Imani huja kwa kusikia!

Lanlady

JF-Expert Member
Feb 27, 2019
1,468
4,899
Kwa siku za hivi karibuni kumekuwa na matamko mengi, maonyo na katazo la kutumia baadhi ya vitu kutoka kwa baadhi ya viongozi wa kitaifa.

Yapo ambayo yana UHALISIA lakini SI YA KWELI! Na mengine huenda ni ya kweli lakini si LAZIMA kuyatamka.
Lengo la kutoyasema ni kulinda afya ya akili kwa wale wanaosikia na hawana uwezo kwa kuepuka kutokana na hali halisi ya maisha wanayoishi!

Mfano ni hili la waziri wa nishati kusema kwamba matumizi ya kuni ni sumu kwa wanaotumia.
Inaweza kuwa ni kweli, lakini je kuna namna ya kuwaepusha watumiaji na matumizi hayo?
Au ni kuwapandikizia hofu na kuanza kuhisi kuwa tayari wameathirika na sumu hiyo na wakati huo hawana mbadala wa nishati hiyo?

Leo hii kumekuwa na matamko mengi yenye kutoa onyo juu ya matumizi ya vitu ambavyo vinatumiwa zaidi na watu wa tabaka la chini.

Wapo waliozungumzia sana kuhusu matumizi ya unga usiokobolewa (dona) kwamba una sumu. Je, utafiti umefanyika kwa kiwango gani? Umefanywa katika mazingira gani?

Au ndiyo yale yale ya namna ya kuhifadhi samaki kwa watu wa kanda ya ziwa(sitaki hata kusema kama alivyosema mhusika) kwamba ni chanzo cha saratani?
Hizi tafiti zinafanywa kwa mlengo upi?

Si ajabu sana leo hii kusikia mtu akisisitiza matumizi ya chakula fulani kwamba kinaongeza nguvu za kiume nk, je kuna ukweli?
Au ni kwa sababu za kibiashara?

Mambo kama haya yanaweza kuonekana ya kawaida lakini yana athari sana kisaikolojia hasa pale mhusika anaposhindwa kupambanua!

Tusaidiane ili kuokoa afya ya akili ya watanzania
 
Back
Top Bottom