Ili tusipate hasara, Serikali ibadilishe Uwanja wa Ndege Chato 75% uwe wa Kijeshi

Tumbiliwaulaya

JF-Expert Member
Nov 22, 2020
280
500
magu chato air.jpg


Kwa heshima na taadhima napenda kuishauri serikali yetu adhimu,ibadirishe matumizi ya uwanja wa ndege chato ili tuepuke hasara itakayo tokana na uwanja huo kutotumika kikamilifu.

Uwanja huu wa kisasa umejengwa huku watanzania wakivutana na kurumbana wengine wakidai umejengwa kisiasa wengine wakisema upo kwenye irani ya chama cha mapinduzi kwa hivyo hakuna makosa, na mengine mengi

CCM answers to opposition on Chato Airport accusations

Mimi si mwana siasa sitaki kusema mengi kuhusu maoni ya wanasiasa hili tuwaachie wanasiasa sisi tuangalie ni nini kifanyike ili uwanja huu uwe wenye manufaa kwa taifa letu.

Kwanza napenda kuwatoa hofu wale wote wanao dhani kuwa uwanja huu baada ya kufariki Rais JP Magufuli basi hauna faida tena kwa kuwa hakuna ndege za kutumia tena uwanja huu, zifuatazo ni faida kadhaa za uwepo wa uwanja huu katika eneo hilo.

Uwanja wa chato upo km 131.26 za anga kwenda uwanja wa ndege Mwanza lakini pia Entebe airport Uganda sio mbali, uwanja huu utafaa zaidi kwa ndege kubwa endapo zitapata dharula ya kutua katika uwanja wa ndege mwanza au hata Entebe, hivyo uwanja ulio karibu zaidi ni Chato kuliko kurejea Dar, Kir au Dom.

Hili halina ubishi liko wazi, na pale Mwanza airport itakapo anza kutumika kikamilifu kimataifa baada ya ujenzi kukamilika an alternative airport in case of emergency ni Chato,hii itakuwa ni sifa ya nyongeza kwa uwanja wa kimataifa Mwanza.

Kwa kuwa watanzania tumezoeshwa kujengewa miundombinu inayofaa kwa wakati uliopo na si miundombinu inayofaa sasa na miaka mingine hamsini mbele, tunaona leo tu peke yake lakini hatuna uthubutu wa kuangalia faida hata ya miaka kumi tu ijayo, kila kitu kina panuka utalii utaongezeka mahitaji kwa ujumla yataongezeka kwa miundo mbinu iliyopo, kwa wale mlio na wasiwasi mnaihukumu Chato airport kwa maono ya miaka mingapi mbele? na ndipo mnapopata jibu la kwamba haina faida?

Kwa mnaojua historia ya nchi yetu mtakumbuka mji wa Mwanza uliwahi kushambuliwa mara kadhaa kwa ndege za kivita toka mataifa jirani mwaka 1972 na kipindi cha vita ya Kagera 1978-1980 kwa misingi ya kutaka kushambulia kikosi chetu imara cha anga kilichopo mwanza, ingawa mara zote majeshi yetu yalifanikiwa kuzidungua ndege za adui, hii inaonyesha kuwa ipo sababu sasa tena ya msingi kukihamisha kikosi cha anga kilichopo mwanza kwenda chato, na hapo kitakuwa kimkakati zaidi kuliko Mwanza.

Tukumbuke lake zone ndio ukanda ulio zungukwa na nchi nyingi kuliko ukanda mwingine wowote ule na mkumbuke jirani au rafiki yako wa leo ndio adui yako wa kesho.

Kwa sasa uwanja wa ndege wa mwanza unatumika kwa madhumuni yote mawili lakini kwa asilimia ndogo za kijeshi na unatambulika kuwa uwanja wa kiraia, kwa Chato iwe tofauti utumike kwa asilimia nyingi kijeshi na chache kiraia, hata kama utajulikana kama uwanja wa kijeshi chato poa tu. Msipoteze muda mpeni mabeyo hicho kiwanja kina mfaa.

Karibuni wenye mawazo ya kuona mbali mchangie katika hili ili kutoa mwanga wa matumizi chanya ya uwanja wa Chato.
 

FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
24,311
2,000
Ushauri wako ni mzuri mno, ila mimi bado nasema hivi tulifikiri nini hadi tukaamua kujenga uwanja huu mkubwa hivi kwa kutumia ma-billioni ya hela kule kijijini? tuanzie ha hapa kwanza - unajua huwezi kutatua tatizo bila kujua chanzo chake.
 

dudus

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
15,243
2,000
Halafu ukishabadilishwa kuwa wa kijeshi automatically hakuna lolote litakaloruhusiwa kuhojiwa kuhusiana na airport hiyo henceforth! Nadhani kutunza legacy ya mwendazake chochote alichokifanya kibadilishwe kuwa cha kijeshi!
 

Pslmp

JF-Expert Member
Mar 18, 2021
1,630
2,000
Yote yenu, mwenye maono yake keshaondoka.

Taifa linalobebwa na mtu mmoja Kwa ngazi ya Uraisi kufikiri yeye na kutenda yeye na katiba imempa Uhuru huo, halafu sasa, baada ya kutenda hivyo, ndio watu waanze kuuliza Kwa nini uliamua kujenga uwanja ama kununua Ndege ili Hali tulitaka utuletee bahari Dodoma, wewe utakuwa Dicteta.

Narudia tena, Wote wanaomuita Raisi wetu awe JPM ama mwingine ajaye kuwa ni Dicteta ni wapumbavu na hawana uelewa wowote

Labda niwaulize nyinyi wajinga mnaomlaumu Hayati JPM, Ni wapi yalipo/ulipo mpango wa kitaifa?

Kama nafasi ya Uraisi imeachwa itende Kwa niaba ya wote, mnategemea nini.

Narudia tena, mpaka huu muda, si Raisi wa Kwanza mpaka sasa, hakuna Rais aliyetenda mengi makubwa na Kwa muda mfupi Kwa nchi yake kama Hayati JPM Kwa mjibu wa katiba Yetu, hayupo!

Watapata tabu sana kufikia kiwango chake wote wanaomfuata.
 

Mwanzi1

JF-Expert Member
Sep 19, 2016
6,005
2,000
Kwani jeshi wakitaka kutumia uwanja wa wowote wa ndege Tanzania watashindwa?
 

kalonji

JF-Expert Member
Feb 17, 2021
6,198
2,000
Ushauri wako ni mzuri mno, ila mimi bado nasema hivi tulifikiri nini hadi tukaamua kujenga uwanja huu mkubwa hivi kwa kutumia ma-billioni ya hela kule kijijini? tuanzie ha hapa kwanza - unajua huwezi kutatua tatizo bila kujua chanzo chake.
Tuanze upya aliyefikiria hivyo hayupo
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom