Yer 10:10 SUV
[10] Bali BWANA ndiye Mungu wa kweli; Ndiye Mungu aliye hai, Mfalme wa milele; Mbele za ghadhabu yake nchi yatetemeka, Wala mataifa hawawezi kustahimili hasira yake.
Imani zipo nyingi, kila mmoja anaweza akawa na mtazamo wake na uelewa wake kuhusu Mungu au miungu, wapo wanachanganya miungu mingine na Mungu, kwa kuamini wote tunabudu Mungu mmoja.
Wengine tunatamka vinywani Mungu mmoja, ila tukija kwenye ukweli tunagundua hatuna Mungu mmoja, wapo wana miungu mingine ila wanajidanganya ni Mungu mmoja.
Katika andiko hili, tunaona tamko hili la kipekee la kibiblia ambalo ni la kimonotheism, monotheism ni imani ya Mungu mmoja wa kweli.
Watu wanaoamini Mungu wa kweli katika Yesu Kristo, hao wanaweza kusema Mungu wao ni mmoja na wa kweli, nje na hapo sio Mungu wa kweli, na hamuwezi kuwa kitu kimoja katika imani na mtu asiyemwamini BWANA Yesu.
Moja ya mapingamizi na makatazo ya msingi aliyoyaweka Mungu wetu ni ibada ya sanamu, hapa ameonyesha vile miungu ya mataifa mengine ni ya uongo, sio hivyo tu haina uhai.
Mungu anajiweka bayana kuwa Yeye ni wa kweli na ana uhai, na sio sanamu sizizo na roho wala uhai wowote ndani yake, na haziwezi kusema chochote.
Unaweza kujiuliza Mungu wa kweli ni yupi? Mungu wa kweli ni yule aliyeumba mbingu na nchi ambapo tupo sasa, anayejifunua wazi kwa watu wake, ambaye ndani yake hakuna udanganyifu au uongo wowote.
Mwanzo 1:1
Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi.
Tumewahi kuona au tunaona sanamu hazina uhai, hazina uwezo wa kuzungumza, hazitembei, na haziwezi kutenda jambo la maana.
Tofauti na Mungu wa Israeli, Yeye ni hai, anaongea, anatenda wazi wazi, anahukumu kwa haki, muumbaji wa vinavyoonekana na visivyoonekana, na anaweza kuingilia historia ya mtu na kuibadilisha kabisa.
Jambo ambalo miungu haina sifa hiyo, hata kama kuna watu wanaamini miungu yenye uhai, bado haina uwezo wa kuwa na sifa kama ya Mungu wa kweli, maana mwenye kutoa uhai ni Mungu wa kweli tu. Sifa yake kuu yupo kila mahali kwa wakati mmoja, ni wa milele, na anahukumu kwa haki, sifa ambayo hata Shetani hana.
Mungu huyu wa kweli sio wa Israeli tu, huyu ni Mungu wa mataifa yote au ulimwengu mzima, mataifa yote yana haki sawa ya kuwajibika kwa Mungu wao, hakuna upendeleo wala ubaguzi katika hili.
Kila mwamini au kila mmoja wetu anapaswa kumtazama Mungu kwa jicho lingine, hofu ya kiungu inapaswa kuwa ndani ya kila mwamini, toba ya kweli inapaswa kuwa sehemu ya maisha ya mwamini, na ibada ya kweli na safi inapaswa kuwa ndani ya mwamini.
Soma neno ukue kiroho
Liwe jua iwe mvua soma biblia na kutafakari
Mungu akubariki sana
Samson Ernest
Je, Yesu alisema kwamba lazima uwe Mkristo la sivyo utaenda motoni?
Hapana kabisa.
Yesu aliahidi na kuthibitisha Pepo kwa wale wasiokuwa na imani ya Utatu.
Hakuna hata aya moja katika Agano Jipya ambapo Yesu aliahidi moto wa jehanamu kwa wale wasiokuwa Wakristo. “Na wanasema: ‘Hatutaingia peponi ila tukuwe Wajusi au Wakristo.’ Hizo ni tamaa zao tu. Sema: ‘Lete ushahidi wenu ikiwa mnasema kweli.’ (Qur’an Tukufu 2:111).
Neno “Mkristo” si neno halali, kwa kuwa hakuna dini iitwayo Ukristo kwa mujibu wa Uislamu.
Kwa mujibu wa Uislamu, Yesu alikuja na kuhubiri Injili. Wafuasi wa Yesu hawakuitwa Wakristo. Dini zote za Mwenyezi Mungu zilifundisha juu ya Umoja wa Mungu Mmoja, jambo ambalo kwa Kiarabu linamaanisha “Uislamu.”
Yesu alihangaika zaidi kufundisha maadili mema na tabia njema kwa wafuasi wake.
Hebu tuangalie baadhi ya maneno ya Yesu katika Agano Jipya:
Matendo ya Mitume 20:34-36 – “Katika kila kitu nilichofanya, niliwaonyesha kwamba kwa kufanya kazi kwa bidii namna hii tunapaswa kuwasaidia wanyonge, tukikumbuka maneno ya Bwana Yesu mwenyewe aliyosema: ‘Ni heri kutoa kuliko kupokea.’”
Mathayo 5:9-11 – “Heri walioonewa kwa ajili ya haki, kwa maana Ufalme wa mbinguni ni wao.”
Mathayo 5:8-10 – “Heri wapatanishi, kwa maana wataitwa wana wa Mungu.”
Mathayo 5:5-7 – “Heri wenye njaa na kiu ya haki, kwa maana watashibishwa.”
Mathayo 5:6-8 – “Heri wenye rehema, kwa maana wao watapewa rehema.”
Mathayo 5:7-9 – “Heri wenye moyo safi, kwa maana wao watamwona Mungu.”
Mathayo 5:3-5 – “Heri wanaoomboleza, kwa maana watafarijiwa.”
Mathayo 5:4-6 – “Heri wapole, kwa maana watairithi dunia.”
Marko 12:29 – “Sikieni Israeli: Bwana Mungu wetu ni Bwana mmoja.” (Angalia hoja dhidi ya Utatu).
Katika maneno haya ya Nabii wetu mpenzi Yesu – rehema na amani ziwe juu yake – tunaona wazi kwamba alihangaika zaidi juu ya “haki.” Haingii akilini kwamba Mwenyezi Mungu awabariki watu na wakati huo huo awatupe motoni .
Yesu aliposema kwamba Mwenyezi Mungu atawabariki wale wanaofanya haki, alimaanisha kweli.
Hii ndiyo Injili ambayo sisi Waislamu tunaamini kwamba Yesu – rehema na amani ziwe juu yake – aliifundisha.
Kuamini katika Mungu Mmoja wa Kweli aliye hai, na kupendana kati ya wanadamu .
Hii ndiyo sababu Waislamu wanaamini kwamba maneno ya Yesu mwenyewe katika Biblia ndiyo ya karibu zaidi na ukweli .
Hakika wamekufuru walio sema: Mwenyezi Mungu ni Masihi mwana wa Maryamu! Na Masihi mwenyewe alisema: ‘Enyi Wana wa Israeli! Muabuduni Mwenyezi Mungu, Mola wangu na Mola wenu.’ Kwani anaye mshirikisha Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu ametamkalia Pepo, na mahala pake ni motoni. Na kwa walio dhulumu hawatakuwa na wa kuwasaidia.”
” (Qur’an Tukufu 5:72).