Imani hizi zinatupeleka wapi?

Imani hizi zinatupeleka wapi?

CharmingLady

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2012
Posts
18,304
Reaction score
12,997
Habari wakuu,

Angalizo kwa Mods...... Iwapo hii mada ilishawahi kujadiliwa humu ruksa kuunganisha.

Kuna imani ambazo watu wengi wanaziamini, kama hizi......

Iwapo baba/mama amefariki huwa wanachukua kipande cha nguo ya marehemu na kumfunga mtoto wa marehemu (hasa watoto wenye umri mdogo) ili asipatwe na maruweruwe, hivi kuna uhusiano gani kati ya maruwereruwe na marehemu?

Nyingine hii, watoto wa marehemu (hasa wadogo) huenda na kugusa paji la uso la marehemu ili kuzuia asipatwe na maruweruwe.

Watoto wadogo (wengi wetu tumewaona katika vyombo vya usafiri wa public au hata mtaani na wengine hivi ninavyoandika ni wahusika) hufungiwa kitambaa cheusi mikononi, kiunoni au hata mguuni. Kitambaa hiko huwa nimewekewa kitovu chake kilichokatika akiwa na umri mdogo, au nywele za kwanza kunyolewa. Hivi hiko kitovu huwa kinasaidia nini au hizo nywele???

Nyine hii: Mtoto akikatika kitovu utasikia USIKITUPE HOVYO, mara peleka kazike kwenu. au mtoto akinyolewa kwa mara ya kwanza, utasikia tuna hizo nywele, mara sijui weka wapi..........

Je kuna mafanikio ya hayo yafanywayo?
 
charminglady kwakweli nimesoma kitu kipya leo kutoka kwako, sijawahi hata kusikia haya. Nilipokua mdogo maiti au jeneza tulikua tunaogopa sana na watu wakipitisha jeneza kwenda kuzika hua unaweza kupata homa kwa ule woga, sijui tulikua tunatafsiri vipi ila tulikua tunaogopa sana. Sasa tena aende kumgusa? Kwanilipotokea mimi hii ni ngumu sana
 
Last edited by a moderator:

Mkuu nahisi unaishi ushuani... Sie tulikulia uswazi tushasikia na kushuhudia mengi aisee... Mengine hata ukisimuliwa unaweza kuona kama kichekesho lakini ndio imani za watu zilivyo!
 
Last edited by a moderator:
hayo ni mambo ya kimila zaidi, ila suala la nywele kwa mtoto mchanga kwa majibu ya mafundisho ya uislam zinapaswa kupimwa baada ya kuzinyoa na uzito wake unaufananisha na thamani ya dhahabu kwa wakati huo, basi ikiwa ni gram kadhaa utamtengenezea hereni akiwa mtoto mwanamke ikiwa mvulana thamani ya dhahabu ile unaitoa sadaka....
 
Imani za watu hizo,hutakiwi kuzijadili humu.
 
Tofauti na kumtolea mtoto hekaluni, au kifanya ibada ya maziko ni ipi? Ni imani na zinapeleka watu kwenye upeo wa imani zao.

Labda tujadili ubora wa imani ya kisabato over imani za kienyeji (mila) but again itakuwa ni malumbano tu. Maana ni sahihi kwa muumini mnayeshare naye imani halafu anafuata na imani nyingine then unajadili naye kuhusu mchepuko wake kiimani. Au kama wote mna imani ya kutoamini uwepo wa Mungu then unaweza kujadili sababu ya mtu kuogopa mzimu ambao according to Atheists ni illusion tu.
 
hakuna imani mbaya duniani, kila imani inamfaa anaeitumia, kwa mfano mbona hujajiuliza kuwa hicho kitovu kikimgusa mtoto kwenye kinena(chini kidogo ya tumbo)kama mtoto huyo ni wa kiume anakuwa -------(Anakosauwezo wa kuzaa) pili....mtoto anafungwa kitambaa mkononi au kiuzi cha sanda kama akifiwa na mzazi ili kumuepusha mtoto kuweweseka, na kuweweseka huku kunatokana na mtoto mdogo anauwezo wa kuona kimvuli cha huyo marehemu,kwani hukaa katika nyumba hiyo au mazingira hayo kwa siku 40, ndo maana ikifika siku 40,tunafanya kitu kinaitwa arobaini ya msiba ambayo watu wengi hawajui ina maana gani, na ndio maana hicho kitambaa hukaa mkononi kwa siku arobaini......hicho ni kitu kidogo nachokifahamu kama nimekosea kidogo basi kumradhi, am human being
 
charminglady kwakweli nimesoma kitu kipya leo kutoka kwako, sijawahi hata kusikia haya. Nilipokua mdogo maiti au jeneza tulikua tunaogopa sana na watu wakipitisha jeneza kwenda kuzika hua unaweza kupata homa kwa ule woga, sijui tulikua tunatafsiri vipi ila tulikua tunaogopa sana. Sasa tena aende kumgusa? Kwanilipotokea mimi hii ni ngumu sana

ni kweli hata mimi nilikuwaga mwoga nikiona majeneza live nimeanza kwenda msibani ukubwani kuanzia miaka 19 kwa mara ya kwanza baada ya kuona majeneza yakiuzwa live hospital flan hivi niliogopa tukio lilikaaa kwenye akili yangu nikaona kama uchuro flani ikabidi niwe nashirikishwa misiba inapotokea
 
Ila watoto wa sasa na utoto wetu ni tofauti, wao wa miaka hii hawaogopi na wanajua kila kitu
 
Ukifuatilia mambo ya mila za watu utashangaa mambo mengi sana,
1.Wengine ile mila ya mke wa marehemu lazima afanye mapenzi na mwanaume wanaita kumtakasa(WAKURYA}.

2.Bint kabla hajaoelewa inatakiwa kwanza atembee na kaka yake(WAMBULU}.
 
attachment.php
 
Attachments

  • DSC06514.JPG
    DSC06514.JPG
    136.4 KB · Views: 585
Back
Top Bottom