Imani Ya Kweli Ya Mungu Mmoja Wa Kweli

Imani Ya Kweli Ya Mungu Mmoja Wa Kweli

Samson Ernest

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2014
Posts
1,119
Reaction score
1,569
Yer 10:10 SUV
[10] Bali BWANA ndiye Mungu wa kweli; Ndiye Mungu aliye hai, Mfalme wa milele; Mbele za ghadhabu yake nchi yatetemeka, Wala mataifa hawawezi kustahimili hasira yake.

Imani zipo nyingi, kila mmoja anaweza akawa na mtazamo wake na uelewa wake kuhusu Mungu au miungu, wapo wanachanganya miungu mingine na Mungu, kwa kuamini wote tunabudu Mungu mmoja.

Wengine tunatamka vinywani Mungu mmoja, ila tukija kwenye ukweli tunagundua hatuna Mungu mmoja, wapo wana miungu mingine ila wanajidanganya ni Mungu mmoja.

Katika andiko hili, tunaona tamko hili la kipekee la kibiblia ambalo ni la kimonotheism, monotheism ni imani ya Mungu mmoja wa kweli.

Watu wanaoamini Mungu wa kweli katika Yesu Kristo, hao wanaweza kusema Mungu wao ni mmoja na wa kweli, nje na hapo sio Mungu wa kweli, na hamuwezi kuwa kitu kimoja katika imani na mtu asiyemwamini BWANA Yesu.

Moja ya mapingamizi na makatazo ya msingi aliyoyaweka Mungu wetu ni ibada ya sanamu, hapa ameonyesha vile miungu ya mataifa mengine ni ya uongo, sio hivyo tu haina uhai.

Mungu anajiweka bayana kuwa Yeye ni wa kweli na ana uhai, na sio sanamu sizizo na roho wala uhai wowote ndani yake, na haziwezi kusema chochote.

Unaweza kujiuliza Mungu wa kweli ni yupi? Mungu wa kweli ni yule aliyeumba mbingu na nchi ambapo tupo sasa, anayejifunua wazi kwa watu wake, ambaye ndani yake hakuna udanganyifu au uongo wowote.

Mwanzo 1:1
Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi.

Tumewahi kuona au tunaona sanamu hazina uhai, hazina uwezo wa kuzungumza, hazitembei, na haziwezi kutenda jambo la maana.

Tofauti na Mungu wa Israeli, Yeye ni hai, anaongea, anatenda wazi wazi, anahukumu kwa haki, muumbaji wa vinavyoonekana na visivyoonekana, na anaweza kuingilia historia ya mtu na kuibadilisha kabisa.

Jambo ambalo miungu haina sifa hiyo, hata kama kuna watu wanaamini miungu yenye uhai, bado haina uwezo wa kuwa na sifa kama ya Mungu wa kweli, maana mwenye kutoa uhai ni Mungu wa kweli tu. Sifa yake kuu yupo kila mahali kwa wakati mmoja, ni wa milele, na anahukumu kwa haki, sifa ambayo hata Shetani hana.

Mungu huyu wa kweli sio wa Israeli tu, huyu ni Mungu wa mataifa yote au ulimwengu mzima, mataifa yote yana haki sawa ya kuwajibika kwa Mungu wao, hakuna upendeleo wala ubaguzi katika hili.

Kila mwamini au kila mmoja wetu anapaswa kumtazama Mungu kwa jicho lingine, hofu ya kiungu inapaswa kuwa ndani ya kila mwamini, toba ya kweli inapaswa kuwa sehemu ya maisha ya mwamini, na ibada ya kweli na safi inapaswa kuwa ndani ya mwamini.

Soma neno ukue kiroho
Liwe jua iwe mvua soma biblia na kutafakari
Mungu akubariki sana
Samson Ernest
 
The Real Source ni mmoja,wote na vyote tumetoka kwake na tumerejea kwake.

Warumi 11:36
Kwa kuwa vitu vyote vyatoka kwake, viko kwa uweza wake, tena vinarejea kwake. Utukufu una yeye umilele.

Kolosai 1:17
Naye amekuwako kabla ya vitu vyote, na vitu vyote hushikana katika yeye.
 
Attachments

  • IMG_4876.jpeg
    IMG_4876.jpeg
    220.2 KB · Views: 16
  • IMG_4877.jpeg
    IMG_4877.jpeg
    291.4 KB · Views: 16
  • IMG_4878.jpeg
    IMG_4878.jpeg
    300 KB · Views: 16
  • IMG_4879.jpeg
    IMG_4879.jpeg
    274.1 KB · Views: 13
  • IMG_4880.jpeg
    IMG_4880.jpeg
    313.2 KB · Views: 16
  • IMG_4881.jpeg
    IMG_4881.jpeg
    225.2 KB · Views: 21
The Real Source ni mmoja,wote na vyote tumetoka kwake na tumerejea kwake.

Warumi 11:36
Kwa kuwa vitu vyote vyatoka kwake, viko kwa uweza wake, tena vinarejea kwake. Utukufu una yeye umilele.

Kolosai 1:17
Naye amekuwako kabla ya vitu vyote, na vitu vyote hushikana katika yeye.
Ubarikiwe sana 🙏
 
Muumba wetu ambaye ndio Chanzo Halisi anaishi ndani yetu sote na sio huko angani kama wengi hudhania,hata Yesu alifundisha ombeni ufalme uje,rejea sala ya baba yetu.

Warumi 3:11
Kila kitu amekifanya kizuri kwa wakati wake; tena ameiweka hiyo milele ndani ya mioyo yao; ila kwa jinsi mwanadamu asivyoweza kuivumbua kazi ya Mungu anayoifanya, tangu mwanzo hata mwisho.
 
Yer 10:10 SUV
[10] Bali BWANA ndiye Mungu wa kweli; Ndiye Mungu aliye hai, Mfalme wa milele; Mbele za ghadhabu yake nchi yatetemeka, Wala mataifa hawawezi kustahimili hasira yake.

Imani zipo nyingi, kila mmoja anaweza akawa na mtazamo wake na uelewa wake kuhusu Mungu au miungu, wapo wanachanganya miungu mingine na Mungu, kwa kuamini wote tunabudu Mungu mmoja.

Wengine tunatamka vinywani Mungu mmoja, ila tukija kwenye ukweli tunagundua hatuna Mungu mmoja, wapo wana miungu mingine ila wanajidanganya ni Mungu mmoja.

Katika andiko hili, tunaona tamko hili la kipekee la kibiblia ambalo ni la kimonotheism, monotheism ni imani ya Mungu mmoja wa kweli.

Watu wanaoamini Mungu wa kweli katika Yesu Kristo, hao wanaweza kusema Mungu wao ni mmoja na wa kweli, nje na hapo sio Mungu wa kweli, na hamuwezi kuwa kitu kimoja katika imani na mtu asiyemwamini BWANA Yesu.

Moja ya mapingamizi na makatazo ya msingi aliyoyaweka Mungu wetu ni ibada ya sanamu, hapa ameonyesha vile miungu ya mataifa mengine ni ya uongo, sio hivyo tu haina uhai.

Mungu anajiweka bayana kuwa Yeye ni wa kweli na ana uhai, na sio sanamu sizizo na roho wala uhai wowote ndani yake, na haziwezi kusema chochote.

Unaweza kujiuliza Mungu wa kweli ni yupi? Mungu wa kweli ni yule aliyeumba mbingu na nchi ambapo tupo sasa, anayejifunua wazi kwa watu wake, ambaye ndani yake hakuna udanganyifu au uongo wowote.

Mwanzo 1:1
Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi.

Tumewahi kuona au tunaona sanamu hazina uhai, hazina uwezo wa kuzungumza, hazitembei, na haziwezi kutenda jambo la maana.

Tofauti na Mungu wa Israeli, Yeye ni hai, anaongea, anatenda wazi wazi, anahukumu kwa haki, muumbaji wa vinavyoonekana na visivyoonekana, na anaweza kuingilia historia ya mtu na kuibadilisha kabisa.

Jambo ambalo miungu haina sifa hiyo, hata kama kuna watu wanaamini miungu yenye uhai, bado haina uwezo wa kuwa na sifa kama ya Mungu wa kweli, maana mwenye kutoa uhai ni Mungu wa kweli tu. Sifa yake kuu yupo kila mahali kwa wakati mmoja, ni wa milele, na anahukumu kwa haki, sifa ambayo hata Shetani hana.

Mungu huyu wa kweli sio wa Israeli tu, huyu ni Mungu wa mataifa yote au ulimwengu mzima, mataifa yote yana haki sawa ya kuwajibika kwa Mungu wao, hakuna upendeleo wala ubaguzi katika hili.

Kila mwamini au kila mmoja wetu anapaswa kumtazama Mungu kwa jicho lingine, hofu ya kiungu inapaswa kuwa ndani ya kila mwamini, toba ya kweli inapaswa kuwa sehemu ya maisha ya mwamini, na ibada ya kweli na safi inapaswa kuwa ndani ya mwamini.

Soma neno ukue kiroho
Liwe jua iwe mvua soma biblia na kutafakari
Mungu akubariki sana
Samson Ernest
Unaweza kuthibitisha huyo Mungu yupo kweli na si hadithi za kutungwa na watu tu?
 
Muumba wetu ambaye ndio Chanzo Halisi anaishi ndani yetu sote na sio huko angani kama wengi hudhania,hata Yesu alifundisha ombeni ufalme uje,rejea sala ya baba yetu.

Warumi 3:11
Kila kitu amekifanya kizuri kwa wakati wake; tena ameiweka hiyo milele ndani ya mioyo yao; ila kwa jinsi mwanadamu asivyoweza kuivumbua kazi ya Mungu anayoifanya, tangu mwanzo hata mwisho.
Upo sawa
 
Hatuwezi kubishana na wewe kila mara, endelea na unachoamini

Kama huwezi kubishana usiweke mada zako hapa.

Kwa nini unataja kubishana wakati tunaweza kufanya zaidi ya kubishana, tunaweza kuelimishana?

Mimi sitaki kuamini, nataka kujua ukweli.

Kuamini unaweza hata kuami i uo go.

Sasa kama huwezi kuthibitisha utajuaje unachoamini ni ukweli?
 
Mtandao huu sio kwa ajili yako peke yako, utaamini kitu usichoamini, hata ulipoambiwa uliufanya moyo wako Mgumuu!
 
Usiangalie nani kauliza swali. Angalia hoja iliyoletwa.

Ukiangalia nani kauliza swali na kumshambulia yeye binafsi hiyo ni logical fallacy.

Ad hominem logical fallacy.

Jikite kwenye mada acha kumuangalia mtoa mada.

Umeshindwa kuthibitisha Mungu wako yupo?
 
Kama huwezi kubishana usiweke mada zako hapa.

Kwa nini unataja kubishana wakati tunaweza kufanya zaidi ya kubishana, tunaweza kuelimishana?

Mimi sitaki kuamini, nataka kujua ukweli.

Kuamini unaweza hata kuami i uo go.

Sasa kama huwezi kuthibitisha utajuaje unachoamini ni ukweli?
Naona unataka uthibitisho, imani haiwezi kuthibitishwa kama utakavyo maana ni kitu cha Kiroho zaidi na si kimwili.
 
Usiangalie nani kauliza swali. Angalia hoja iliyoletwa.

Ukiangalia nani kauliza swali na kumshambulia yeye binafsi hiyo ni logical fallacy.

Ad hominem logical fallacy.

Jikite kwenye mada acha kumuangalia mtoa mada.

Umeshindwa kuthibitisha Mungu wako yupo?
Mtoa mada ambaye amejiwekea hakuna Mungu na hata akielezwa haelewi, unataka tuendelee kubishana naye kila siku?, wakati upofu ni mkubwa na amekataa kusaidiwa apone hilo. Soma kulichoandikwa acha kuendekeza mabishano yasiyo na msingi wowote.
 
Hujaweza kuthibitisha kwamba Mungu yupo?

Kwa nini unasema Mungu yupo wakati huwezi kuthibitisha Mungu yupo?

Huoni kuwa unaweza kuwa unapotosha watu kuwa Mungu yupo wakati hayupo?

Unajali kama imani yako ipo katika ukweli au unahubiri tu imani yako bila kujali kama ipo katika ukweli?
 
Back
Top Bottom