Ilikuwa lazima TBC kufanya sherehe ya World Cup?

Ilikuwa lazima TBC kufanya sherehe ya World Cup?

Hivi wanajamvi kuna ulazima gani hasa kutumia resources za taifa hili kufanya ghafla ya kufunga kombe la dunia? Inanishangaza kuona mali za nchi na hata muda adimu wa nchi hii watu wanakaa na kujipongeza eti wameweza kurusha matangazo ya kombe la dunia.

ukiwa hukualikwa acha chuki, na kama unaishi kwa chuki hamia israel
 
Kwani ni lazima utazame? kuna ma channel kibao ya ndani na nje ya nchi. Ukisikia kuhororoja kwa nyanya mbichi ndio hivi.

Hawa watu wanaolaumu ndio mabingwa wa kuitazama TBC!! Achana nao, isingekuwa TBC wasingepata huo mpira wa Kombe la dunia.
 
Mwanzo mzuri, ikiisha hapo tuhoji na mawe ya msingi kuwekwa kwa gharama na uzinduzi wa shughuli ambazo watu wanalipwa ka ajili hiyo!!!!

Ili viongozi wajue watu wako macho na wanahoji, baada ya muda wengi wataanza kujiuliza mara mbili kabla ya kufanya mengi!!
 
Kizazi cha nyoka lazima kifurahie. Pole kwa kupiga makofi hata mkiwa chooni.
 
Hongera tbc...achani kulalanmika. Wao watapataje hata hizo allowance. Nyie kila siku mko safari wenzenu kujinafasi mnaona haya. Kaa kimya kama huna cha kupost
 
Watz tunalalamika fanya kazi huko makazi mnamikutano kila siku au kuwa hairushwi ndo mnachonga.. wasingetusha mngrporomosha matusi. Tbc msisikilize watz hawana jema
 
Hivi wanajamvi kuna ulazima gani hasa kutumia resources za taifa hili kufanya ghafla ya kufunga kombe la dunia? Inanishangaza kuona mali za nchi na hata muda adimu wa nchi hii watu wanakaa na kujipongeza eti wameweza kurusha matangazo ya kombe la dunia.

ndo kodi zishaliwa tena hivyo,mara kamati ya mapambo,ukumbi na posho.ccm bana
 
Fungu kuu limevyutwa hiyo ilikuwa kuboresha uvutaji wa fungu
Ili wajinga wasijuwe na wajanja wakihoji wajibiwe kwa kutolewa mfano wa hafula hiyo!
 
Mkuu Nyanya Mbichi, kwa vile walianza kwa tafrija, wanamaliza kwa tafrija na kupongezana kwa kazi kubwa na nzuri walioifanya kututangazia kombe la dunia!.

Lengo la kuitana ni ku share nazuri na wenzio.

Matukio hayo na mengine yote ya TBC yamegharimiwa na mimi na wewe, yeye na yule, sisi na wao, wale na yule, yeye na yule, na wao, na wale kupitia kodi zetu na hatuna tatizo na hilo.

Kuna sherehe ngapi za kitaifa zinagharimiwa na mabilioni ya shilingi what for, mbona hamsemi?!, badala ya kuishukuru TBC imekuletea kombe la dunia mechi zote bure, ndio kwanza unalaumu!.

Ama kweli watu hawana shukrani, ukimtendea meme, atalalamika, ukimtendea ubaya ndio kabisa!.

Watanzania tumezidi mno kulalamika, kila kitu kulalamika, kwani wewe ulitakaje?, pati iwe ya Brasil tuu tukifanya party huku unaumia roho?!.

Pole!.
Pasco
Halafu Pasco acha kuongea kama unaongea na watu wa 1960's!
Ni nini hapo unaita shukurani?
kuna shukurani kwa kile tunacholipia?
 
Itakuwa ni salio la wafadhili wa ule mtanange;
Vinginevyo nao walijisahau kama wale walioanza kurushiana
mangumi huku tunawatazama.
 
Halafu Pasco acha kuongea kama unaongea na watu wa 1960's!
Ni nini hapo unaita shukurani?
kuna shukurani kwa kile tunacholipia?
Mkuu daviey69, shukrani ni appreciation for the little you got. Wewe hats kama umeoa na una familia, ni jukumu lako to provide for your family, kumnunulia nguo mkeo, ni jukumu lako, na yeye ni haki yake kuvishwa na wewe!, lakini bado unapomletea, kama ana shukrani, atasema asante!.

TBC wametutangazia Kombe la Dunia, kuna watu wamefadhili michuano hiyo, kuna watu hawakulala na wamekuwa wakikesha usiku na mchana kuhakikisha tunaona, ile party ni appreciation za uongozi wa TBC kwa wote ukiwemo wewe uliongalia!.

Hata kama unaiendesha TBC kwa kodi yako, wanapofanya vizuri, unawajibu wa ku appreciate!. Mbona kwenye miziki, tunalipa kiingilio, na muziki ukikolea, tunapiga makofi, tunatunza, na bia tunawanunulia?!.

Ukosefu wa shukrani, appreciation ni tatizo kubwa humu JF!.

Tubadilike!.

Pasco
 
Last edited by a moderator:

Alaaa kumbe ndo maana hata ikulu na wizara inatengewa fungu la CHAI. Ha ha haaaa Yai moja ikulu shs 1000! Hawana hata haya! Anyway ni SHUKRANI TUUU. Asante Pasco kutufungua macho!
 
Alaaa kumbe ndo maana hata ikulu na wizara inatengewa fungu la CHAI. Ha ha haaaa Yai moja ikulu shs 1000! Hawana hata haya! Anyway ni SHUKRANI TUUU. Asante Pasco kutufungua macho!
Mkuu Aikandao, mtoto wa Mangi Mkuu, yes yai la 1,000 ni la kuku wa kienyeji!, ndio mayai yanayoliwa mule kwenye nyumba kuu ni ya kuku wa kienyeji tuu!. Kwenye kula vizuri, kula vitamu na kula raha!, hakuna haya!. Hata mimi sina haya kwenye hayo unless unapenda vya kizungu, kuku wa kizungu, mayai ya kuku wa kizungu na huduma za kizungu, theya are all cheaper!, vya kienyeji ghali!. Au ?!.
Pasco
 
Back
Top Bottom