Bado unanishambulia mimi badala ya kujibu hoja.
That is ad hominem logical fallacy.
Jibu maswali.
Kwa nini ukubali hayo maneno ni ya ukweli na si hadithi za watu tu?
Hicho kitabu kina uongo mwingi sana, ambao tunaweza kuonesha huu ni uongo, kimantiki.
Sasa kwa nini tukubali hayo maneno ni ukweli, na si hadithi za uongo za kutungwa na watu tu?
Umeshasema kitabu cha uongo, hiyo itabaki kwako na wewe ukiwa unaamini uongo vilevile, na biblia imesema wazi kuhusu watu kama ninyi 👇
Zaburi 14:1
"Mpumbavu amesema moyoni, Hakuna Mungu..."
Kwa hiyo huwezi kunipa shida kwa sababu
Biblia inasema kutokukubali Mungu yupo ni upumbavu, ikiashiria kuwa kuwepo kwake ni jambo lililo wazi kama nilivyofafanua hapo awali.
Na kinachonifanya mimi niamini Mungu yupo ni neno lake, imani yangu inatokana na neno la Mungu.
Waebrania 11:6
"Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza, kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye upo, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao kwa bidi."
Hapa imani inaamini Mungu yupo, na namwendea kila wakati kumwona, uwepo wake ni dhahiri kwetu.
Kutokuamini kwako haiwezi kuondoa ukweli wowote kuwa Mungu yupo.