabia hiyo ya kunyenyekea na kuwalaki viongozi ndio imetufikisha apa tulipo
Anzisha Basi chama chako ili usinyenyekee mtu
 
Lema usimlinganishe na Nyerere wala Mandela Nyerere hakumtukana Malkia wala Mandela hakumtukana Vorewood. Nyerere na Mandela waliomba one man one vote Lema aliomba nini?
 
.....Umeongea dhati iliyo dhahiri mkuu, Sijaona bias katika bandiko lako hili nathubutu kusema hii ni miongoni mwa post bora za mwaka 2016 hongera mleta mada!
 
Ndugu wanajamvi;

Nikiwa kwangu nachukua muda kidogo natafakari hali ya nchi yangu kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni najikuta najuta sanaa na pengine kwenda mbali na kumlaumu Mola kwanini aliniweka kwenye ardhi yenye nuksi na mambo ya ajabu namna hii ila ghafla napatwa na ujasiri ukiniambia tulia neema inakuja "je hii neema ninayoambiwa ndo ukombozi ule ambao tunausubiri baada ya miaka 50 au? Yangu macho!

:UJASIRI WA LEMA NI FAIDA NA YA WATANZANIA:

Mwalimu. J. K Nyerere alishtakiwa na walowezi kwa makosa mengi ya kichochezi yote akiwa anapigania uhuru wa Tanganyika, hayati Nelson Mandela alitiwa hatiani kwa miaka 27 na makaburu yote alikuwa anapinga ubaguzi wa rangi.

G. LEMA yupo kisongo kwa kosa la uchochezi! Namsihi Lema kuwa ujasiri wake ndio kimbilio la wanyonge na Mwanasiasa yoyote yule anayepinga udhalimu anatakiwa asiogope kulala kisongo au kisutu. Ushujaa wa Lema unakuja pale kwenye kusimamia ukweli wa anachokiamini na kuiweka hadharani.

Katika mapambano ya sasahivi yaliyojaa uonevu wa kila aina tunamuitaji mtu jasiri kama G. Lema ambaye amung'unyi maneno, ambaye haogopi kulala kisutu au kisongo, ambaye haogopi kufilisiwa, ambaye yupo kufa kwa kile anachokiamini.

:MAFASHISTI WAONDOKE TUBAKI NA WATU WENYE FALSAFA NA DAMU YA UKOMBOZI:

Mwaka 2015 Kuna genge fulani bila kujali maslahi ya Taifa lilitaka kufanya uhuni ambao kwangu niliukataa tokea mwanzo ndipo tofauti zetu zilipoanza na baadhi ya wanajamii wezangu. mengi yamesemwa pengine ata kuzidi ninavojua mimi lakini "ALL IN ALL" kwa maoni yangu imetosha imetosha hili genge lingewaachia wenye sifa waongoze mapambano juhudi zao tumeziona zimetosha waachie wengine.

Baada ya uchaguzi wa mwaka 2015 tulitegemea strategies za kuomba msamaha kwa makosa ambayo yalifanyika chini ya MBOWE lakini la asha! Ndipo alipoendelea kuwatusi watanzania ya nguoni, kwamba leo hii E. lowasa na F. Sumaye wanaijua chadema kumzidi E. Wenje, J. Nasari mpaka wateuliwe kuwa wajumbe wa mkutano mkuu na CC ya chama watu ambao kuja kwao chadema bado imeacha giza nene mpaka leo wanafika tyuu na kuabudiwa kama sakramenti takatifu.

Huu ndio unyani ambao alikemea mch. Mtikila, mimi sijaona alilolifanyia Tanzania E. Lowasa la maana mpaka baadhi ya watu mnamuabudu kiasi hiki, bora ata mara 100 hayati Moringe Sokoine. Lowasa hana damu na dhamira ya dhati ya ukombozi ata figisu figisu zake za kuondoa katiba ya Warioba tuliona kwanini tumwabudu kiasi hiki vijana wezangu! Huu ni unyani wa hali ya juu.

Utakuta ata humu JF kila siku hakukosi post kuhusu E. Lowasa kwenye hili jukwa, ni nani huyu na kaifanyia Tanzania nini? Maana ata mwl. Nyerere hakuna post zake mda mwingine lakini huyu hukosi!! Huu pia ni Unyani wa hali ya juu. Yaani tunageuka kuwa watumwa wa watu, badala ya kuwa wa kwanza kuukemea huu utumwa unaotumaliza serikalini kupitia katiba mbovu unaotukandamiza.

-Lema yupo anasota kisongo kwa ajili ya kutetea watu wanyonge ila mafashisti na mabwenyenye wanakimbilia kugawana vyeo kule Nyasa, wao wapo kwa akiji ya vyeo.

-Ben Saanane kapotea kwenye mazingira ya kutatanisha hakuna majibu yanayoridhisha baada ya kuiwekea mkazo wa kumjua halipo mafashisti wanakimbilia kupeana vyeo kule nyasa

_Huyo mnayemwabudu kama sakramenti takatifu ndo vile kama hajui kuwa Ben Saanane kapotea, ndo hajui kabsaa kuwa Lema yupo jirani na yeye Kisongo pale yeye yupo busy mikoani kutafuta watu wanaomlaki na kumtukuza kama Yohana mbatizaji.

Hatuna tume huru ya uchaguzi ila watu wanakimbilia mkoani kulakiwa na kupokelewa na kuimbiwa na nyimbo za kutukuzwa baada ya kuishinikiza serikali tupate Tume huru kuna swala la katiba mpya hilo ndo wameshaisahau kabsaa.

Ila kwangu mimi naamini CCM imechoka na haina pumzi tena ya kuiletea maendeleo ndo maana kuna mambo ya ajabu kwelikweli hivo tuwe na subira tyuu mda si mrefu ukombozi unakuja ombi langu kwenu na kuwapinga na kuwaondoa hawa mafashisti kwenye mapambano ili tupunguze maadui kwenye hii vita.

Tunawataka vijana wenye fighting sprit kama Lema, Heche, Malisa, mnyika, zito, na, wengine tuuh ila wengine hawa huu ndio mlango wa kutokea kwa sababu wanamitego ya hatari usipotegua na wewe unakuwa nyani unaanza kuwatukuza na kuwaimbia. Angalia Lisu alichotufanyia watanzania kaingia mtegoni bila kujua na Msigwa hivohivo sasa hivi wanamtumikia OSANA bila kujua.

Sauti za wanyonge zimechoka kulia na ipo siku mungu atawajibu ila ni vyema tujifunze namna ya kukabiliana hili genge kabla kwenda kwenye field battle kwenyewe ili tupunguze maadui na mizigo mizito tuliyoibeba hii itatusaidia kushinda vita hii kwa haraka mno!

Ni wako kijana mtiifu, mzalendo na mwanaharakati wa kweli Tanzania.
Tutoleee unafiki hapa, list ya mashujaa wako wamejaa makada wa chama tawala

Back
Top Bottom