Imeniuma sana, vijana tuwaheshimu mama zetu

Daaaaah! haya mambo yapo.lkn inakuwaje umthamini mkeo kuliko mama yako huo ni ujinga sana na huwezi kufanikiwa kwa vyovyote vile utaharibikiwa tu.na ujinga ni pale unaporuhusu mwanamke akutawale huo ni ujinga wa mwisho
 
Imeniuma sana, huyo mama hana tofauti na aliezaa shoga.!
 
Inasikitisha sana,mkuu msaidie Jiran yako Kwa kumtafuta private uongee nae Kwa utaratibu umsaidie kugundua kosa lake kisha mshauri akamuombe msamaha mama yake kabla haijawa too late akajajuta maisha yake yote.Nakupenda sana mama...
 
Kuna umuhimu pia Wa kujua "mawazo ya mwenzako changanya na yako"

Kamwe Siwez kumshauri Mme wangu eti amtimue mzazi wake yeyote, awe mama au baba, kwangu Mimi ni Wa thamani kwa sababu wao ndo wamefanya niitwe Mrs.... Laiti Kama wasingemzaa Leo ingekuwa historia nyingnge.

NOTE: wamama/wadada wanawake wenzangu, tuwapende na kuwaheshimu wazazi Wa pande zote mbili, wawe wako au Wa mmeo. Tusibague. Maana bila wao msingelikuwa Leo Mr&Mrs......

Mapungufu kwa kila mwanadamu yapo lkn tujitahidi kuchukuliana kwani hakuna aliye mkamilifu hata kidogo.
umeongea point sana,kwakweli siwezi kumchukia mzaa chema no matter what,nitachukuliana nae tu,naomba Mungu anisaidie.
 
Ni miaka mitatu Sasa toka mama yangu atoweke dunian, R. I. P mama Makuku Rey.

Namkumbuka sana mama yangu, Sema tu huwez kuazma mama wa mtu mwingne, ingewezekana ningemny'ang'any'a mama huyo jiran yako asojua kuwa mama ni wa muhimu kuliko mke

Pole sana
 
nimesikitishwa sn na uzi huu. kiukweli huyo mwanaume hana msimamo ktk maisha yake. ndio maana anakubali ushauri wa kipumbavu kutoka kwa mkewe mwenye chuki navroho mbaya. hivi angekuwa mama yake angeshauri afukuzwe ? kweli hiki ni kizazi cha nyoka.
 
nakumbuka nilivokuwa mdogo nikiwa shule ya msingi..nikimkosea mama ananikanya na kuniambia MAMA YAKO NI MAMA YAKO HATA KAMA NI MJINGA. yalikuwa yananiuma sana maneno hayo
 
Dah

Huyo baba atatafuta alomroga asimpate.........


Hivi unaanzaje kumfukuza mama yako???

Na mwanamke anayethubutu kukushawishi umfukuze mama yako atakuja kumtenda mambo makubwa abaki kinywa wazi
 
Dozi ya limbwata toka kwa mkewe imemzidi nguvu hadi kamfukuza mama yake aliyemuhifadhi tumboni miezi Tisa akamzaa kwa uchungu pia akamkuza. Mungu amusamehe.
 
Ataionja joto ya jiwe akiwa na mke wake wanaona hivihivi siku si nyingi hakika machozi ya mzazi hayadondoki bure.
 
Ukweli hawa wanawake wanaoolewa miaka hii ni wavivu tena wana roho mbaya sana. Wengine hata chakula au maji ya kunywa wanafungia.

Huyo jamaa yako na mkewe ni barua wameandika kwa Mungu wangojee majibu yao.
 
Ninarudia kusema kisa cha ndugu yangu wa karibu alisomeshwa na wazazi wake. Baba yake alikuwa na ulemavu kidogo mguu mmoja. Ila alipigania elimu ya wanawe.

Akapata kazi tra ni afisa mkubwa. Akajenga nyumba nzuri pale kijijini.

Wazazi wake walikuwa na kanyumba kadogo wao wanakaa humu pamoja na mifugo yao.

Wakamwomba mtoto wao awaruhusu wakae kwenye jumba lake as ile yao inavuja. Jamaa akagoma.

Nafupisha.....
Baba akaugua akafa. Kilichofuatia ni ...... Kumkuta baba yake amekaa sebuleni huku alishakufa.

Nyumba haikaliki tena.

Be careful wakati mwingine.
 
Back
Top Bottom