Imeniuma sana, mke wangu anatembea na baba yake mdogo

Baada ya changamoto hii utakuwa umeiva katika nyanja ya mapenzi, tulia acha kumfikiria kama ndiye mwanamke pekee duniani hapo ni vigumu.Nina uhakika ndani ya muda mfupi atarudi analia ...usije kurogwa kumrudia ni sawa na mtu aliyeonja NYAMA ya MTU....Afadhali umejua haya sasa songa mbele maisha yanaendelea ni ya kawaida katika mapenzi ...Ila sasa mtafute Mungu akuonyeshe mke wako halisi
 
Ndugu Achana nae huyo...hata akikiri na mkarudiana , Tayari kaharibu historia itawatesa sana hamuwezi kua kama Zamani. Dawa ya Jeuri ni Kiburi
 
Nakushauri uachane na huyo mwanamke kwa maana alipofikia huwezi mrudisha, na ukiendelea mfatilia kwa kutaka kuishi naye unaweza ukawa na maisha mabaya kuliko matarajio yako.
Naomba utulize akili kama miezi 6, tafuta mwanamke mzuri anayejitambua oa kwa utaratibu, ni wakati wa wew kuwa karibu sana na Mungu kuliko kipindi chochote ili akuonyeshe kitu.
Yamenikuta Mimi ingawa sijasomesha lkn nimejipa likizo kwa muda na nahisikia amani sana.

Mwisho akirudi huyo mwanamke mchape hata makofi umfukuze hapo kwako mara nyingi walimu wa kike siku hizi ni wana tamaa sana hivyo wahuni sana.
Usisahau kumchukua mwanao pia umechelewa kumpa mimba ingine ndo maana anajiona binti.
Achana naye aoleww na baba ake

Mungu akutie nguvu
 
Wanajamvi nimekuja na simanzi kubwa sana moyoni. Sijawahi kuumia kiasi hiki, maelezo ni marefu lakini ngoja nifupishe ili nisiwachoshe.

In short nina mke wangu nmeishi nae kwa mwaka 1 kama mke na mume. Ingawa mazingira ya kikazi yametufanya tuwe mbali kidogo lakini nmekuwa najitahid kufika kwake mara kwa mara sababu sio mbali sana(sisi ni watu wa Kanda ya Ziwa ki-makazi lakini sio kwetu).

Tatizo limekuja kuna tetesi nilipewa na dada yake kuhusu mahusiano kati ya mke wangu na mzee mmoja mwenye umri wa miaka 46. Mbaya zaidi ni baba yake mdogo na mke wangu ingawa walikwishatalakina na mkewe ambaye ni mama mdogo wa mke wangu kitambo kidogo kimepita.

Chanzo cha wao kukutana ilikua mke wangu ali carry somo moja apo UDSM ikabidi arudi kufanya hio course basi huyo mzee akamchukua aende nyumbani kwake amuangalizie wanae huku akienda chuo basi mchezo ukaanzia apo mzee kamrubuni mke wangu kuanza kutoka nae.

Kama mwanzo nilivoeleza, dada wa mke wangu aliniambia hicho kitu ila nikapuuzia sababu huwa na tabia ya uchonganishi pia huwa mahusiano yetu sio mazuri.

Nilichoamua nikafanya uchunguzi mwenyewe kwa njia zangu ninazozijua nikagundua ukweli. Mimi ni mtu wa IT basi nakaja kugundua hata baadhi ya vitu kama simu, camera, mavazi na pesa mke wangu analeta huwa vinatoka kwa huyo mzee maana nlikua napatwa shaka na spendings zake kulingana na kipato chake cha ualimu.

Basi tumeenda hivo lakini ndani kukawa na visa kikitoka hiki kinakuja kile ikafikia akaanza kuninyima sex anadai simfikishi wakati namjua vzuri na huwa namfkikisha, kwa hilo sina shaka hata tone.

Nikirudi nyuma kidogo mimi ndio nimemsomesha chuo tangu mwaka wa kwanza mpaka kamaliza na nimegharamika mambo mengi juu yake. Hapa tulipo tuna mtoto 1 wa kiume ana miaka 4 sasa.

Muda huu na andika post hii mke wangu yupo Dar, nimemuuilza yupo kwa nani hasemi. Nimeumia sana ikabidi niongeee na mama mkwe nikamueleza situation. Akampigia simu mwanae, kilichofuata akanitusi na kunitamkia maneno ambayo yamenichafua sana nafsi yangu.

Namnukuu "Unampigia simu mama akusaidie nini?, kama nato** si mimi wewe inakuhusu nini? Na nakuapia lazima nit**we huku ili utulie."

Imeniuma sana mpaka sasa moyo wangu umefunga siwez tena tena endelea nae ingawa nampenda na bila mimi asingekua hapo alipo leo" Nimejizuia sana kulipa kisasi nimeshindwa ukizingatia familia yao nimeibeba sana kwa mambo mengi.

Nikumbushe kitu, ukwel ni kwamba nilikuwa sijatoa mahari mpaka sasa ingawa tuliishi nae kama mke na mume. Lakini mpango ulikua mwezi huu na nilikua nimekwisha andaa kila kitu. Hata nashindwa nianze vipi kuwaeleza wazee.Nina mengi nimeyaruka kuyaeleza maana mimi si mwandishi mzuri. Natamani ningemsimulia mtu aandike.

Naomba ushauri wenu wadau na maswali pia kama yapo ila kama nitapata mtu wa kunipa njia nzuri ya kisasi nitafurahi.

Asanteni
Hamia kwa mdogo wake maana ni informer mzuri. Pia tenda wema nenda zako mkuu
 
Niongeze kitu hapo mimi nime lelewa na mama wa kambo baada ya mama yangu kufariki, maisha nliyo yapitia sikupenda mwanangu aishi tena nliteseka Sana
Pole sana, lkn usiwe mtumwa kwa mwanamke, utakufa kwa pressure za mwanamke

Utavunja record ya kuteseka ukiwa mtoto na ukiwa mtu mzm unajitambua.
Kama mwanao atateseka mpeleke kwa bibi au kwa mama yake utamhudumia akiwa huko lkn Eti uoe kwa sababu ya mtoto!!! Kuna mambo muhimu utahitaji kuyafanya zaidi ya ya huyo mtoto yumkini hata kumsaidia mtoto mwenyew lkn mkeo atakusumbua.jipange na ujipime

Achana naye nakushauri unless ukuwa na haja ya kuomba ushauri
 
Unafaa kutunga riwaya ila unakosea kama bongo movies umesema mna mwaka mmoja halafu mna mtoto wa miaka minne mhn haya bhana
 
mkuu hebu jaribu kuicheki hii movie TEMPTATION CONFESSIONS OF A MARRIAGE COUNSELOR,ya 2013..imechezwa na jurnee smollet-bell,lance gross,kim kardashian,vanessa williams,robbie jones,renee taylor,ella joys,brandy norwood,and many more,nahisi itakusaidia sana kujua nini cha kuamua juu ya hilo zito unalopitia,naona tatizo limeshabihiana sana na scenerio nzima ya hii movie,kama mshabiki wa movie naamini hii itakupa suluhisho,itafute mkuu!
 
Wanajamvi nimekuja na simanzi kubwa sana moyoni. Sijawahi kuumia kiasi hiki, maelezo ni marefu lakini ngoja nifupishe ili nisiwachoshe.

In short nina mke wangu nmeishi nae kwa mwaka 1 kama mke na mume.

Hapa tulipo tuna mtoto 1 wa kiume ana miaka 4

Asanteni

Okay bye
 
Pole, ni part ya life yako nw. Ni ww utakayeamua nn ufanye. That's satanic work tu, just relax tu kama wiki hivi. Fanya kama hujaumizwa na matusi yake, omba kwa ajil yake. Send her gud SMSs every night.
Tafuta sehemu nzuri tulivu, ili kupumzika kutokana na stress ulizonazo nw. I'm sure baada ya muda atajutia makosa yake, be ready kumusamehe..
Wrong advise. ...it doesn't work like that ..love ikishafifia kwa hamna hii ni vyema ukatulia na hakikisha humrudii na wala hulipi kisasi cha aina yoyote just be good kwa wote hususani waliokutenda na hakikisha huwaonyeshi kuumia kwako hata chembe japo kimoyomoyo unajua ni maumivu makubwa sana umeyapata, ukiweza hili hakika wao wataumia mara dufu kuliko wewe..then jipe muda kataa kuibeba familia yake kama mwanzo ..anza mchakato wa kumpata mwenzi mpya hii dunia ina watu zaidi ya Bilioni ni wewe tu kuchagua unataka wa sampuli gani ..have a great day Mr.IT man.
 
Angalizo:Siku yoyote duniani mwanamke akikwambia umfikishi baada ya kua nae katika mahusiano ujue kaliwa/kaonja mahali pengine akapata ladha tofauti ndo na maana anafanya comparison, kama huyu wa ndugu yetu kaliwa sana mpaka kaizoea, yaani ndugu mkapa umfikishe lazima auwaze xxxx wa huyo mwingine, So sad kwa kweli..
 
kama unaamini mungu yupo,basi amini ipo siku haya mambo yatafika mwisho,usipende kufikiri mangapi umemfanyia,bali shukuru amekuzalia kamwana,usipende kutatua jambo ukiwa na hasira,kaa tuliza akili tafuta watu wazima watakupa hekima zaidi ya kutatua jambo hili kibusara zaid,na hapo ndipo atashangaa anakukomoa lkn wewe hukomoleki,
 
Pole sana Kaka,mimi sijaoa lakin kwa akili yangu na nnavojua kidini,kijamii hata kimila pia haruhusiwi kulipa kisasi,maana tayr una familia ya mtoto mmja hutakiwi kukua katika mazingira ya majuto kwa kukosa makes ya wazazi wawili calm down pls sikiliza ushauri wa watu lakini sio namna ya kulipa kisasi hawa ni viumbe dhaifu sana

DINI ZOTE ZINARUHUSU KISASI LABDA DINI YAKO KWA AJILI YAKO KURANI INASEMA HIVI: LIPIZIANENI KISASI ILI HESHIMA IWEPO MIONGONI MWENU MAANA MTU AKIKUPIGA NA WEWE UKAMPIGA ATAKUHESHIMU LAKINI UKIPIGWA UKATULIA ATAKUONA MNYONGE BADO ATAKUCHEZEA. BIBLIA YASEMA JINO KWA JINO KATIKA KITABU CHA TORATI SASA WEWE ANDIKO LA KUZUIA KISASI UMELIPATA WAPI HIVI UNAJUA UCHUNGU WA MKE KWELI WEWE MSHAURI TU KWA SABABU ZA KIBINADAMU ASILIPIZE KISASI LAKINI SIYO DINI ZIMEKATAA. KWENYE UKRISTO WAKO HUKOHUKO WALE WALIOMBAKA YULE DADA NINI KILIWAPATA BAADA YA KUTAHIRIWA NA WAYAHUDI MBONA WALIANGAMIZWA FAMILIA NZIMA KWA KOSA LA MTU MMOJA MUWE MNASOMA NA KUELEWA MSIPOTOSHE WATU.
 
Wanajamvi nimekuja na simanzi kubwa sana moyoni. Sijawahi kuumia kiasi hiki, maelezo ni marefu lakini ngoja nifupishe ili nisiwachoshe.

In short nina mke wangu nmeishi nae kwa mwaka 1 kama mke na mume. Ingawa mazingira ya kikazi yametufanya tuwe mbali kidogo lakini nmekuwa najitahid kufika kwake mara kwa mara sababu sio mbali sana(sisi ni watu wa Kanda ya Ziwa ki-makazi lakini sio kwetu).

Tatizo limekuja kuna tetesi nilipewa na dada yake kuhusu mahusiano kati ya mke wangu na mzee mmoja mwenye umri wa miaka 46. Mbaya zaidi ni baba yake mdogo na mke wangu ingawa walikwishatalakina na mkewe ambaye ni mama mdogo wa mke wangu kitambo kidogo kimepita.

Chanzo cha wao kukutana ilikua mke wangu ali carry somo moja apo UDSM ikabidi arudi kufanya hio course basi huyo mzee akamchukua aende nyumbani kwake amuangalizie wanae huku akienda chuo basi mchezo ukaanzia apo mzee kamrubuni mke wangu kuanza kutoka nae.

Kama mwanzo nilivoeleza, dada wa mke wangu aliniambia hicho kitu ila nikapuuzia sababu huwa na tabia ya uchonganishi pia huwa mahusiano yetu sio mazuri.

Nilichoamua nikafanya uchunguzi mwenyewe kwa njia zangu ninazozijua nikagundua ukweli. Mimi ni mtu wa IT basi nakaja kugundua hata baadhi ya vitu kama simu, camera, mavazi na pesa mke wangu analeta huwa vinatoka kwa huyo mzee maana nlikua napatwa shaka na spendings zake kulingana na kipato chake cha ualimu.

Basi tumeenda hivo lakini ndani kukawa na visa kikitoka hiki kinakuja kile ikafikia akaanza kuninyima sex anadai simfikishi wakati namjua vzuri na huwa namfkikisha, kwa hilo sina shaka hata tone.

Nikirudi nyuma kidogo mimi ndio nimemsomesha chuo tangu mwaka wa kwanza mpaka kamaliza na nimegharamika mambo mengi juu yake. Hapa tulipo tuna mtoto 1 wa kiume ana miaka 4 sasa.

Muda huu na andika post hii mke wangu yupo Dar, nimemuuilza yupo kwa nani hasemi. Nimeumia sana ikabidi niongeee na mama mkwe nikamueleza situation. Akampigia simu mwanae, kilichofuata akanitusi na kunitamkia maneno ambayo yamenichafua sana nafsi yangu.

Namnukuu "Unampigia simu mama akusaidie nini?, kama nato** si mimi wewe inakuhusu nini? Na nakuapia lazima nit**we huku ili utulie."

Imeniuma sana mpaka sasa moyo wangu umefunga siwez tena tena endelea nae ingawa nampenda na bila mimi asingekua hapo alipo leo" Nimejizuia sana kulipa kisasi nimeshindwa ukizingatia familia yao nimeibeba sana kwa mambo mengi.

Nikumbushe kitu, ukwel ni kwamba nilikuwa sijatoa mahari mpaka sasa ingawa tuliishi nae kama mke na mume. Lakini mpango ulikua mwezi huu na nilikua nimekwisha andaa kila kitu. Hata nashindwa nianze vipi kuwaeleza wazee.Nina mengi nimeyaruka kuyaeleza maana mimi si mwandishi mzuri. Natamani ningemsimulia mtu aandike.

Naomba ushauri wenu wadau na maswali pia kama yapo ila kama nitapata mtu wa kunipa njia nzuri ya kisasi nitafurahi.

Asanteni

POLE SANA KWA YALIYOKUFIKA MIMI NI MWATHIRIKA KAMA WEWE ILA WEWE UNA BAHATI HUJAFUNGA NDOA NAYE MWACHE KABISA KWANI KAMA KAFIKIA MAHALI PA KUKUTAMKIA ANAFANYWA BASI HUNA NAFASI KATIKA MOYO WAKE TENA NATAKA UFAHAMU MAMA NA BINTI YAKE KWA ASILIMIA 98% HUWA ANAKUBALIANA NA MWANAYE NA ANAMUUNGA MKONO USISHANGAE SIKU MOJA MAMA MKWE WAKO ATAKAPOKUTOLEA UVIVU NA KUKUPA MAKAVU. KOSA ULILOFANYA NI KUMSOMESHA MWANAMKE USIMSOMESHE KWA AHADI MTAOANA KULE ALIKO NDIKO ALIKO MPENZI WAKE AU MUME WAKE WEWE NI BOYA TU NA NDIYO MAANA KAPATA UJASIRI WA KUKUPA MAKAVU. NA UKIMG'ANG'ANIA SANA ATAKUUWA MAANA KULE ALIKO PENZI LIMEKOLEA NA WEWE UNAONEKANA KIKWAZO JIANDAE. KUHUSU KISASI HILI SIYO ENEO LA KUFUNDISHANA UHALIFU KISASI UTALIPA KUTOKANA NA MAUMIVU ULIYO NAYO NA USIFUNDISHWE NA MTU MWINGINE NJE YA NAFSI YAKO. KUMBUKA NI VEMA NA HAKI KUVUNJA UCHUMBA KULKO KUVUNJA NDOA HAKUNA DINI INAYOZUIA KISASI SOMA BIBLE NA KURANI UTAPATA MAJIBU.
'' TPX JIHADHALI TPX NAFUTIKA '' BADO MMOJA
 
naumia sana hasa nikiwaza mwanangu
HUO NI UDHAIFU WA KUTAKA KUMRUDIA KWA KIGEZO CHA MTOTO, HIVI KAMA AKIFA SASA HIVI MTOTO HATAISHI?? KAMA WEWE UNARIDHIKA ENDELEA KUSHEA NA MUME MWENZIO NA UWE MPOLE USIPOST VITU HAPA WAKATI MAJIBU UNAYO.
 
Una uhakika huyo ni mtoto wako? Mwanamke anatembea na baba yake mdogo? You can't be serious bro. Kaa nae mbali make mnatengeneza kizazi cha laana.
 
Back
Top Bottom