ILIPOISHIA...!!

ILIPOISHIA...!!

Joined
Jul 9, 2016
Posts
62
Reaction score
16
Wakati huo john alikuwa amezidisha ile tabia ya ulevi uliopindukia.wazazi wake kwa kutaka kuepukana na aibu hiyo wakamshawishi aoe kwa matumaini kuwa pepo mbaya aliemkumba mwanao angeondoka baada ya vuta nikuvute ya miezi kadhaa john aliafiki shauli hilo kwa masharti ya kupewa shilingi milioni mia sita za kitanzania za kuanzisha biashara ya usafirishaji wa mizigo alitimiziwa.mwanamke wake wa kwanza kumuoa aliitwa prisca mgahawani msichana uyo alietumia usichana wake wote kujituma kimasomo na kufanikiwa kupata shahada tatu nje ya nchi hakukataa pale wazazi wake walipomiuta na kumkutanisha na familia ya maganga waliotaka amuoe kijana wao na kilichommaliza kabisa prisca ni siku aliyokutanishwa na john na kuvikwa pete ya uchumba aliapa kutoisahau siku hiyo kweri ni mzuri wa sura na umbo pengine ata zaidi ya sifa alizosikia kwa rafiki zake kama sikosei watakuwa wamekosea waliposema ni handsome bali walitakiwa kuongeza neno’’sana’’ katika sentensi hiyo ayo yote yalielea kichwani kwa prisca pindi alipomtia machoni john naam! Kijana alieteka dare s salaam kwa uzuri na sifa zingine kemu kemu na muda huu anamchumbia na kumtaka awe mke wake bahati ilioje! Maskini hakuwa na wazo lengine alikubali pasipo kufikiri kama anamfahamu kitabia au la…!


*****************

Baada ya miaka miwili walifanikiwa kupata watoto wawili ambao waliwaita Isaac na david .baada ya apo ndoa yao iligeuka chungu kwa prisca kwani alichemsha kuishi na john aliegeuka mbogo vitisho visivyoisha ,kuludi usiku wa manane na vipigo alivovipata baada ya kuuliza mabadiliko ya ghafla ni sababu zilizomshawishi kuomba talaka .katika hali ya kushangaza kwa prisca john hakustushwa na ombi ilo hilo tofauti kabisa na prisca alivotegemea alidhani angeombwa msamaha na huo kuwa mwisho wa mateso kwenye ndoa yake na furaha kuchukua nafasi,alikosea sana kwani kama angefahamu moyo wa john ulivyo asingepoteza muda wake kuwaza ivyo.taratibu zikafuatwa hatua kwa hatua hatimaye john ma prisca wakatalikiana na kugawana kila walichochuma kwa miaka miwili ya ndoa yao na watoto wao wawili Isaac na david wakiwa na ruhusa ya kuishi na mama yao iliotoka kwa mahakama.

Itaendelea.. Nahitaji sana komenti zenu ili kunitia moyo na kunirekebisha makosa wakuu.
 
Nzuri sana ila usikae muda mrefu sana kabla ya hujaituma nyingine
 
Back
Top Bottom