Tuongelee AirBnB + Tourism hapa Tanzania. Watu wanatengeneza pesa nyingi. Experience ya miezi 2 nikisafiri Tanzania

MURUSI Hebu fafanueni vizuri huo utapeli wa jamaa na amewahi kumtapeli nani usikute ni chuki binafsi mnaleta.

Wengine tupo serious tunataka tufanye biashara na jamaa.
Acheni roho za kishetani nyie matanzania , wapi mmepigwa hela zenu.


Mbona kuanzia mwanzo hadi hapa tulipo katika thread hii Hakuna mtu kaleta real evidence kuhusu kutapeliwa zaidi ya kumchafua mtu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acheni roho za kishetani nyie matanzania , wapi mmepigwa hela zenu.


Mbona kuanzia mwanzo hadi hapa tulipo katika thread hii Hakuna mtu kaleta real evidence kuhusu kutapeliwa zaidi ya kumchafua mtu

Sent using Jamii Forums mobile app

Mkuu hao watu wanaona WIVU nikiandika mambo mazuri hapa JF.

1 • Wanatamani wangekuwa wao ndiyo wanafanya hiki nachokifanya (hii inaweza kuwa reason kubwa lakini hawana uwezo)

2 • Ni haters. Haters are going to hate no matter what.

3 • Lakini kwangu watahangaika sana. I keep doing what I’m doing . Na hii ndiyo inayowaumiza zaidi.

4 • No matter what they gonna say or do I won’t stop

Blessed Sunday from Njiro, Arusha 🥂
 
Habari niko Zanzibar, n
Greetings JF massive!

It’s been long time.

Nimekuwa busy nikisafiri Tanzania na Kenya.

Mwaka 2020 nimepanga kusafiri zaidi hapa Tz ili niielewe zaidi nchi yangu na mimi kutumia opportunity kutengeneza pesa kupitia tourism.

Nashukuru nimekamilisha awamu ya kwanza na sasa ninarudi mzigoni hapa JF nikiendelea kuandika na kufundisha kuhusu online freelancing, dropshipping na njia nyingie tofauti za kutengeneza pesa Online kama vile AirBnB (hii leo nitaongelea kidogo) lakini pia leo nitaongelea kuhusu Tourism hapa Tz na muelekeo wake.

Je, uingie kwenye biashara ya utalii au usiingie?

Je, pesa zipo au ni nini?

Nakusihi kaa mkao wa kutulia kwasababu this post is going to be long.

Lakini usijali nitaweka picha ili isiwe boring.

Kwa watu wanaonitumia emails or everywhere nitaanza kujibu j3. Leo ninamuda kwaajili ya hii post tu.

1 • December 19, 2019, Hot Spring, Boma Ng’ombe Moshi.

View attachment 1370843

Hii sehemu watu wengi hawaijui. Lakini ni moja sehemu poa sana yakwenda ukiwa Arusha au Moshi.

Kutoka Boma hadi Maji Moto Spring ni mwendo wa dk 30 hivi kwa gari.

Nimefika Maji Moto saa 4 asubuhi hivi nikitokea Arusha na marafiki wawili.

Mmoja toka Atlanta US mwingine mTz kama mimi. Wote hawa ni girls. Kidume peke yangu.

Tumefika reception (ipo kilawaida sana) tukalipa entrence fee tukaingia. Mgeni ni Tsh 10,000 Mtanzania Tsh 5,000.

Hapa tumekuta families toka Kenya na familia za kitanzania zinazopenda kufanya utalii wa ndani hasa kipindi cha mwisho wa mwaka wanakula bata.

Kila mtu anatabasamu.

Kitu kilichonishangaza wakenya wengi wanaofahamu hii sehemu labda kuliko waTz.

Inashangaza unauliza watu Arusha hawafahu au hawajawahi kufika Hot Spring.

Inabidi uende pale ukajitakase man.

Hii place is magical.

Hot Spring ni sehemu nzuri si tu mazingira yake na maji masafi. Lakini pia maji yake ni ya uvuguvugu. Sehemu hii ina miamba moto inayosababisha maji kupata moto.

Maji yake ni masafi hatari. Unazamisha shilingi 500 divers wanaifuata hadi chini wanaichukua kwa meno.

Hii nilifanya. Jamaa aliniambia ukitupa 500 naweza kuifuata halafu naichukua kwa meno. Nilipanda nayo juu unanipa $5.

Hot Spring tumeogelea hadi mida ya saa 9 hivi alasiri. And yes we had lunch box.

Ukienda adventure yoyote na unajua uwezekano wakupata msosi mzuri inabidi uwe na lunch box upunguze njaa. Pia maji ya kunjwa yakutosha. Stay hydrated people.

Ok. Tumemaliza huo muda tukaanza Safari yakurudi Arusha.

2 • January 1, 2020 Magoroto Tanga.

View attachment 1370846

View attachment 1370847

View attachment 1370848


Magoroto ipo Muheza Tanga.

Nimefika Muheza very late in th evening.

Mpango wangu nikitaka nikakae kwenye tent ️ pale Magoroto estate lakini nilichelewa kufika Muheza kwahiyo nikapata lodge nzuri nikakaa hapo for one night.

Asubuhi mapema after after breakfast (hapa pia nikakutana na wakenya toka Mombasa kama sita hivi nao wanapata breakfast waelekee Magoroto.

Niliongea nao kidogo wakaniambia ndiyo mara yao ya kwanza kuwa Tz na wamependa kila kitu kwa siku yao ya pili. Walifika jana yake kama mimi.

Njia ya kwenda Magoroto ni mbaya sana.

My idea was to rent a car Muheza but nikapata ushauri mzuri sana Kwa bodaboda hodari kabisa Steven kwamba he can give me a ride to Magoroto forest.

And he was right.

Njiani nimekuta magari mengi yamekwama au wanafikiria kugeuza.

Kama hauna option ya 4X4 vehicle usiende na Alphard mkuu wangu.

Nilikutana na watu wanaenda na Alphard Magoroto. Yes unaweza kufika lakini utaua gari yako.

Nimefika Magoroto forest saa 3 :30 hivi asubuhi.

Nikaenda mapokezi. Nikalipa kila kitu + including 2 nights stay kwenye tents zao.

Saa 4 hivi asubuhi tukaanza activity ya kwanza hiking to water falls and viewing point.

Magoroto is beautiful.

Kijani kila sehemu.

Njiani tunakutana na wakazi wanakijiji wanatembea kwenye njia nyembamba zilizofunikwa na miti mirefu ya asili.

Kwenye hii hiking tulikuwa 3 na guide wanne.

Wawili ni brothers toka Musoma. Wote ni wafanyakazi kwenye provate sector na mmoja aliniambia kwasababu kazi zake anakuwa busy sana kwahiyo ikifika December lazima asafiri aende sehemu iliyotulia either na mshikaji wake au mamiloo.

Poa sana Hii experience kukutana na watanzania wenzako mkifanya utalii wa ndani.

Day Two in Magoroto.

Hii siku nilitumia horseback riding asubuhi. Mchana I stayed in my tent na kuogelea. Jioni nilitumia kwaajili ya visualization na kushukuru kwa yote yaliyotokea toka niwe hapa siku moja iliyopita.

Day Three in Magoroto.

6am nilikuwa na darasa la kiswahili Online kwa saa moja.

Nikafundisha kwa saa moja halafu sasa ratiba yangu ya kilichonileta hapa ikaendelea.

Yes, mimi ni mwalimu wa Kiswahili. I teach people Kiswahili Online. Na hii opportunity ilianza baada ya mimi kufanya kazi fulani UpWork na kujenga mahusiano mazuri na client. Kumbe naye ana website ya kufundisha lugha.

Ok...

Siku ni kwaajili ya bike ride halafu napata lunch nakuwa nimemaliza 2 nights three days. Tayari kurudi Arachuga.

I will definitely go back to Magoroto. Soon.

3 • January 14, 2020 Nairobi Kenya

View attachment 1370849


Ninasafiri kwenda Nairobi mara nyingi sana. Na mara zote inakuwa kwa kazi fulani.

This time ni kwaajili ya kukutana na some long time friends wakitokea US.

Tar 12 January nafanya booking AirBnB.

Napata two bedroom apartment mtaa wa Mararo Avenue off, Riara Rd, Nairobi, Kenya.

Ni apartment nzuri. Ni safi, furniture ni nzuri na pia communication na host wangu ni nzuri sana.

Plan ni kukaa hapa one night halafu Arusha Tz.

Asubuhi baada ya breakfast asubuhi (we prepare breakfast ourselves) tunaenda Karen tusalimia some friends waliohamia kesho toka German la baadae kuanza Safari ya Aruasha.

Karen ni sehemu nzuri sana Nairobi. Many wealth people live there. Ni sehemu nzuri kwa watu wenye familia. Nimeona kuna nyumba nyingi na wenyeji watu wakasema hapo wanaruhusu kujenga nyumba tu na si apartment buildings.

Saa 9 hivi jioni tunaanza Safari kurudi Arusha. We are driving ourselves hatuwazi kuchelewa.

4 • February 8, Singida Tanzania.

View attachment 1370850


Singida was not in my list. Lakini kwasababu mimi na traveling buddies wangu hatukuwa na haraka na lengo ni exploitation tukakaa Singida for one night.

Singida hakuna AirBnB kwahiyo tukachagua one of the best hotels in Singida. Mita chache toka hotel kuna Lake Singidani.

Jioni tuliyofika hatukupata time nzuri yakuangalia nini cha zaidi kwenye hili ziwa kwahiyo kesho yake asubuhi kabla ya check out tukaamua tuende na yoga mats pale ziwani kwaajili ya yoga.

Hii sehemu nitarudi tena. This time nitakuwa na group la tourists na ninawapatia yoga session. Pia muda wa jioni good music huku watu waki-enjoy drinks zako

Ok.

Around 11 am tukaanza Safari kuelekea Mwanza Tz.

Tukapita Tabora, Shinyanga halafu tukaingia Mwanza.

Tabora kuna kipande cha barabara ni kibovu sana.

Ni rahisi kupata ajali kama ni dereva mpya.

Na hii sehemu alikuwa anaendesha manzi toka US. She loves to drive na ana speed si mchezo.

5 • February 9, 2020 Mwanza Tz.

View attachment 1370851

Baada ya takribani saa 5 hivi tunaingia Mwanza.

Ni saa 12 jioni. Tunaelekea nyumba tuliyo rent AirBnB hapa Mwanza.

Hii nyumba (three bedroom house) ni nzuri sana.

Ina View matata ya lake Nyanza (Victoria) 180 degrees.

Pia ni mita chache tu hadi kwenye fukwe ya ziwa.

Ni modern house kwahiyo kila kitu ndani ni high end items. Kuanzia furnitures hadi vitanda comfortable vya kulalia. Madirisha makubwa you can see the view of the lake from your bedroom.

Ningeweza kuweka picha hapa lakini Nadhani haitakuwa sawa kama mmiliki wake anapitia humu.

Kingine nilichogundua and you can’t bel Mwanza kulikuwa na nyumba/apartments tatu tu AirBnB. Wakati Arusha ni zaidi ya nyumba/apartments 400+

Inabidi watu wa Mwanza tuongee vizuri. Utalii unakuja kwenu mjiandae.

Watu siku hizi hawapendi kukaa hotel au lodge. Tunataka apartment au nyumba. Iwe kwa siku chache au miezi.

Well, hapa mwanza Plan ni kukaa two weeks.

Siku moja baada ya kufika asubuhi tunaelekea Bujora Sukuma Museum.

View attachment 1370852

View attachment 1370856

View attachment 1370857

View attachment 1370858

Ukitaka kufahamu kuhusu utamaduni wa kina ngosha basi hapa ndiyo mahala sahihi.

Big ups kwa Wasukuma. Utamaduni wenu ni imara sana na ancestors wenu walikuwa vichwa kwelikweli.

Siku ya pili tunaenda sokoni kununua veggies, fruits na kila kitu tunachohitaji kwaajili ya kupika siku chache zijazo.

Oh nisisahau tukaenda na Rock City Mall.

Sehemu nzuri na maduka mengi yanaongezeka pale.

Day three Saanane National Park.

View attachment 1370860

View attachment 1370862

Ukienda Mwanza make sure you get time to visit Saanane island.

Tumefika sehemu ya kulipia kabla yakunda boat saa 3 asubuhi hivi.

Tukalipa kila kitu. Captain akafika na small boat tukaenda hadi kisiwani tukiongozana na guide. A very beautiful girl from Arusha. She just finished college na yupo pale akijitolea na kupata experience.

Saanane ni nzuri sana. Kuna Zebras, Wildbeast, Gizalle, Lion (in the cage though) different species of birds + spectacular view of lake Nyanza.

Hii siku ilikuwa nzuri sana. Tour yetu (kwenye hii Park ni kutembea kwa miguu) iliishia jumping stone. Tulikuta wanafunzi wa shule ya binafsi ya sekondari nao wamekuja hapa.

Day Four

Malaika Beach and resort.

View attachment 1370864

Hii resort ni nzuri sana. Mazingira ni clean

View attachment 1370865


Pia food katika restaurant ni nzuri. Japo hawana option nyingi kwa vegans tunaotumia plant based meal.

Hii resourt wateja wake ni government officials lakini pia diplomats.

Mwanza utalii bado haujakuwq vizuri. Kwahiyo japo hii resort ni nzuri sana (5 star) lakini watalii toka nchi nyingine hakuna kabisa. Restaurant kulikuwa na watu labda watatu na wote inaonyesha ni wenyeji wa hapa Mwanza.

Day Five.

Hii siku tulipanga kwenye Gambosh.

Yes Gambosh kijiji kinachopatikana Geita (you can correct me if I’m wrong).

Tatizo tulilopata watu wa hapa Mwanza hawafahamu sana kuhusu Gambosh.

Wengi wanasema aaah nilisikia tu.

Tukajaribu kuongea na tour company hapa Mwanza napo hatukupata maelezo mazuri kwahiyo ikabidi tuahirishe. Labda kipindi kingine nitapenda niende Gambosh na nisimuliwe visa vyota vya huu mji/kijiji cha kusadikika.

Kwa siku zilizofuata tulikuwa tuna explore Mwanza town.

We visited some of best restaurants in town kwaajili ya lunch ya dinner.

Pia siku moja kabla yakuondoka one of friends in Mwanza akapendekeza tuende Cask Bar & Grill. Very nice place Hii ipo Rock City Mall sehemu ya nyuma.

Hitimisho.

I’m thinking of organizing Tour to Magoroto na baadae Kigali Rwanda + South Africa kwa siku za baadae.

Let me know if you are interested in traveling na tunaweza safiri pamoja.

Cheers 🥂

Sent from my iPhone using JamiiForums
Habari niko Zanzibar ni Tour Operator , na deal sana na Eco & Cultural Tourism, tuwasiliane info@ecoculture-zanzibar.com
 
Back
Top Bottom