Imekuwaje Mkataba wa Amani kati ya Congo na Rwanda, Tanzania tumewekwa kando?

bikira latifah

JF-Expert Member
Joined
Oct 27, 2016
Posts
793
Reaction score
2,516
Nimefuatilia leo mkutano wa kuweka saini amani kati ya Rwanda na Congo naona Trump kawaalika kenya,Burundi,Uganda kama mashahidi Tz imerukwa

Ikumbukwe kuwa Tz ndio ilikuwa mstari wa mbele kupigania amani ya congo tumepoteza masolja wengi sana kule zaidi ya kenya saaasa mbona Tz skuizi tunawekwa kando tena nlitegemea samuya angekuwepo white house leo

Pia naambiwa makamu wa Raisi wa uganda alikuwepo Tz imewekwa kando je kuna nini?
 
hawawezi kuwaalika vichaa ..raisi wa mchongo anaropoka pumba hovyoo kama mwendawazimu , nani amualike?
 
Sasa mkuu angepewa nafasi huyu mama angeongea nini pale kuhusu upatanisho? Vitu kama hivi si vya kuandaliwa speech bali unaongea yanayotoka kwenye fikra zako direct huku dunia ikishuhudia. Sasa ulitaka hayo mataifa yakachambwe kwa kushikiwa kiuno na kidole juu huku kwenye taifa lake hali inayoelekea ni huko huko ilipokuwa Congo?šŸ¤£šŸ™Œ
 
Hii ni win for Tanzanians too, Congo wanahitaji bidhaa nyingi sana na bandari ya Dar kulisha watu wake, mahindi na mazao mikoa ya kusini ni fursa, lakini kwa hii serikali corrupt isiyojali maslahi ya watu wake sioni matumaini yeyote, at least majirani wataacha kuuana for nonsense
 

Nchi imepoteza hadhi yake na muelekeo wa maendeleo. Inatia simanzi kwani Tanzania ilikuwwa nchi ya kupigiwa mfano lakini leo inakalibia kufanana na nchi kama Somalia! Nchi imekosa wazee wenye hekima ambao wangeweza kusaidia kuwapatanisha makundi mbali mbali ya jamii yenye mitazamo kinzani kisiasa.Hapa ndipo wananchi wanamkumbuka marehemu Mwalimu Nyerere na busara zake.
 
Jamini kulikoni Tanzania kisiwa cha amani na nchi jirani kwa Rwanda na Burundi, na DRC haikutuma mwakilishi katika kusaini makubaliano kati ya Rwanda na DRC. Je, hii inaonesha kuwa tanzania ni failed state
 
Kweli sisi ni laana.
Lakini kama una so called Rais anajibu partners , tena Development partners kuwa WHO ARE YOU kweli hapo kuna kitu! Kuna Rais hapo? Kuna mtu hapo?
Kuna serikali hapo?

Ona sasa Kiranja Mkuu USA amemtolea nje kumshirikisha kama shahidi wa makubaliano hayo. Kumbuka Tanzania ndiye alikuwa Baba wa kusimamia Amani Africa.

Nadhani kama kuna kosa alilifanya Mungu ni kuwaumba weusi (anyway kama kweli yupo).
 
Yaani kurudisha heshima yetu ni kuiondoa tu CCM. Bila hivyo tutaweka kundi moja na Somalia
 
Wala hakuna haja ya Tanzania kualikwa sababu, vita ni kati ya Rwanda na Congo, hata Uganda hakualikwa japo ana majeshi ya ndani ya Congo, na M23 kinara wa vita pia hakualikwa
Kaeni kwa kutulia....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…