Imani ya mama inanitatiza

Imani ya mama inanitatiza

Chokochoko

JF-Expert Member
Joined
Oct 15, 2011
Posts
438
Reaction score
184
Wakubwa heshima zenu na wadogo hi,

Kuna jambo limeniumiza moyowangu sana naamini humu nitapata mtazamo mwema na wenye hekima.

Nimelelewa kwenye familia ya kikristo ila siongelei dini ni yeyote mwenye hekima anaweza toa maoni yake, Nina imani sana kuwa Mungu ni muweza wa mambo yote yooote yanayotukabili, huwa napenda kuachilia kila kitu kwa Mungu na familia yangu ndioilivyo miles hivyo,

Sasa mkasa ndio huu hapa, mwaka Jana sitsusahau baba yangu alipata ajali mbaya sana nusura tungemkosa ila kwabahati nzuri hakufa ila aliumia sana tulimuuguza mwaka mzima.

Niliomba sana Mungu amponye nakushirikiana na familia yangu tulikuwa tunaomba kwabidi nakuwashirikisha watumishi wa Mungu wamuombee na kwa uweza wa Mungu akaja kupona sasahivi yupovizuri kabisa ni jambo kubwa kwetu na lakushangaza lakimiujiza kwahali aliyokuanayo.

Sasa hivi majuzi nikawa naongea na mama kwanjia yasimu tuu maana wao wako mkoa, nikamuulizia baba anavyoendelea nanini chaajabu ni statement aliyonijibu eti ingekua kama siyo yeye kwenda kwa mganga wa kienyeji kwabidii baba tungemkosa, yaaani daah sikuamini hayo maneno Kama yangeweza kumtoka yeye any way nikapuuza tuu.

Imepita Kama miezi 6 hivi mdogo wangu alipata matatizo akarudi nyumbani japo kimaisha hajakaa vizuri ni mtu wakuyumbayumba sana ila navyojua nikutokana na life style yake ndio inayomfanya asisimame kimaisha.

Sasa niliongea na watumishi wa Mungu wawe wanamuombea hadi juzi hapa mtumishi mmoja akanieleza kuwa huyu dogo amefungwa na watufulani, anyway nikaongea na mama kwakusudi la kumsaidia kimaombi zaidi cha ajabu sasa statement aliyoijibu mama.

maombi yatachelewa nitaongea na mganga atamsaidia upesi nimeishiwa nguvu moyo wangu umeniuma kuona nyakati kama hizi mama ndio keshatekwa naimani za kishirikina kiasi hiki.

Naombeni msaada wenu wa mawazo nifanyeje mama mzazi akishatekwa hivyo.
 
Kazi unayo ya kubomoa madhabahu ya kichawi na ushirikina kwenye familia yenu.
 
A
mwombee tu namuheshimu mama yako
Amebonyezewa kwenye kona mbaya Shetani bana, imeandikwa hamkosi kuzijua bila zake , sasa huyo ni mama yako mzazi neno la Mungu linasema amlaumue babaye au mamaye taa yake itazimwa, usithibutu kumlaamu wewe ingia rohoni piga Miungu anayoitumainia yote isambaratishe, abakie mkavu
 
A

Amebonyezewa kwenye kona mbaya Shetani bana, imeandikwa hamkosi kuzijua bila zake , sasa huyo ni mama yako mzazi neno la Mungu linasema amlaumue babaye au mamaye taa yake itazimwa, usithibutu kumlaamu wewe ingia rohoni piga Miungu anayoitumainia yote isambaratishe, abakie mkavu
amina mtumishi..
 
Mkumbushe mama yako kuwa Shetani hawezi kumtoa Shetani mwenzake. Kinachofanyika kwa waganga wa kienyeji na washirikina ni kuongeza Pepo juu ya lile lililoko ndani yako ili lilitulize lile ulilonalo. Ndio maana utapewa masharti kadhaa ambayo ukiyakiuka utakuwa na hali mbaya zaidi.
 
Msaada hapo ni kumuombea huyo mama kwa bidii zote ili aachene na hizo imani za kishirikina na kumgeukia Mungu.
 
KWELI NA HAKIKA Mganga wa kienyeji hana msaada wowote kwa binadamu.

Angekuwa na uwezo angejiganga kwanza na kujinufaisha kimakazi na kiuchumi.

Mwambie mama aachane na imani ya waganga wa kienyeji kwani watamconnect na mambo yatakayomgharimu maisha yake yote na hata ya vizazi vyake.
 
Ni kumweka tu kwenye maombi, maana yeye anaamini mganga kuliko Mungu ila mkiendelea kumuelimisha atajua kuwa Mungu ni mkuu kuliko mganga
 
pole sana halafu hajaanza siku hizi huyoo

kaanza mda mrefu anavyoonesha
 
Back
Top Bottom