Ili tusipate hasara, Serikali ibadilishe Uwanja wa Ndege Chato 75% uwe wa Kijeshi

Ndo madhara ya nchi kuongozwa na mawazo ya mtu mmoja.Deni la taifa limepanda kwa vitu visivyo na ulazima kwa sasa,chato airport, kuhamia dodoma, ikulu mpya hizi pesa zingemaliza kabisa tatizo la ajira nchini
 
Ukipata akili hutaandika ujinga kama huu
 
La mhimu kidogo uliloandika hapa, ni kupinga kumlinganisha JPM na Nyerere, Hilo nakupa zote, mengine ni utopolo,

Ukija kupata akili ndipo utatambua kuwa hata hiyo mifumo huwa haiwekwi na Raisi ispokuwa ni wananchi wenyewe wanapoona kunahitajika hivyo, niambie leo, Je katiba inamapungufuu au haina?

Ukinijibu Hilo, nitakuuliza tena, Kwa nini Rais anaogopa kutupa katiba?

Unadhani ni Nani wa kutupa katiba Kati ya Raisi na wananchi?

Je, mifumo unayoitaka inatokona na nini??

Ukiyajibu hayo, nitakuona wewe hukwenda shule kusomea upumbavu
 
Hili ni wazo zuri sana
Big Up sana... Mawazo yako yamesadifu na nilichokua ninakiwaza muda mrefu. Kubadili airport ya Chato kuwa ya kijeshi ni wazo zuri sana na lenye tija.
Mimi naunga mkono hoja
 
Mara PAAAAAA jamaa kaibukia chato - naona watu watakavyokimbizana kuzikana kauli zao..
 
Kibali kinatolewa muanikie mpunga na mihogo stay tune ile hasara kubwa sana ....
 
... kwa jinsi Chato ilivyo jirani na mipaka yetu nyeti, pamoja na uwanja huo kugeuzwa kuwa wa kijeshi vilevile inahitajika kambi kubwa ya jeshi zaidi ya LUGALO!
👊 ✌️💥
 
Kweli kabisa
 
Sioni kama ni hasara kwa uwanja wa ndege kujengwa Chato. Kama ulivyoandika unaweza kutumiwa na jeshi kwa muda huu lakini kwa mipango ya miaka mingi ijayo wakati uwanja ule wa Mwanza ukiwa na shughuli nyingi ule wa Chato utakuwa ni uwanja msaidizi.

Tatizo letu watanzania ni kuendekeza siasa kwenye kila kitu. Kaskazini vipo viwanja vya ndege vingi na vinaigharimu pesa nyingi serikali katika kuvitunza lakini ule wa Chato unatazamwa kwa nongwa za ukabila!!.

Umeweka hoja ya uwanja mbadala kuwepo kwa sababu za kiulinzi, wenye akili zilizotulia watakuwa wamekuelewa.
 
Watu wanahasira sana na Shujaa wa Mazezeta ukijifanya kumsifiasifia ndio maana unakutana na majibu kama hayo
Wakati mwingine mnapomtukana JPM mnakuwa mkieleweka kama watu mnaotaka kuuendeleza ukabila na ushamba, tuhuma mbili alizopewa marehemu muda mwingi akiwa rais.
 
Tuondoe muono wa kila kitu kwa leo tuu. Uwanja wa Kilimanjaro ulianza kutumika miaka kumi baada ya kujengwa.

Uwanja wa Songwe ilichukuwa miaka 7 kuanza kutumika baada ya kujengwa, mpaka leo hii kuna ndege bado haiwezi kutua Songwe na ni ndege za kawaida tuu. Na ulijengwa kwa gharama kubwa kuliko uwanja wa Kilimanjaro.

Uwekezaji wa kiuchumi hauwekezwi kwa kuangalia leo tuu.
 
Mkuu jaribu kufikiria kwa mapana.. hakuna ukabila.. suala hili linaangaliwa kwa manufaa ya nchi.. Chato Airport hapana na ni hasara kubwa kwa taifa.. Viwanja kaskazini sio vingi unavyosema na gharama hazipo unavyosema.. KIA inajiendesha.. Arusha Airport inajiendesha.. Manyara Airstrip iko busy high season pamoja na Seronera.. Tanga Airport haitumiki
 
Hapo unapojaribu kuonyesha kuwa Chato airport haitakuja kuwa muhimu ndipo unapokosea.

Tanzania mwisho sio leo wala kesho wapo wawekezaji watakaokuja kutumia uwanja huo wa chato. Ni ubinafsi kudhani kuwa miaka ijayo hakutakuwa na watu wabunifu.

Tuondokane na hizi dhana za ukanda kila eneo linazo rasilimali ambazo zitakuja kuziinua miaka ijayo.

Sio Chato tu vipo viwanja vingi vya ndege vinapitia kipindi kigumu sasa lakini zipo siku vitakuwa vikitumiwa na kuingiza pesa.
 
Mkuu nakuelewa.. Kumbuka hapo Chato Airport imelala Billion zaidi ya 50. Uwanja mpaka uwe effective kwa matumizi ni miaka ya mbeleni sana.. Mkuu ulishawahi kufika Chato?
Uwanja kama wa Mwanza unahitaji upgrade kubwa sana.. Eneo la packing za ndege.. Jengo la Abiria.. Upanuzi wa tax packing.. Uwanja wa Mwanza unatakiwa uwe wa kimataifa... Hilo lilitakiwa kufanyika kwanza kabla ya kukimbilia kujenga Chato
 
Mkuu kwa sasa umeme unasambaa nchi nzima naamini zipo fursa nyingi zinakwenda kuibuliwa.

Nyumbani Ngara kuna ile shughuli ya nickel kuanza kuchimbwa maana yake kuna fursa nyingine za kijamii zina kwenda kuinuka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…