EWGM's
JF-Expert Member
- Jul 22, 2013
- 1,521
- 2,112
Akili za Watanzania waliowengi ni kama bendera huwa wanafata upepo tu, hakuna tofauti ya wasomi wala wauza karanga mitaani. Kwa hurka hii mbaya sioni kama kuna siku tutanasuka kwenye hili tope zito la umbumbu. Nchi ikishakosa utofauti wa uelewa ni ishara tosha kuwa kuna shida.
Sijaelewa bado kama tatizo ni siasa au elimu, ujinga au uvivu, serikali au mazingira. Kwanini idadi ya watu kuwa wapumbavu inaongezeka siku hadi siku?
Ila hala hala kiangazi kinakuja na tope linaanza kukauka hivyo nasema tukiendelea hivi hatapona mtu.Wenye macho na waone na wenye masikio wasikie kama taifa tuko kwenye hali mbaya
==========================================================
UPDATE; 09/10/2017
Mvua zimeshasimama kunyesha na yale madimbwi/mabwawa machache yameanza kukauka. Hii ni ishara tosha kuwa kiangazi kinakuja na mioto michache iliyobaki imeanza kunyauka na mingine kufa kabisa. Ardhi imeanza kuwa ngumu na unyevuunyevu umeanza kupotea, hii ni ishara tosha kuwa ile safari yetu inajikamilisha. Jua likizidi sana ardhi itaanza kuwa ngumu na kuanza kupasuka basi tope limeshakauka.
Weledi haupo tena watu wanafanya mambo kufurahisha mtu/watu au kikundi fulani, kila mjinga au mwerevu mwenye fursa na yeye anaitisha press conference. Ikiwa makanisa yote yanasimama kwenye msingi wa ukistro iweje isahaulike Kristo alisimamia nini na pia upande huu mwingine wanataka kujua idadi yao wako wangapi nchini,hii ni ishara tosha safari imewadia.
Ikishafika mahali Katiba ikawa daftari la mazoezi kwamba sentensi inaweza kupigiwa mstari mwenkundu na sentensi ikaandikwa upya tena na mtu mmoja mpaka hapo tujue tumeshakaribia kufika. Tumenasa kwenye tope zito na linakauka kwa kasi mno ila kila kukicha najiuliza tutachomokaje hapa?
Some problems are so complex that you have to be highly intelligent and well-informed just to be undecided about them.