zegamba180
JF-Expert Member
- Oct 8, 2014
- 818
- 536
Mwanamke unapoudhiwa na tabia za mumeo, ongea na mumeo kwa upendo. Andaa mazingira rafiki ya maongezi. Wanawake huwa mnakosea sana kutojua muda na mahari pa kuongelea kero zenu.
Kwa kukosea huko daima ntaendelea kulalamika wanaume zenu wanawadharau.Mwache mumeo apumzike, awe ametulia. Omba kuongea nae. Akikataa mwache hadi wakati ujao, ila akikubali ongea.
"Asante mume wangu mpenzi, kwa kunijali mkeo ukakubali kunisikiliza mume wangu unaponitukana mbele ya watoto wakati mwingine bila kosa, Najisikia vibaya mume wangu. Kwasababu unanidhalilisha mkeo na kuwaathiri watoto kisaikolojia pia.
Mimi kama binadamu wa kawaida naumizwa sana matusi yako mume wangu. Nakuomba mume wangu uniite chumbani uniulize ama unieleze nilipokosea, ehee mume wangu mpenzi. Napendekeza kama kuna tatizo ama nakukwaza tujadiliane mume wangu."
Zungumza taratibu yamuingie huku umekaa nae karibu.
Daima tuimarishe ndoa zetu.