Ilikuwa haina maana kuzishindanisha shule, labda top students

Ilikuwa haina maana kuzishindanisha shule, labda top students

choza choza

JF-Expert Member
Joined
Jan 17, 2019
Posts
2,289
Reaction score
4,093
Shule za serikali kweli zinapata zero nyingi kuliko shule za Private

Lakini tukumbuke shule za Serikali zingejiendesha kama za private(mfano wa shule za gvt zinazojiendesha ki private Ilboru, mzumbe, Tabora boys nk) hizo zero sizingetokea kwasababu hao wakupata zero wangeishia kidato cha kwanza.

Sasa shule A inafanya mchujo mkali kuanzia form 1 hadi form iv kisha anachukua vipanga tupu anawafundisha.

Shule B anapewa watoto wenye uwezo tofauti tofauti na anatakiwa asiwachuje apabde nao wote mpaka form iv kisha baada ya Necta unamuita shule A ni bora anajua kufundisha zaidi wakati kachukua cream tupu.

Ndio maana kwa level ya Advace huu ushindani uko fair kwasababu wote private na goverment wanachukua cream zilizojichuja form 4.

Hivyo ilikuwa ni kuwapigia tuu promo Privates school ili wafanye elimu biashara.

NB: licha ya hivo mishahara duni na kutokua na motisha kwa walimu, uhaba wa walimu, wingi wa wanafunzi gvt schools pia ni factor ambayo inasababisha ufaulu duni.
 
Back
Top Bottom