AirTanzania
JF-Expert Member
- Mar 17, 2011
- 1,139
- 1,040
Heshima yako Maggid, Hili suala ni gumu sana kuna interest za watu wazito na linasemekana hili jambo lina mkono wa kifreemasons ndio maana babu anataka mia tano ile namba ina maana kubwa! Hili la dola moja nimelisikia hivi punde limenifanya nianze kuamini kuwa fremasons wanamkono ukiitazama ile dola moja utaona alama zao iangalie kwa makini kuna picha ya piramid juu yake kuna kama jicho! Usihadaike na kuumiza kichwa kuhusu maswala ya exchange rates kwani Mungu wa Isaya na Yakobo ni mwenye mapenzi na wanaadamu hawezi kuwapeleka sehemu inayowadhalilisha na kuishi maisha ya wanyama! Si tunasikia watu wanajisaidia porini na wanateseka kisawasawa kungoja "kikombe"? Upo wapi utu hapo? Kuna wengine humu JF wana miradi yao ya kubeba wanaoenda Loliondo kwa babu kwahiyo tegemea upinzani mkubwa wa hoja zako.
maggid,
hapa utatolewa macho, babu hapa jamvini siyo simple kama unavyofikiria. mbali na imani potofu, kudanganyika na ubishi/ignorance nk baadhi ya watu hapa wana maslahi ya kiuchumi kutokana na hii biashara ya kikombe,
usifikiri ni imani peke yake, wapo wanaotengeneza cash kila siku!
so watch out brother
you have been warned!
Ndugu Zangu,
JANA usiku muda mfupi kabla ya taarifa ya habari, TBC1, kulikuwa na mahojiano ya mwandishi wa TBC na Babu wa Loliondo.
Kati ya aliyoyaongea, Babu anasema, kuwa Mungu ndiye aliyepanga bei ya tiba ya kikombe iwe shilingi mia tano. Kuwa alimwonyesha mia tano! Na Mungu akamwambia wageni walipe dola moja!
Tafsiri yangu;
Pamoja na kuwa mwandishi hakumuuliza Babu maswali magumu, bado Babu wa Loliondo hakunisogeza hata hatua moja kutoka kwenye msimamo wangu. Kuwa tiba ya Babu ni Abrakadabra.
Tujiulize swali moja tu; hivi Mungu huyo ni Mungu gani anayebagua waja wake. Kuwa wengine walipe mia tano na wengine dola moja?
Jamani, hivi Mungu huyu wa Babu wa Loliondo naye anafuatilia exchange rate kila siku? Itakuwaje basi, shilingi ikipanda au kushuka thamani dhidi ya dola ya Marekani? Babu itabidi aoteshwe haraka ndoto nyingine ili abadilishe bei ya kikombe!
Na kwenye taarifa ya habari iliyofuatia ikaripotiwa, kuwa Serikali imeshindwa kutoa tamko jana juu ya tiba ya Babu kwa vile Babu amesema kamati iliyoundwa iende kwanza Loliondo!
Mnajua tena mambo haya ya imani! Alitamka mwanakamati mmoja kwenye TBC1. Na leo imeandikwa kwenye gazeti moja, kuwa Serikali itatoa tamko leo juu ya tiba ya ' Babu'.
Naam. Tamko hili liharakishwe kutolewa kabla ' Babu' hajaoteshwa ndoto, kuwa ' Tamko Lisitishwe hadi itakapotamkwa tena!'. Na nani? Fikiri mwenyewe.
Si ilipata kusemwa, kuwa kila kukicha, kuna kioja kinazuka kutoka Afrika!
Maggid
Iringa,
Jumapili, Machi 27, 2011
Naona watanzania siku hizi mmeingiliwa na Mambo ya kusema Freemasonry, kitu kidogo Freemasons, fulani kanya -Freemasons, Mbwa kakojoa -Freemasons, mwizi kaiba- Freemasons, babu na kikombe chake -Freemasons, Shekhe Yahya atabiri Kikwete kuwa Fisadi- Freemasons, tanzania ni maskini-Freemasons. Kila kitu mmekiweka kwenye Freemasons. Am sick and tired of this Freemasons songs, its like ccm sing Amani na utulivu
Maggid anakataa kuwa babu kaoteshwa na Mungu kwa kuwa Biblia inasema "Naye Baba aliyenituma hunishuhudia. Ninyi hamjapata kamwe kusikia sauti yake, wala kuuona uso wake Yohana 5:37" Maggid anathibitisha kuwa Biblia inasema kuwa sisi pamoja na "babu" hatujapata kamwe kusikia sauti ya Mungu wala kuuona uso wake!Nadhani babu ana zaidi ya majini Maimuna Tafakari!
Maggid, itakuwa vizuri kwa waandishii wafatilie hali halisi ya mahospitali ili muweze kulinganisha na kabla maswala ya babu yalivyokuwa. Kuna habari za kuaminika kuwa KCMC imefurika watu wanaotoka kupata kikombe cha babu! Hospital za Arusha na Moshi yaani KCMC na Mount Meru kumekuwa na taarifa za kupokea maiti zilizokwisha kuharibika. Waandishi waisaidie jamii kujua hii hali wasitumie jina la babu kujipatia mia tano na wao kwa kuuza magazeti tu!
Sitak kuamin kwamba maggid uwezo wa kufikiri ni mdogo. BABU ameoteshwa mia tano kwa kuwa ni hela ya Kitanzania ambayo kila mtz anaiweza kuipata awe maskin au tajiri. na khs 1USD hiyo ni currency maarufu dunian kote na inajulikana kila mahali. Tatizo lako ulitaka BABU aoteshwe Currency za kutoka UARABUNI ndo ungerizika na kuamin kama hutak kuamin kaa kimya waache wenye iman wakatibiwe, SHEIKH YAHYA YUPO KUWATIBU WATU KAMA NINYI BABU HANA MAJIN MAIMUNA.
DAH!! U TOTALY POOR n LITTLE KNOWLEDGE IN TORTOLOGY POLE SANA BIBLIA HAISOMWI KWA ANDIKO MOJA MOJA KAMA UFANYAVYO WEWE NENDA KASOME WAKORINTHO UONE MUNGU ANAVYOONYESHA UKWELI WA NDOTO ZA MABABU SIKU ZA MWISHO.
Mtu mzima mwandishi wa habari anachallenge babu kuchagi mia tano na dola I . Hivi ww unataka aishi vipi na hao wanaofanyakazi nae wale mawe? Kwani si sera kuwa wageni walipie huduma in dollers.? Hata huko misikitini kwako mashehe huomba sadaka maana hawafanyi kazi nyingine. I hate such poor way of writting to publoc. Crazzy
Maggid,
Utakufa kwa wivu, husuda na kijiba cha roho. Ulianza na CHADEMA yakakushinda, umevagaa Babu pia...yatakushinda.
Mwaka huu lazima ujinyonge tu.
By the way kwa nini usiandike historia ya chama chetu kikkongwe na biograph ya mtabiri wetu mkuu na mtoa ulinzi usioonekana kwa kingozi wetu mkuu?
Ndugu Zangu,
Hata kama Watanzania wote watahamia kwa ' Babu' wa Loliondo, mimi nitabaki kijijini kwetu Nyeregete, alikozikwa babu yangu. Na itabaki kuwa hivyo, labda waje kunibeba na karandinga la jeshi.
Maggid,
Iringa.
na baaaaaaaaaaado hii inaonyesha ni jinsi gani watanzania tulivyokuwa watu wa kupelekwa pelekwa, yaani mpaka viongozi wetu wanonyesha ni jinsi gani walivyokuwa na upeo mdogo it means wanaweza kudanganywa muda wowote na kutuweka watanzania matatizoni, hivi je ikatokea yale maji yaje kuleta sumu kwenye miili yetu si inamaaana tutapoteza watanzania wengi ikiwemo viongozi wetu pia. jamani watanzania tuamke na tusikurupuke, tumemsahau mpaka MUNGU sasa tumamuangalia babu. heeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee siamini jamani
Ukimuona mtu na akili zake anaenda kwa babu kutafuta uzima, ujue kahangaika sana muda mrefu sasa hanabudi kuenda kujaribu ili apate uponyaji ambao kautafuta bilamafanikio kwa muda mrefu. Mtu kama maggid na wapambe wake, hawajapatwa na matatizo km ya hiv, kifua kikuu, saratani, na kisukari wakaonja adha yake.pemgine km wangeshapata wangetushuhudia kuwa wao japokuwa wanaumwa hawawezi kwenda ila wanasubiri kuendelea na mateso yao hadi wafe.... Pengine hapo wanganza nishawishi nami kwa hoja zao... Lakini kupayuka tu huku wengine wakipata taaaaaaabu kiafya haiingii akilini mwangu!!!